- Africa Cup of Nations Januari 14 2026 dakika 120 wanaume kazini
- Morocco 4-2 Nigeria AFCON 2025 wakitinga fainali kwa ushindi wa penati.
- Senegal vs Morocco fainali ya AFCON 2025 Januari 18,2026.
Morocco 4-2 Nigeria AFCON 2025 hatua ya nusu fainali. Yassine Bounou mlinda mlango wa Morocco alikuwa shujaa kwa kuokoa penati mbili za wachezaji wa Nigeria. Wababe hawa ilibidi mshindi apatikane kwa penati baada ya dakika 120 ubao kusoma 0-0. Ushindi huo unaipeleka hatua ya fainali na inatarajiwa kucheza na Senegal kusaka bingwa wa Afrika.
Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Morocco 4-2 Nigeria AFCON 2025

Wakati ushindi wa Morocco 4-2 Nigeria AFCON 2025 ukiwapeleka wenyeji fainali rekodi nyingi zimeandikwa. Ni mchezo uliokuwa umebeba hisia za wengi kutokana na ukubwa wake. Burudani ilikuwa inashuhudiwa kutoka Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Rabat. Dakika 90 ilikuwa Nigeria 0-0 Morocco, dakika 30 ilikuwa Nigeria 0-0 Morocco.
Bounou aliokoa penalti mbili kupitia kwa Samuel Chukwueze na Bruno Onyemaechi kwenye mchezo uliokuwa na presha kubwa mwanzo mwisho. Mwamuzi wa kati alikuwa Daniel Laryea kwenye mchezo huo wa nusu fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa. Fainali Itakuwa ni Senegal vs Morocco, Januari 18 2026.
Takwimu za mchezo
| Nigeria | Morocco | |
| 2 | Mashuti | 16 |
| 1 | Lenga lango | 5 |
| 51% | Umiliki | 49% |
| 29 | Faulo | 19 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 2 | Kadi za njano | 0 |
| 1 | Kona | 5 |
| 120 | Dakika | 120 |
Morroco rekodi
Vijana wa Nigeria chini ya Kocha Mkuu, Eric Chelle malengo ya kufika fainali yameishia hatua ya nusu fainali. Nu Walid Regragui Kocha Mkuu wa Morocco timu yake inakwenda hatua ya fainali kuwakabili Senegal.
Morocco imeandika rekodi yakutofungwa katika jumla ya mechi 26. Kumekuwa na uwekezaji mkubwa katika soka kwa muda wa miaka 10 sasa kupitia kwa mfalme Mohammed VI ikiwa ni sehemu ya utamaduni na mabadiliko katika jamii.
Ikumbukwe kwamba Morocco ni timu ya kwanza kutoka Afrika kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Dunia Qatar 2022. Morocco inatarajiwa kupata ushindani mkubwa vs Senegal yenye Sadio Mane.
SOMA HII: AFCON 2025 matokeo na ratiba hii hapa/ Msimamo, live scores

Takwimu za mchezo wa Senegal vs Misri

| Senegal | Misri | |
| 11 | Mashuti | 4 |
| 4 | Lenga lango | 1 |
| 65% | Umiliki | 35% |
| 10 | Faulo | 11 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 2 | Kadi za njano | 1 |
| 6 | Kona | 1 |
| 1 | Otea | 1 |
Matokeo ya hatua ya nusu fainali AFCON 2025
| Senagel | 1 | 0 | Misri |
| Nigeria (2 P) | 0 | 0 | (4 P) Morocco |

