Matokeo ya CAF Champions League 2025/26Mpanzu CAF
  • CAF Champions League 2025/26 matokeo ya raundi ya kwanza na pili yote yapo hapa.
  • Stade Malien 2-1 Simba SC, kadi nyekundu kwa Allasane Kante yatibua mipango ya Dimitar Pantev.
  • JS Kabylie 0-0 Yanga SC, St Eloi Lupopo 1-1 Al Hilal Omdurman.

Matokeo ya CAF Champions League 2025/26 ni moto wa kuotea mbali kila timu inasaka ushindi. Kuna mechi 6 hatua ya makundi nyumbani tatu na ugenini tatu. Tayari ni mechi mbili zimechezwa zikisalia mechi nne kupata timu mbili zitakazotinga robo fainali. Haya hapa matokeo ya mechi za  raundi mbili.

SOMA HII: Simba SC 0-1 Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26/ Highlights, stats, match report

Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

image

Kamata matokeo ya CAF Champions League 2025/26 utashangazwa

Hakuna kulala, matokeo ya CAF Champions League 2025/26 kila dakika msimamo unabadilika. Hii inatokana na ushindani uliopo. Kuna timu ambazo zimeambulia kipigo mechi mbili mfululizo zikiongozwa na Simba SC ya Tanzania.

Matokeo ya CAF Champions League 2025/26
Simba SC ugenini mchezo wa CAD Champions League. Source: Simba SC.

Haya hapa mataokeo ya raundi ya pili

Novemba 30,2025
St Eloi Lupopo 1-1 Al Hilal Omdurman
Magoli yamefungwa na Henock Molia dakika ya 79 Kea St Eloi Lupopo na dakika ya 12 kwa Al Hilal Omdurman kupitia Abdelrazing Abderraouf Omer.

Stade Malien 2-1 Simba SC
Magoli yamefungwa na Taddeus Nkeng dakika ya 16 na Ismaila Simpara dakika ya 23 kwa Stade Malien huku Neo Maema alifunga dakika ya 54 kwa Simba SC.

Kiungo Alassane Kante alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 82 kwa kucheza faulo mbaya kwa mpinzani wa Stade Malien.

SOMA HII: Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League/ Prince Dube afunga goli la ushindi New Amaan Complex

image

Novemba 29,2025
Petro de Luanda 1-1 Esperance ST
Magoli yakifungwa na Tiago Reis dakika ya 49 kwa Petro de Luanda na Abounacar Diakite dakika ya 89 kwa Esperance ST.

Power Dynamo 0-1 Pyramids

Goli la Pyramids likifungwa na Mohamed Reda dakika ya 51.

Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League
Diarra kipa namba moja wa Yanga SC 2025/26.

November 28, 2025

JS Kabylie 0-0 Yanga SC

Rivers United 1-2 RS Berkane
Magoli yakifungwa na Mamadou Lamine Camara dakika ya 37 kwa Rivers United huku Mounir Chouiar akifunga dakika ya 90+9 na lile la usawa dakika ya 90+7 na Youness El Kaabi.

AS Far Rabat 1-1 Al Ahly

Magoli yakifungwa na Mouhcine Bouriga dakika ya 37 kwa mkwaju wa penalti kwa AS Far Rabat na Mahmoud Trezeguet dakika ya 68 kwa Al Ahly.

MC Alger 0-0 Mamelodi Sundowns

Novemba 21,2025

Al Hilal Omdurman 2-1 MC Alger
Magoli yalifungwa na Mohamed Raman dakika ya 75 na Abdelrazing Omer dakika ya 45 lile la MC Alger ni Mustafa Karshoum alijifunga dakika ya 53.

Matokeo ya CAF Champions League raundi ya kwanza

JS Kabylie vs Yanga SC CAF Champions League leo Novemba 28,2025
Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Simba SC 2025/26. Source: Yanga SC.

Novemba 22,2025
Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat
Goli la Yanga SC limefungwa na Prince Dube dakika ya 58

Mamelodi Sundowns 3-1 St Eloi Lupopo
Magoli yamefungwa na Nuno Santos dakika ya 4 na 77, Marcelo Allende dakika ya 61 lile la St Eloi Lupopo limefungwa na Ramos Kashala Wanet dakika ya 44.

Al Ahly SC 4-1 JS Kabylie
Magoli mchezo ya Al Ahly yamefungwa na Mahmoud Trezeguet dakika ya 36 na 84, Mohamed Sherif dakika ya 39 na Mohamed Hadid dakika ya 90+3. Lile la JS Kabylie ni Mohamed El Shenawy dakika ya 90.

Esperance ST 0-0 Stade

RSB Berkane 3-0 Power Dynamo
Magoli ya RSB Berkane yamefungwa na Paul Bassene dakika ya 65, Mounir Chouiar dakika ya 16 na lile la ufunguzi ni Aaron Katebe dakika ya 13.

Pyramids 3-0 Rivers United

Magoli Ahmed Atef Otta dakika ya 72, 57 na dakika ya 52.

Novemba 23,2025
Simba SC 0-1 Petro de Luanda
Goal Benny dakika ya 78 pasi ya Tiago Reis.

SOMA HII: Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League, Azam FC yapoteza / Highlights, magoli

image

Hitimisho

Matokeo ya CAF Champions League 2025/26 yamewaliza wengi na wapo ambao wamecheka. Mashabiki wa Simba SC huzuni inaendelea kwa kuwa mechi zote walipoteza. Je mnyama ataendelea kugawa pointi kwenye mechi nne zilizobaki? Jibu litapatikana raundi ya tatu.

Share this: