- Highlights Novemba 28, 2025 JS Kabylie 0-0 Yanga SC mechi ya pili kati ya 6 kundi B.
- Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League 2025/26.
- Azam FC 0-1 Wydad Casablanca Caf Cofideration Cup, Aziz Ki akimbizwa hospital.
Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League 2025/26. Waarabu wa Algeria walikuwa wanapewa nafasi kushinda hatua ya makundi, Uwanja wa Hocine Ait Ahmed na matokeo rasmi 0-0. Wakati Yanga SC ikipata pointi moja ugenini, Azam FC 0-1 Wydad Casablanca CAF Cofideration Cup. Matajiri wa Dar wamepoteza wakiwa nyumbani.
SOMA HII: Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League/ Prince Dube afunga goli la ushindi New Amaan Complex
Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League kimkakati

Licha ya kuwa ugenini, Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League mbele ya mashabiki wao. Pedro Goncalves, Kocha Mkuu wa Yanga SC aliwaruhusu wapinzani kumiliki mpira.Waarabu wa Algelia waliliandama lango mithili ya nyuki waliambulia patubu.
| JS Kabylie | Yanga SC | |
| 63% | Umiliki wa mpira | 37% |
| 16 | Mashuti yaliyopigwa | 11 |
| 6 | Mashuti yaliyolenga lango | 3 |
| 7 | Kona | 0 |
| 0 | Kadi nyekundu | 0 |
| 3 | Kipa okoa hatari | 6 |
| 1 | Kadi ya njano | 2 |
SOMA HII: Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025: Kazi imeanza, Wananchi watoa tamko zito

Kikosi cha JS Kabylie kilichoanza vs Yanga SC
Mlinda mlango
Hadid
Mabeki
Hamid
Madani
Belaid
F.Nechat
Viungo
Boudjemaa
Babar Sarr
Boudebouz
Washambuliaji
L.Akhrib
Mahious
Merghem
Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya JS Kabylie
Mlinda mlango
Diarra
Mabeki
Zimbwe Jr
Hamad Bacca
Dickson Job
Israel Mwenda
Viungo
Maxi Nzengeli
Duke Abuya
Pacome Zouzoua
Mudathir Yahya
Ecua
Mshambuliaji
Prince Dube
Matokeo na mechi ijayo
JS Kabylie 0-0 Yanga SC, Novemba 28,2025.
Yanga SC vs JS Kabylie, Februari 13,2026.
Msimamo wa kundi B CAF Champions League

| Timu | Mechi | Pointi | Shinda | Sare |
| 1. Al Ahly | 2 | 4 | 1 | 1 |
| 2.Yanga SC | 2 | 4 | 1 | 1 |
| 3. AS Far Rabat | 2 | 1 | 0 | 1 |
| 4. JS Kabylie | 2 | 0 | 0 | 1 |
SOMA HII: JS Kabylie vs Yanga SC CAF Champions League Novemba 28/ Lineups, H2H, livescore

Azam FC 0-1 Wydad Casablanca CAF Cofederation Cup

Wawakilishi wa Tanzania kwenye CAF Cofideration Cup, Azam FC wamepoteza pointi sita. Kwenye mechi mbili walizoshuka uwanjani ugenini na nyumbani walipoteza. Mchezo wa Novemba 28,2025 ulikuwa ni wapili kwa Azam FC.
Florent Ibenge Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji walijitoa kwa asilimia kubwa licha ya kukosa matokeo kwenye mchezo wao wa pili. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ulisoma Azam FC 0-1 Wydad Casablanca ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi.
Bao la ushindi lilifungwa na Nordin Amrabat dakika ya 57 kipindi cha pili lilidumu mpaka mwisho wa mchezo ikiwa ni mechi ya pili Azam FC kupoteza baada ya kuanza ugenini kufungwa 2-0 dhidi ya AS Maniema.
Ibenge amesema wachezaji walifanya kazi kubwa ndani ya uwanja wanastahili pole licha ya kukwama kupata ushindi.
“Ninaweza kusema pole kwa wachezaji kwa kuwa walikuwa katika mchezo mzuri, walikimbia sana na mwisho tumekosa matokeo hivyo makosa tutafanyia kazi kwa mechi zijazo,”.
Msimamo wa kundi B Caf Confideration Cup 2025/26
| Timu | Mechi | Pointi | Shinda | Sare |
| 1. Wydad Casablanca | 2 | 6 | 2 | 0 |
| 2. Maniema Union | 1 | 3 | 1 | 0 |
| 3. Azam FC | 2 | 0 | 0 | 0 |
| 4. Nairobi United | 1 | 0 | 0 | 0 |
Ni timu mbili ambazo zitamaliza nafasi za juu zitasonga mbele hatua ya robo fainali. Ikitokea timu zikawa sawa katika pointi hapo mshindi atatazamwa kupitia h2h dhidi ya timu wanayolingana pointi. Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Kwenye mchezo wa jana kiungo Aziz Ki mara baada ya mchezo kukamilika alipatwa na tatizo ma kuwahishwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Hitimisho
Yanga SC yaibana mbavu JS Kabylie CAF Champions League 2025/26 ikiwa ugenini. Ni mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa katika hatua ya makundi. Matokeo hayo yanawafanya wanajangwani kuwa kwenye nafasi nzuri kutinga hatua ya makundi. Kutoka kundi B la CAF Champions League ni Al Ahly na Yanga SC zinapewa nafasi kupenya.

