MoriceMorice
  • Stade Malien vs Simba SC ni mchezo ambao unatarajiwa kuangaziwa sana na mashabiki wikiendi hii.
  • Mnyama baada ya kipigo cha kwanza nyumbani, swali ni je, Simba SC itashinda ugenini?
  • Jeshi la mnyama kupaa Alhamisi hii kwenda Mali.

Baada ya kuwa na mwanzo mbaya wa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Petro Atletico, kwenye Ligi ya mabingwa Afrika. Kikosi cha Simba Alhamisi hii kitaanza safari ya kuelekea nchini Mali, kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Stade Malien hatua ya makundi ya Ligi. Stade Malien vs Simba SC ni mchezo huu ni wa pili wa hatua ya makundi kwa timu hizi za kundi D.

SOMA HII PIA: Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto| Matokeo na wafungaji

Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Kuhusu mchezo wa Stade Malien vs Simba SC

Stade Malien vs Simba SC
Rushine

Mchezo huu wa pili wa hatua ya makundi, unatarajiwa kupigwa siku ya Jumapili saa moja jioni, kwa majira ya Afrika Mashariki. Simba wanaobuluza mkia kwenye kundi lao, watakuwa wanasaka ushindi wa kwanza wa hatua ya makundi msimu huu. Stade Malien wao wanakamatia nafasi ya tatu baada ya sare ya mchezo wao wa kwanza vs ES Tunis ugenini.

Simba SC ikipaa, Semaji Ahmed atoa tamko zito

Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi
Ahmed Ally

Kufuatia safari hiyo, Meneja wa Habari na mawasiliano wa Simba SCm, Ahmed Ally amesema: “Mchezo uliopita ulikuwa mwanzo mbaya ambao haupaswi kutukatisha tamaa, wala kutuvunja moyo. Ni mwanzo mbaya ambao unapaswa kutupa nguvu ya kupambana kwa mechi zijazo. Mapambano yanaendelea, hatujawahi kuishia njiani.

“Matokeo tuliyopata dhidi ya Petro yanaumiza, lakini hatuna budi kuyapokea kwa sababu si mambo mageni kwenye mpira. Argentina alifungwa mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la 2022 pale Qatar, dhidi ya Saudi Arabia kila mtu alishangaa. Hawakukata tamaa na wala hawakuvurugana, walijipanga upya, wakasahihisha makosa yao kilichotokea ni historia ya Dunia.

SOMA HII ZAIDI: Simba SC vs Petro de Luanda CAF Champions League funga kazi hatua ya makundi/ Jezi mpya

Ahmed: “Hatupaswi kuvurugana.”

Semaji ameendelea kusema: “Wanasimba wenzangu hatupaswi kuvurugana, wala kukataa tamaa. Bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mechi zijazo. Muhimu ni kurejea katika Uwanja wa mazoezi, kurekebisha tulipokosea na kurejea kwa nguvu kubwa katika uwanja wa mapambano

“Tusijitoe wenyewe kwenye mashindano, tuzungumze yote lakini tusisahau kuwatia moyo wachezaji na kuwapa nguvu watupambanie mechi zijazo. Imani yangu mbele ya Simba hasa kimataifa haijawahi kuyumba. Haijalishi tumeanzaje au tumepoteza mara ngapi, lakini daima mwisho wetu hua ni mzuri.

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho

Kikosi kinachosafiri
Kikosi kinachosafiri

Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa kikosi kimemaliza mazoezi ya mwisho Tanzania leo Jumatano, kesho Alhamisi kikosi kinatarajia kuanza safari kwenda Mali. Kikosi kinatarajiwa kuongozwa na Meneja Dimitar Pantev.

Kikosi cha Simba SC kinachotarajiwa kuanza vs Stade Malien  

Yakoub, Kapombe, Mligo, De Reuck, Camara, Nangu, Mpanzu, Ahoua, Kibu, Kante, Morice

Msimamo wa kundi D

  1. Petro de Luanda pointi 3, mechi 1
  2. Esperance pointi 1, mechi 1
  3. Stade Malien pointi 1, mechi 1
  4. Simba SC pointi 0, mechi 0

Kuhusu kipa Pinpin Camara

Mousa Camara
Mousa Camara

Katika hatua nyingine uongozi wa Simba umetoa taarifa ya maendeleo kuhusu kipa wao namba moja, Pinpin Camara. Kipa huyo alipelekwa nchini Morocco kwa ajili ya matibabu. Taarifa ya Simba imeeleza kuwa: “Golikipa Moussa Camara amekamilisha matibabu yake nchini Morocco na sasa anarejea nchini kwa ajili kusubiri kupona akiwa chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu. Taarifa zaidi kuhusu hali yake zitaendelea kutolewa.”

SOMA HII PIA: Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 haya hapa | Simba SC na Yanga SC zapewa waarabu

Hitimisho

Stade Malien vs Simba SC ni mchezo ambao unatarajiwa kuangaziwa sana wikiendi hii, hii ni kutokana na umuhimu wa matokeo ya mchezo kwa timu zote mbili. Simba hawapaswi kuruhusu kupoteza mchezo huu, ikiwa wanataka kufuzu hatua ya Robo Fainali. Licha ya ubora wao Simba SC pia watapaswa kuchukua tahadhari kubwa za nje na ndani ya uwanja, kuelekea mchezo huu

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.