- Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC amefunga goli la ushindi kwenye mchezo wa hatua ya makundi Uwanja wa New Amaan Complex.
- Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League Novemba 22,2025.
- AS FAR Rabat ya Morocco rekodi imevunjwa ugenini kwa kupokea kichapo anga la kimataifa mchora ramani akiwa ni kiungo Mudathir Yahya.
Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League matokeo rasmi ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi. Wananchi wameanza kwa ushindi nyumbani mbele ya wenyeji wao waliokuwa katika mchezo wa kwanza kundi B. Prince Dube amevunja mwiko wa timu hiyo kutofungwa katika mechi 7 zilizopita za mashindano.
SOMA HII: Yanga SC vs AS FAR Rabat CAF Champions League ni leo Novemba 22 2025/ Matokeo, ratiba
Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League Zanzibar

Ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex umesoma Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League. Ukuta wa AS Far Rabat ulivunjwa kwa pasi ndefu ya kiungo Mudathir Yahya dakika ya 58. Prince Dube ambaye alikamilisha kazi kwa kufunga goli pekee la ushindi.
AS FAR Rabat kwenye mechi 7 za ushindani walikuwa hawajapoteza. Ushindi ilikuwa mechi 5 huku wakiambulia sare mbili. Huu unakuwa mchezo wa kwanza kuambulia kipigo wakiwa ugenini.
Kampeni za hatua ya robo fainali zimeanza kwa kasi huku Yanga SC kete ya kwanza wakikomba pointi tatu kundi B. Ushindi huo unawafanya wananchi kuongoza kundi kwa muda. AS Far Rabat inashikilia mkia ikiwa haijakusanya pointi.
Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa Februari 6,2025. Katika mchezo ujao Yanga SC itakuwa ugenini. Pointi tatu zinatafutwa ili timu mbili zitinge hatua yar obo fainali.
SOMA HII: Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025: Kazi imeanza, Wananchi watoa tamko zito

Goli la Prince Dube na maajabu yake
Prince Dube mfungaji wa goli la ushindi katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi. Majabu ya Dube yamepatikana baada ya majaribio ya mara kwa mara kuzuiliwa na mlinda mlango wa AS FAR Rabat. Miongoni mwa jaribio ambalo alifanya Dube ilikuwa ni dakika ya 6.
Goli hilo alifunga kipindi cha pili akitumia pasi ya Mudathir Yahya. Nyota mwingine aliyefanya jaribio kali ilikuwa ni Maxi Nzengeli dakika ya 30. Uimara wa kipa wa AS FAR Rabat uliweka lango salama dakika 45 za kipindi cha mwanzo.
Msimamo upo namna hii

1. Yanga SC pointi 3 mechi 1
2. JS Kabylie pointi 0 mechi 0
3. Al Ahly pointi 0 mechi 0
4. AS FAR Rabat pointi 0 mechi 1
Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya AS FAR Rabat

Djigui Diarra
Israel Mwenda
Zimbwe Jr
Dickson Job
Ibrahim Bacca
Duke Abuya
Maxi Nzengeli
Mudathir Yahya
Prince Dube
Pacome Zozoua
Celectin Ecua
Wachezaji wa akiba
Aboutwalib Mshery, Bakari Nondo, Boka, Balla Conte, Sheikhan Khamis, Lassine Kouma, Doumbia Mo, Edmund John, Boyel.
Kikosi cha AS Far Rabat kilichoanza dhidi ya Yanga SC
Tagnaouti
Bach
Abdelhamid
Louadni
Carneiro
Derrag
Hrimat
Hammoudan
Slim
Slim
Ait Ouarkhane
Al Fahli
Wachezaji wa akiba
El Khayati, Mendy, Bouriga, Khabba, Habessi, El Bouchoali, Ech Chemmakh, Ait Khassou, Hadraf.

Hitimisho
Yanga SC 1-0 AS FAR Rabat CAF Champions League imeonesha ukubwa wa timu za ukanda wa Afrika Mashariki. Nyota wa mchezo Prince Dube amepeleka kilio kwa AS Far Rabat. Mudathir alishindwa kujizuia alishangilia kwa nguvu baada ya goli hilo kufungwa.

