Chelsea vs ArsenalChelsea vs Arsenal
  • Vita ya ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL), itaendelea tena wikiendi hii kwa mechi kali ya London Derby.
  • Chelsea vs Arsenal Uwanja wa Stamford Bridge, hapa hatumwi mtoto dukani.
  •  Timu zote zitaingia katika mchezo huu baada ya matokeo ya ushindi mkubwa kwenye masghindano ya UEFA Champions League.
  • Arsenal wametoka kuichapa Bayern Munich 3-1, huku Chelsea wao wakiwakanda Barcelona 3-0.

EPL inaendelea tena wikiendi hii kwa mechi kali, huku macho yote yakiwa kwenye mchezo mkubwa wa ‘London derby’ ambapo Chelsea watakuwa wenyeji wa Arsenal. Chelsea vs Arsenal ni dabi ambayo kwa mara ya kwanza katika historia ilipigwa mwaka 1907. Timu zote mbili zinauendea mchezo huu zikitoka kushinda dhidi ya timu vigogo Ulaya amba oni Barcelona na Bayern Munich.

SOMA HII PIA: Arsenal vs Chelsea: Preview, Team News, H2H & Prediction

Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Chelsea vs Arsenal

Eze
Eze

Tangu kuanza rasmi kwa dabi hii ya London mwaka 1907, Chelsea na Arsenal zimekutana mara 74. Katika michezo hiyo Chelsea imeshinda mechi 25, Arsenal wameshinda mechi 28. Mechi 21 kati ya hizo zilimalizika kwa matokeo ya sare. Haya hapa matokeo ya mechi zao tano zilizopita;

Arsenal 1-0 Chelsea (March 16, 2025)

Chelsea 1-1 Arsenal (November 10, 2024)

Arsenal 4-0 Chelsea (April 23, 2024)

Chelsea 2-2 Arsenal (October 21, 2023)

Arsenal 3-1 Chelsea (May 2, 2023).

SOMA HII ZAIDI: arsenal vs Chelsea- Ni Dabi ya London.

Mechi 5 zilizopita za Chelsea

25 Nov Chelsea 3-0 Barcelona

22 Nov Burnley 0-2 Chelsea

8 Nov Chelsea 3-0 Wolverhampton Wanderers

5 Nov Qarabag FK 2-2 Chelsea

1 Nov Tottenham 0-1 Chelsea

Mechi 5 zilizopita za Chelsea

26 Nov Arsenal 3-1 Bayern Munich

23 Nov Arsenal 4-1 Tottenham

8 Nov Sunderland 2-2 Arsenal

4 Nov Slavia Prague 0-3 Arsenal

1 Nov Burnley 0-2 Arsenal

Kikosi tarajiwa cha Chelsea vs Arsenal

Kikosi cha Chelsea (-)
Kikosi cha Chelsea

Kipa: Sanchez

Walinzi: James, Chalobah, Tosin, Cucurella

Viungo: Gusto, Caicedo, Neto, FernandezM, Garnacho

Mshambuliaji: Joao Pedro.

SOMA HII PIA: SPORT
Chelsea FC: Habari za Hivi Karibuni, Ratiba, Taarifa ya Kikosi na Maarifa ya Kubashiri

Kikosi tarajiwa cha Arsenal vs Chelsea

Chelsea vs Arsenal
Kikosi cha Arsenal

Kipa: Raya

Walinzi: Timber, Saliba, Hincapie, Calafiori

Viungo: Eze, Zubimendi, Rice, Saka, Trossard

Mshambuliaji: Merino

Rekodi zinazungumza mengi kuhusu Chelsea vs Arsenal  

Ukweli ni kuwa Chelsea wamekuwa na rekodi bora wakicheza nyumbani msimu huu, 43.5% ya pointi zao za ligi zimepatikana Stamford Bridge.  Ushindi wao wa 3-0 dhidi ya Barca unamaanisha, wamefunga mabao sita bila kuruhusu bao kwenye mechi zao mbili za mwisho nyumbani. Chelsea wamefunga bao katika mechi tano kati ya sita zilizopita za ligi na kushinda mechi tatu mfululizo bila kuruhusu bao, kwa mara ya kwanza tangu Machi 2022.

Chelsea wamepata ushindi mmoja tu, katika mechi zao 11 zilizopita za Ligi Kuu dhidi ya Arsenal. Baada ya kupoteza mechi sita kati ya saba zao ugenini dhidi ya Chelsea kati ya 2013 na 2018, Arsenal hawajafungwa katika mechi sita zilizopita Stamford Bridge. Hii itakuwa mara ya tano kwa Arsenal kukutana na Chelsea wakiwa kileleni mwa ligi.

Arteta agoma kufungwa na Chelsea

Usiku wa Jumatano, Arsenal walipata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Bayern tangu 2015. Pamoja na kuvunja rekodi ya mechi tano bila ushindi, pia walimkaribisha nahodha Martin Odegaard ambaye alikuwa majeruhi. Raia huyo wa Norway alikosa mechi nane kutokana na jeraha la goti, lakini ana rekodi nzuri dhidi ya Chelsea.

Odegaard hajafungwa katika mechi nane dhidi ya Chelsea, ameshinda 6 na kutoa sare 2. Katika mechi hizo amefunga mabao mawili na asisti tano. Hii inamfanya kuhusika moja kwa moja kwenye mabao mengi zaidi ya ligi dhidi ya Chelsea, kuliko timu yoyote nyingine.

Kwa upande wa Arteta dhidi ya Chelsea ana 58.3% ya ushindi dhidi ya Chelsea. Arsenal wamefunga mabao 24 na kuruhusu 13, katika mechi 12 dhidi ya Chelsea tangu Arteta aanze kukinoa kikosi hiko japo kipigo chake cha kwanza kama kocha kilikuwa dhidi ya Blues Desemba 2019.

Hitimisho

Cucu vs Yamal
Cucu vs Yamal

Chelsea vs Arsenal inakwenda kutoa taswira mpya ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England. Kuelekea Jumapili, mpaka sasa kwa mujibu wa tathimini ya Kompyuta maarufu ya utabiri ya Opta Arsenal wanapewa 41.9% ya kushinda, huku Chelsea wakipewa 32.6%. Matokeo ya sare yanatarajiwa kwa 25.5%. Ushindi kwa Chelsea Jumapili utawaweka rasmi kwenye mbio za ubingwa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.