Yanga SC vs Fountain Gate FCYanga SC vs Fountain Gate FC
  • Nyota wa Yanga SC, Dube na Pacome Zouzoua leo Alhamisi walikuwa mwiba mkali.
  • Nyota hao wameifungia Yanga SC mabao muhimu yaliyowawezesha timu hiyo, kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate.
  • Mchezo huu amba ni mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya NBC ulipigwa kwenye Uwanja wa KMC.

Mastaa wawili wa Yanga SC, Pacome Zouzoua na straika Prince Dube leo Alhamisi walikuwa mwiba mkali, hivyo kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate. Hii ni katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya NBC. Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulipigwa kwenye Uwanja wa KMC.

SOMA HII PIA: UTATA MTUPU ISHU YA BRUNO NA DUBE 2023/24

Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu magoli ya Dube na Pacome kwenye ushindi wa Yanga SC 2-0 Fountain Gate FC

Dube X Pacome
Dube X Pacome

Wakirejea kutoka Algeria na wakiwa hawajapata muda mrefu sana wa kupumzika kutokana na urefu wa safari, Yanga walipaswa kuhakikisha hawatoki nje malengo yao. Hivyo Wananchi wameendelea kuthibitisha ubora wao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Hii ni baada ya kupata ushindi muhimu wa mabao 2–0 dhidi ya Fountain Gate FC. Mchezo huo umepigwa leo Desemba 4, 2025, jijini Dar es Salaam. Ushindi huo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Yanga SC nchini, umeonyesha tena ubora wa kikosi cha timu hiyo.

SIMA HII ZAIDI: Mfungaji bora 2024/25 Jean Ahoua ataivunja rekodi yake? Pacome, Prince Dube kwenye mtihani

Mchezo ulikuwaje?

Ecua vs Fountain Gate FC
Ecua vs Fountain Gate FC

Mara tu baada ya filimbi ya mwamuzi kusikika Yanga SC walianza kwa kishindo, walionesha nia ya kutawala mchezo. Hii ilifanyika kupitia mfumo wao wa kasi, na mashambulizi ya kupangiliwa vizuri. Eneo la kati ya Uwanja chini ya kiungo Duke Abuya walihakikisha wanadhibiti mchezo.

Viungo hao walisukuma mipira mbele kwa washambuliaji, hii iliifanya safu ya ulinzi ya Fountain Gate ipate wakati mgumu kuzuia mashambulizi ya Wananchi. Licha ya Fountain Gate kujaribu kupooza mashambulizi ya Yanga SC, presha ya wenyeji ilionekana kuwazidi.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa katika kipindi cha kwanza kupitia mkwaju wa penalty, baada ya Mlinzi wa Fountain Gate FC kunawa mpira ndani ya eneo la hatari. Mkwaju huo uliwekwa kimiani na straika, Prince Dube na kuipa Yanga SC uongozi uliowapa utulivu na kuwatia Fountain Gate presha ya kutafuta kusawazisha.

Fountain wajibu mapigo

Fountain Gate walijitahidi kuingia kwenye mchezo dakika za mapema katika kipindi cha pili kwa kuweka nguvu kwenye mashambulizi ya kushtukiza. Jitihada hizo ziligonga mwamba kwani safu ya ulinzi ya Yanga SC ilikuwa imara na yenye umakini. Golikipa wa Yanga alifanya kazi kubwa, akiokoa michomo kadhaa hatari ambayo huenda ingewarudisha Fountain Gate mchezoni.

Huku dakika zikiendelea kuyoyoma, Yanga walizidi kuimarisha umiliki wa mpira. Katika dakika za mwisho kabisa, walipata bao la pili kupitia mpira wa kutengenezwa vizuri uliotoka kwa kiungo Duke Abuya, na kumaliziwa kwa ustadi na Pacome hivyo kumshinda kipa wa Fountain Gate. Bao hilo lilizima kabisa matumaini ya wageni kurudi mchezoni na kuhakikisha Yanga wanaondoka na pointi tatu muhimu.

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League/ Prince Dube afunga goli la ushindi New Amaan Complex

Yanga SC yaendeleza rekodi

Msimamo wa Ligi
Msimamo wa Ligi

Ushindi huu ni muhimu kwa Yanga kwani unaendeleza rekodi yao nzuri msimu huu, huku ukiwapa morali ya kuikabili ratiba iliyosongamana kuelekea mwisho wa mwaka. Ikumbukwe Yanga hawajapoteza mchezo wa ligi mpaka sasa, kati ya michezo waliyocheza. Yanga wamecheza mechi 5, wameshinda mechi 4 na kutoa sare mechi moja.

Kocha Yanga SC awasifu mastaa wake

Dube na Pacome
Abuya-Mchezaji bora wa mechi

Mara baada ya mchezo huo, Kocha wa Yanga SC, Pedro amesema amefurahishwa na nidhamu ya wachezaji wake. Kocha huyo pia ameahidi kuwa timu itaendelea kufanya kazi kwa bidii, ili kuhakikisha inawapa mashabiki wao matokeo bora. Ikumbukwe ushuindi huu umeifanya Yanga kufikisha pointi 13.

Hitimisho

Mechi hii Yanga SC vs Fountaina Gate FC imeonyesha kuongezeka kwa ushindani kwa ujumla. Licha ya ushindani huo bado ubora wa kikosi cha Yanga SC umeendelea kuwa nguzo kuu ya matokeo bora. Hii ni licha ya ugumu wa ratiba inayowakabili ya mashindano ya ndani na kimataifa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.