- Arsenal vs Bayern Munich kinawaka leo kwenye dimba la Emirates, Kaskazini mwa London.
- Mara ya mwisho timu hizi kukutana pale Emirates, matokeo yalikuwa sare ya mabao 2-2.
- Huu utakuwa mchezo wa 15 kwa timu hizo kukutana katika historia ya mashindano rasmi.
- Aprili 17, 2024 ndio mara ya mwisho kukutana ambapo Bayern Munich walipata ushindi wa 1-0.
Mchezo ghali wa mashindano ya UEFA Champions League utapigwa usiku wa leo. Arsenal vs Bayern Munich, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Emirates uliopo Kaskazini mwa jiji la London, utakuwa wa kufa na kupona. The Gunners wameweka rekodi kali ya ushindi wa asilimia 100 mpaka sasa kwenye michuano hii, hii ni baada ya kushinda mechi nne kati ya nne.
SOMA HII PIA: Arsenal vs Liverpool: 1 Premier League Clash Filled with Excitement and Expectations
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

H2H, Arsenal vs Bayern Munich

Timu hizi zimekutana mara 16 katika michezo rasmi ya ushindani ambapo, Bayern Munich wameshinda mechi 8. Arsenal wao wamefanikiwa kushinda mechi 4 pekee, huku mechi 4 zikimalizika kwa matokeo ya sare. Hivyo swali ni je, usiku wa leo nani ataibuka mbabe?
SOMA HII ZAIDI: Bayern Munich vs Borussia Monchengladbach: A Bundesliga Battle of Strategy and Skill
Mechi 5 za mwisho za Arsenal
Arsenal 4-1 Tottenham
Sunderland 2-2 Arsenal
Slavia Prague 0-3 Arsenal
Burnley 0-2 Arsenal
Arsenal 2-0 Brighton
Mechi 5 za mwisho za Bayern Munich
Bayern Munich6-2Freiburg
Union Berlin 2-2 Bayern Munich
PSG 1-2 Bayern Munich
Bayern Munich 3-0 Bayer Leverkusen
FC Köln 1-4 Bayern Munich
Arsenal vs FC Bayern Munich ni vita kali ya rekodi

Bayern Munich ndio vinara wa msimamo wa Champions League, wakiwa na 100% ya ushindi katika michezo minne. Wamewafunga baadhi ya vigogo kama PSG na Chelsea na kuchukua nafasi ya kwanza kwenye msimamo. Mapka sasa wababe hao wa Bundesliga wamefunga mabao 14 mengi kuliko timu zote.
Bayern wanaingia katika mchezo huu wakiwa hawajapoteza mchezo wowote msimu wa 2025-26, tayari wamepata ushindi mara 17 katika mechi zao 18 zilizopita. Kocha Vincent Kompany ameipa Bayern uimara na nguvu kubwa ya kushambulia, na matokeo yanaonekana wazi. Arsenal nao wanaingia wakiwa na utawala wa ligi ya England.
Arsenal Wamefunga mabao 11, wastani wa mabao 2.75 kwa mchezo bila kuruhusu bao lolote, katika michezo ya hivi karibuni. Arsenal wanaingia katika mchezo huu wakiwa na rekodi ya michezo 15 bila kupoteza, wakiwa wameshinda michezo 13, ikiwemo ushindi wa 4-1 dhidi ya Spurs wikiendi iliyopita. Kikosi cha, Mikel Arteta kimejawa na ari ya kufanya vizuri na kwenda mbali msimu huu.
SOMA HII PIA: Arsenal vs Chelsea: Preview, Team News, H2H & Prediction
Kikosi cha Arsenal vs Bayern Munich

David Raya anatarajiwa kuendelea kusimama langoni, huku William Saliba akiiongoza safu ya ulinzi. Martín Zubimendi na Declan Rice watadhibiti eneo la kiungo, huku Leandro Trossard na Bukayo Saka wakibeba majukumu ya kuwalisha washambuliaji. Mikel Merino anatarajiwa kuanza mbele ya mshambuliaji Viktor Gyokeres.
Kikosi cha Arsenal ni;
Kipa: Raya
Walinzi: Timber, Saliba, Hincapie, Calafiori
Viungo: Zubimendi, Rice; Saka, Eze, Trossard
Mshambuliaji: Merino
Mfumo: 4-2-3-1
Kikosi cha Bayern Munich vs Arsenal

Kwa Bayern, Manuel Neuer anatarajiwa kuanza golini, huku Jonathan Tah na Dayot Upamecano wakitengeneza kiini cha ulinzi. Joshua Kimmich atabeba majukumu ya kiungo, huku Michael Olise na Harry Kane wakiongoza mashambulizi.
Kikosi cha Bayern Munich;
Kipa: Neuer
Walinzi: Laimer, Upamecano, Tah, Guerreiro
Viungo: Pavlovic, Kimmich, Olise, Karl, Gnabry,
Mshambuliaji: Kane
Taarifa za majeruhi Arsenal vs FC Bayern Munich
Arsenal watawakosa wachezaji watano muhimu; Viktor Gyokeres, Martin Odegaard, Gabriel Magalhaes, Gabriel Jesus, Kai Havertz.
Bayern wao watawakosa mastaa wao watatu ambao ni; Musiala, Davies na Gnabry ambaye yuko mguu nje, mguu ndani.
Hitimisho

Arsenal vs FC Bayern Munich ni mchezo wa vita ya kusaka uongozi wa msimamo wa UEFA Champions League. Timu zote mbili zikiwa na rekodi ya 100% ya ushindi zinakutana kuulizana nani atapoteza alama? Unatarajiwa kuwa mchezo wa ushindani unaokutanisha timu zenye mzania unaokaribiana kwa ubora na huenda mchezo huu ukaisha kwa matokeo ya sare ya mabao.

