Yanga SC vs AS FAR (-)Yanga SC vs AS FAR (-)
  • Kesho Jumamosi hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itaanza kutimua vumbi rasmi.
  • Visiwani Zanzibar kutakuwa hapatoshi, ambapo kutapigwa mchezo mkali wa Yanga SC vs AS FAR.
  • Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Jumamosi ya Novemba 22, 2025.

Yanga SC vs AS FAR CAF 22/11/2025, ndiyo Habari kubwa kwenye vijiwe vya soka kwa sasa. Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, utakaopigwa kesho Jumamosi 22 Novemba 2025. Mchezo huu utachezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs AS FAR CAF Champions League: Kocha Pedro awaandalia dozi waarabu

Cheza sasa ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Bado hujashinda na SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Yanga SC vs AS FAR historia ya H2H

Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa timu hizi kukutana, katika mashindano rasmi ya kimataifa. Hivyo kila timu inatarajiwa kuuendea mchezo huu, kama Daraja la kuandika historia mpya kimataifa. Ikumbukwe mchezo utaanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Yanga yafanya mazoezi ya mwisho Zanzibar

Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Ali Kamwe umeweka wazi kuwa kikosi chao kilichosafiri Jumanne kwenda Zanzibar, leo kimefanya mazoezi ya mwisho. Kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuwa na mastaa wote, isipokuwa baadhi ambao wana majeraha.

Yanga SC vs AS FAR tiketi zimeanza kuisha

Yanga SC vs AS FAR
ununuzi wa tiketi

Kuhusu utaratibu wa tiketi za kushuhudia mchezo huo, mpaka Makala hii inaandikwa baadhi ya maeneo ya uwanja tiketi zilikuwa zimeisha.  Uongozi wa Yanga SC ulitangaza kuwa tiketi za VIP tayari zimeisha. Pamoja na hayo uongozi wa Yanga SC, umesisitiza mashabiki wa timu hiyo wasikubali kukosa burudani hiyo.

SOMA HII ZAIDI: Matokeo ya Yanga SC 2025/26 | Wafungaji, magoli, ratiba ya mechi zijazo

Kikosi tarajiwa cha Yanga SC vs AS FAR

Kuelekea mchezo huo kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:

Kipa: Djigui Diarra

Walinzi: Israel Mwenda, Mohammed Hussein, Dickson Job, Ibrahim Bacca.

Viungo: Celestine Ecua, Zouzoua Pacome, Mohammed Doumbia, Balla Conte, Maxi Nzengeli.

Washambuliaji: Prince Dube

Yanga wamepangwa dhidi ya timu gani makundi

Yanga SC vs AS FAR
Kundi la Yanga SC

Katika droo ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/26, ambayo ilipangwa nchini Afrika Kusini Novemba 3, mwaka huu. Yanga SC walipangwa kwenye Kundi B, pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS FAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria.

SOMA HII PIA: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF Champions League/ Live scores

Yanga SC kuisaka Robo Fainali Zanzibar

Ukiachana na mchezo huo, uongozi wa Yanga SC umeweka wazi kuwa mechi zao zote tatu za kimataifa hatua ya makundi, zitapigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Kwa msimu huu wa mashindano ya kimataifa, huu ndio unatarajia kuwa uwanja wao wa nyumbani. Mchezo dhidi ya AS FAR ukiwa ndiyo karata ya kwanza kwa Yanga SC.

Ratiba kamili ya Yanga SC hatua ya makundi CAF Champions League

Yanga SC vs AS FAR inatarajiwa kuchezwa Novemba 22, 2025

JS Kabylie vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Novemba 28, 2025

Al Ahly vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa Januari 23, 2026

Yanga SC vs Al Ahly inatarajiwa kuchezwa Januari 30, 2026.

AS FAR vs Yanga SC inatarajiwa kuchezwa 6, Februari 2026.

Yanga SC vs JS Kabylie inatarajiwa kuchezwa Februari 13,2026.

Yanga SC vs AS FAR, Kocha Pedro awaandalia Waarabu dozi

Alichosema kocha Yanga SC kuhusu Yanga SC vs AS FAR

get (-)
Kocha Yanga

“Kesho ni mchezo wetu wa kwanza kwenye hatua ya makundi, kila mtu anasema ni kundi la kifo kwa sababu ya timu kubwa nne. Lakini kama unataka kuwa bingwa lazima ushindane na mabingwa. FAR Rabat wana timu nzuri ambayo ina wachezaji bora. Sisi tuna timu bora sana ambayo ina muunganiko mzuri pia. Tukipata hamasa ya kutosha kutoka kwa mashabiki basi tutakuwa na mchezo bora zaidi.

“Falsafa yangu ni kuutawala mchezo kwa gharama yoyote ile. Nahitaji wachezaji wangu wajitume sana. Malengo yangu makubwa ni timu kucheza vizuri. Matokeo ya mchezo wa kesho naamini yatatokana na namna ambavyo tutacheza vizuri, namna ambavyo tutaongeza utulivu na umakini,” amesema kocha Pedro.

Hitimisho

Yanga SC vs AS FAR 22/11/2025 CAF ni mechi ya kufa na kupona. Licha ya ubora wa AS FAR ambao wanauonyesha katika ligi ya Morocco, bado umadhubuti wa Yanga SC kimataifa umezidi kuimarika. Misimu miwili iliyopita walicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mashabiki wao wanatamani kuona timu inaandika rekodi nyingine kubwa zaidi msimu huu, hasa baada ya kuishia makundi msimu uliopita.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.