- Simba SC 0-1 Petro de Luanda ndio matokeo rasmi kwenye CAF Champions League 2025/26 hatua ya makundi..
- Petro de Luanda wamechukua pointi tatu muhimu wakiwa ugenini kwa kumchapa mnyama Uwanja wa Benjamini Mkapa.
- Bernardo Dias ndiye mfungaji wa goli la ushindi akimfunga kipa Yakoub Suleman aliyeanza kikosi cha kwanza chini ya Dimitar Pantev.
Simba SC 0-1 Petro de Luanda ndio matokeo kwenye mchezo wa CAF Champions League 2025/26 hatua ya makundi. Mchezo huo ulipigwa Novemba 23,2025 Uwanja wa Benjamini Mkapa. Mnyama Simba SC ameangusha alama tatu muhimu kwenye mechi muhimu. Mchezaji Bernardo Dias alicheka na nyavu dakika ya 78 kwa pasi Tiago Reis likiwapa ushindi wageni kutoka Angola.
SOMA HII: Matokeo ya Simba SC 2025/26 | Ratiba, vinara wa ufungaji
Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

Uwanja wa Mkapa matokeo Simba SC 0-1 Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26

Kete ya kwanza nyumbani Simba SC 0-1 Petro de Luanda CAF Champions League. 2025/26 mnyama ameshindwa kupata ushindi akiwa mwenyeji mechi za kimataifa. Matokeo hayo yanamfanya aburuze mkia kundi D akiwa hajakusanya pointi.
Match highlights Simba SC vs Petro de Luanda
| Simba SC | Petro de Luanda | |
| 56% | Umiliki wa mpira | 44% |
| 0 | Kona | 0 |
| 11 | Jumla ya mashuti | 7 |
| 1 | Mashuti yaliyolenga lango | 2 |
| 0 | Goli | 1 |
Kadi za njano
| Simba SC | Jina la mchezaji | Petro de Luanda |
| Kinito | Dakika ya 21 | |
| Jonathan Toro | Dakika ya 60 | |
| Dakika ya 90 | Jean Ahoua |
SOMA HII: Makundi Klabu Bingwa Afrika CAF 2025/26 haya hapa | Simba SC na Yanga SC zapewa waarabu

Mabadiliko Simba SC vs Petro de Luanda
Jonathan Sowah in 53 out Joshua Mutale
Jean Ahoua in 53 out Naby Camara.
Ladakc Chasambi in 73 out Morice Abraham.
Steven Mukwala in 84 out Allasane Kante kwa upande wa Simba SC.
Gilberto in out Gigal
Tiago Reis in out Jo Paciencia.
Joao Julinho in out Benny kwa Petro de Luanda.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza vs Petro de Luanda

Yakoub Suleiman, Mligo, Mutale Joshua, Kante, Shomari Kapombe, Morice Abraham, De Reuck.
Naby Camara, Wilson Nangu, Ellie Mpanzu, Neo Maema.
Wachezaji wa akiba ni Hussen Abel, Duchu, Chamou, Semfuko, Jean Ahoua, Chasambi, Mwalimu, Jonathan Sowah na Steven Mukwala.
SOMA HII: MC Alger ya Mokwena yaanza kwa kipigo 2-1 Al Hilal Omdurman CAF Champions League

Kikosi cha Petro de Luanda vs Simba SC
Hugo, mabeki Aderito, Kinito, Afonso, viungo Anderson, Jorge, Rubio, Hossi, Benny na Gigal, mshambuliaji Paciencia.
Mbinu za Kocha Mkuu wa Petro de Luanda Franc Artiga zilijibu ugenini kwa kupata pointi tatu muhimu. Simba SC chini ya Meneja Mkuu, Dimitar Pantev mchezo wa kwanza nyumbani hatua ya makundi inaangusha pointi. Mechi mbili zimebaki kwenye hatua ya makundi kwa mnyama kucheza nyumbani.

Msimamo wa kundi D
- Petro de Luanda pointi 3, mechi 1
- Esperance pointi 1, mechi 1
- Stade Malien pointi 1, mechi 1
- Simba SC pointi 0, mechi 0
Hitimisho
Simba SC 0-1 Petro de Luanda CAF Champions League 2025/26 pointi tatu zimepokonywa Uwanja wa Benjamini Mkapa. Mechi mbili zijazo kibarua kitakuwa kigumu zaidi. Petro de Luanda wanaongoza kundi D huku Simba SC ikiwa inaburuza mkia.

