- Coastal Union 0-1 Yanga SC ni matokeo yaliyopita Desemba 7,2025 kabla ligi kusimama.
- Yanga SC hawana utani wamerejea kazini maandalizi ya mechi zijazo msimu wa 2025/26
- Bakari Nondo, Job, Mohamed Mohamed ni miongoni mwa wachezaji waliopo Misri maandalizi ya AFCON
Yanga SC hawana utani wamerejea kazini baada ya mapumziko. Mabingwa hao watetezi wameanza mazoezi ikiwa ni maandalizi kwa mechi zijazo msimu wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba mchezo wa mwisho kushuka uwanjani ilikuwa ugenini Coastal Union 0-1 Yanga SC. Goli la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Prince Dube.
SOMA HII: Ligi Kuu Bara NBC: Yanga SC haikamatiki, Azam yaichakaza Simba SC
Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC hawana utani wamerejea kazini mapema

Benchi la ufundi la Yanga SC hawana utani wamerejea kazini kujinoa kwa mechi zijazo. Ikumbukwe kwamba ligi ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora imesimama kwa muda. Sababu za ligi kusimama ni kupisha AFCON 2025 itakayofanyika Morocco.
Kutoka kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pedro Goncalves wapo wachezaji walioitwa katika majukumu ya taifa. Wachezaji wa Yanga SC walioitwa timu ya Tanzania ni Bakari Nondo, Mohamed Hussen, Ibrahim Bacca. Beki wa kati Dickson Job naye yupo kwenye orodh chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Timu ya Tanzania imeweka kambi nchini Misri. Hayo ni maandalizi kuelekea AFCON 2025 kabla ya kukwea pipa kueleka Morocco. Jambo hilo ni sababu ya ligi kusimama hali iliyopelekea wachezaji kupewa mapumziko.
SOMA HII: Kocha mpya Simba SC jina mezani/ Kocha Yanga SC CV zake zatua Msimbazi, utambulisho wapangwa

Mapumziko muda wake umeisha Yanga SC

Kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano Yanga SC, Ali Kamwe alibainisha wachezaji walipewa mapumziko. Hao ni wale ambao hawakuitwa katika majukumu ya taifa. Mwisho wa mapumziko ilikuwa ni Desemba 15,2025.
“Benchi la ufundi limetangaza mapumziko kuanzia Desemba 7 mpaka Desemba 15, wakirejea Desemba 15 watafanya mazoezi mpaka Desemba 20 kisha watapumzika tena mpaka Desemba 28.
“Wachezaji watapata fursa ya kwenda kusherehekea sikukuu na familia zao, kabla ya kurejea tena mazoezini Desemba 29 kwa ajili ya maandalizi na wote tunafahamu kuwa mwezi Januari tuna mechi za kimataifa pamoja na za nyumbani kwa kutegemea ratiba ya bodi ya ligi itakavyopangwa,” alisema Kamwe.
SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF Champions League/ Live scores

Kazi imeanza namna hii
Wachezaji wa Yanga SC ikiwa ni pamoja na Dennis Nkane, Yao, Israel Mwenda, Edmund John wameanza mazoezi. Chini ya benchi la ufundi wamekuwa na program tofautitofauti. Leng oni kuzidi kuwa imara.
Wachezaji hao Desemba 16, 2025 walikuwa na program ya GYM. Kurejesha uimara baada ya kuwa nyumbani kwa muda. Hata hivyo ratiba inaonyesha kuwa hawatakaa muda mrefu kambini wataivunja kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mchezo wa mwisho kwa Yanga SC
Mabingwa hao watetezi wa ligi hawajapoteza mchezo mpaka sasa. Desemba 7, 2025 walivuna pointi tatu ugeneni. Ilikuwa Coastal Union 0-1 Yanga SC goli la Prince Dube.
Matokeo hayo yanafanya Yanga SC kufikisha jumla ya pointi 16. Ni mechi 6 timu hiyo imecheza ndani ya msimu wa 2025/26.
Msimamo 5 bora NBC
- JKT Tanzania pointi 17 mechi 10
- Yanga SC pointi 16 mechi 6
- Pamba Jiji FC pointi 16 mechi 9
- Mashujaa FC pointi 13
- Simba SC pointi 12 mechi 5
Hitimisho
Yanga SC hawana utani wamerejea kazini kujinoa kwa mechi zijazo kimataifa na kitaifa. Timu hiyo imecheza mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi. Ushindi ni mchezo mmoja ikiwa nyumbani na sare mchezo mmoja ugenini.

