Real Madrid vs Celta VigoReal Madrid vs Celta Vigo
  • Ligi Kuu nchini Uhispania itaendelea leo Jumapili, kwa mechi kadhaa kupigwa.
  • Real Madrid vs Celta Vigo ni miongoni mwa mechi bora ambazo zitafuatiliwa zaidi.
  • Mchezo huu utapigwa dimbani Santiago Bernabeu, ikiwa ni mchezo wa kwanza baada ya mechi 6 mfululizo ugenini.

Ligi Kuu nchini Uhispania itaendelea leo Jumapili kwa mechi kadhaa kupigwa. Miongoni mwa mechi bora ambazo zitafuatiliwa zaidi ni mchezo wa Real Madrid vs Celta Vigo. Mchezo huu utapigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu, ikiwa ni mchezo wa kwanza baada ya mechi sita mfululizo ugenini.

SOMA HII PIA: La Liga Table 2025/26

Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Real Madrid vs Celta Vigo: Live Score, h2h, lineups, utabiri

Timu hizi zimekutana mara 57 katika historia yao, ambapo Real Madrid wameshinda mechi 39. Celta Vigo wao wamefanikiwa kushinda mechi 12 tu, Huku mechi sita zikiisha kwa matokeo ya sare. Katika michezo 5 iliyopita walipokutana, Real wameshinda mech izote na hawajapotezamchezo wowote kati ya mechi 19 zilizopita walipokutana.Mechi ya mwisho kukutana ilikuwa Mei 4, mwaka huu ambapo Real walishinda magoli 3-2.

Mechi 5 zilizopita za Real Madrid

Athletic Club 0–3 Real Madrid – 3/12/25

Girona 1–1 Real Madrid – 30/11/25

Olympiacos 3–4 Real Madrid – 26/11/25

Elche 2–2 Real Madrid – 23/11/25

Rayo Vallecano 0–0 Real Madrid – 9/11/25

Kikosi kinachotarajiwa cha Real Madrid

Kikosi cha Madrid (-)
Kikosi cha Madrid

Kipa: Courtois

Walinzi: Asencio, Militão, Rüdiger, Carreras

Viungo: Valverde, Tchouaméni, Güler, Bellingham

Washambuliaji: Vinicius Junior, Mbappé.

SOMA HII PIA: PSG vs Real Madrid Julai 9 2025 live: H2H, Vikosi, utabiri, habari za timu

Mechi 5 zilizopita za Celta Vigo

Sant Andreu 1–1 (6–7 pen) Celta Vigo – 4/12/25

Celta Vigo 0–1 Espanyol – 30/11/25

Ludogorets Razgrad 3–2 Celta Vigo – 27/11/25

Alavés 0–1 Celta Vigo – 22/11/25

Celta Vigo 2–4 Barcelona – 9/11/25

Kikosi Kinachotarajiwa cha Celta Vigo

Kikosi cha Celta Vigo
Kikosi cha Celta Vigo

Kipa: Radu

Walinzi: J. Rodríguez, Starfelt, Alonso

Viungo: Rueda, Beltrán, Román, Carreira

Washambuliaji: Aspas, Iglesias, Zaragoza.

Dondoo muhimu kuhusu Real Madrid vs Celta Vigo

Kabla Real Madrid hawajapapatuana na Man City katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lazima wakabiliane na Celta Vigo. Los Blancos ambao walikuwa wakiongoza msimamo kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya Barcelona, waliangukia pua na kutoa sare dhidi ya Rayo Vallecano, Elche na Girona mwishoni mwa Novemba. Hii iliwafanya waporomoke kutoka kwenye uongozi wa msimamo.  

Celta Vigo pia wanaingia kwenye mchezo huu bila kuwa na form nzuri. Kikosi cha, Claudio Giráldez kimekusanya pointi tatu katika mechi moja tu kati ya tano zilizopita katika mashindano yote. Zaidi ya hapo, wageni hawajawahi kuifunga Real Madrid tangu 2017.

Hata hivyo, Madrid amba ni mabingwa wa Ulaya mara 15, hawawezi kumdharau mpinzani yeyote kutokana na ushindani mkali na Barcelona kutafuta ubingwa wa Hispania.

Taarifa za majeruhi

Real Madrid vs Celta Vigo
Kuhusu Trent

Trent Alexander-Arnold anarudi katika wodi ya majeruhi baada ya kupata jeraha la paja katikati ya wiki. Anatarajiwa kukaa nje kwa miezi miwili, akijiunga na Dani Carvajal na Ferland Mendy ambao watarejea mwaka 2026.

Eduardo Camavinga pia ana jeraha la kifundo cha mguu alilopata dhidi ya Athletic Club. Ingawa halionekani kuwa kubwa, anaweza kukosa mechi ya leo, kama ilivyo kwa Dean Huijsen na David Alaba.

Kutokana na jeraha la Camavinga, Alonso atamtegemea Federico Valverde kuchukua nafasi yake, huku beki wa kati Raúl Asencio akitarajiwa kucheza kama beki wa kulia.

Tofauti na Real Madrid, sehemu kubwa ya kikosi cha Celta Vigo kipo kamili. Ni Mihailo Ristić na Joseph Aidoo tu, ndio ambao wanachunguzwa kufuatia majeraha. Aidoo alicheza dakika 11 tu, dhidi ya Sant Andreu kabla ya kuumia na anatarajiwa kukosa safari ya kwenda Madrid.

Wachezaji wengi muhimu watarudi kikosini. Hii ni baada ya kupumzishwa kwenye mechi ya Kombe la Mfalme, katikati ya wiki. Shinikizo litakuwa kwa Borja Iglesias, ambaye hajapata magoli mengi amefunga mabao mawili katika mechi 11 zilizopita.

SOMA HII ZAIDI: BARCELONA VS REAL MADRID 26/4/2025, USO KWA USO FAINALI COPA DEL REY

Hitisho: Utabiri wa Matokeo Real Madrid vs Celta Vigo

Real Madrid vs Celta Vigo unatarajiwa kuwa mchezo wa ushindani. Licha ya kwamba Madrid hawako katika kiwango chao cha juu, lakini kurejea kucheza nyumbani baada ya mechi sita mfululizo ugenini kutawapa motisha kubwa. Celta Vigo wana nafasi ya kufanya jambo kuzingatia safu ya ulinzi ya Madrid iliyodorora, hasa mlinzi Asencio ambaye amyekuwa na makosa mengi. Hata hivyo, Real na kasi ya Mbappe vinawapa nafasi kubwa zaidi ya ushindi.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.