- Leo 30 Novemba 2025, imekuwa siku kubwa kwa Wanamsimbazi.
- Hii ni kufuatia ratiba ya matukio makubwa, ikiwemo Mkutano mkuu wa Simba SC wa mwaka, ambao umefanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
- Pamoja na mkutano mkuu huo, pia Mnyama alishuka uwanjani katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Stade Malien vs Simba SC.
Leo Jumapili, 30 Novemba 2025, klabu ya Simba SC imefanya mkutano wao mkuu wa mwaka katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Mkutano huo wa kikatiba uliwakutanisha wanachama na viongozi wa Simba SC. Lengo kuu la mkutano huu kwa kawaida huwa, ni kujadili ripoti ya mapato na matumizi ya msimu uliopita, pamoja na kuthibitisha bajeti na mpango wa fedha kwa msimu wa 2025/2026. Haya hapa ni baadhi ya mambo mazito yaliyoibuka kwenye mkutano huo.
SOMA HII PIA: Simba SC vs RS Berkane CAF waipeleka Uwanja wa Amaan, Mei 25 2025 fainali ya maamuzi
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Bajeti ya Bilioni 29.5 yatajwa Mkutano mkuu wa Simba SC

Katika mkutano huu, kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Simba SC, Suleiman Kahumbu, uongozi wa timu hiyo umeweka bajeti ya shilingi bilioni 29,555,207,704 kwa mwaka ujao wa fedha. Katika bajeti hii, inatarajiwa klabu kufanya matumizi ya shilingi bilioni 27,161,824,254. Hii ni ongezeko la bajeti kwa asilimia 13.5 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka uliopita.
SOMA HII ZAIDI: Kizungumkuti Yanga SC vs Simba SC Kariakoo Dabi/ Mechi ipo au haipo?
MO bado anaibeba Simba SC
Katika ripoti hiyo mfadhili na mwekezaji wa Simba SC, Mohamed Dewji, ameendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye bajeti ya msimu huu. Kahumbu alibainisha kuwa Dewji alichangia kiasi cha shilingi bilioni 4 katika bajeti ya mwaka uliopita. Katika bajeti ya sasa amechangia angalau shilingi bilioni 6.
Serikali yatoa msimamo mzito, kuhusu mabadiliko ya uendeshaji

Katika Mkutano mkuu wa leo, ulihudhuriwa na baadhi ya wageni waalikwa, wageni hawa ni maafisa wa serikali, pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali. Mmoja wa wageni mashuhuri aliyefika ni, Hamis Mwinjuma maarufu ‘Mwana FA’, ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Katika hotuba yake Naibu Waziri FA alisisitiza kuwa serikali haitalazimisha klabu yoyote nchini, ikiwemo Simba kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji bila idhini ya wanachama wake.
Aliendelea kusema Jukumu la serikali, ni kuhakikisha mchakato wowote unaotekelezwa unazingatia sheria za nchi na kanuni zinazowezesha usalama na uwazi wa michezo. Hivyo hatima ya mabadiliko ya uendeshaji wa Simba ipo mikononi mwa wanachama. Ikiwa watakubali kuendelea, kutathmini upya, au kubadili mwelekeo basi maamuzi yataheshimiwa. Kiongozi huyo alisisitiza kuwa Serikali ina matumaini kwamba mjadala utafanyika kwa busara, sio hisia, na katika maslahi mapana ya klabu na maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu nchini.
Mtafaruku waibuka ukumbini

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi ndani ya ukumbi huo, kulizuka sintofahamu miongoni mwa wanachama kuhusu mchakato wa uwekezaji. Hii ni baada ya baadhi ya wanachama kuwa na maoni mseto juu ya wawekezaji gani, wanaweza kuongoza timu hiyo. Wapo ambao walitoa maoni juu ya kumuamini mwekezaji wa muda mrefu wa timu hiyo Mohammed Dewji huku wengine wakionyesha mashaka.
Wale waliionyesha mashaka walihoji juu ya uwezekano wa wafadhili wengine kupewa nafasi ya kuwekeza fedha zao. Mawazo hayo ni kwa kuwa wanaamini huenda hiyo inaweza kuwatoa sehemu moja na kwenda mbele zaidi. Ikumbukwe kumekuwepo tetesi za wawekezaji wengine kupewa timu.
SOMA HII PIA: SIMBA YASHUSHA STRAIKA MPYA MCAMEROON KIMYAKIMYA
Hitimisho

Licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza, lakini mkutano mkuu wa leo wa Simba SC, 30 Novemba 2025, unaweza kuchukuliwa kama mwanzo wa sura mpya kwa klabu. Hii ni katika kuonyesha dhamira ya mageuzi, uwajibikaji, na usimamizi wa kisasa. Kupitishwa kwa bajeti mpya, michango ya mfadhili mkuu, na msimamo wa serikali kuunga mkono mchakato kwa heshima ya maamuzi ya wanachama, yote haya ni ishara chanya. Tusubiri na kuona hatua za mbeleni kwao.

