- Yanga SC vs KMC NBC Premier League ni mechi ya moto Novemba 9,2025, Uwanja wa KMC Complex.
- Yanga SC imepata ushindi katika mechi 11 jumlajumla walipokutana kati ya michezo 14 ya ligi.
- Matokeo ya mwisho walipokutana ilikuwa KMC 1-6 Yanga SC msimu wa 2024/25.
Yanga SC vs KMC ni mchezo utakaochezwa Jumapili, Novemba 9,2025, Uwanja wa KMC Complex. Wababe hawa tangu 2018 wamekutana mara 14. Yanga SC imeshinda mechi 11 huku KMC ikipata ushindi katika mchezo mmoja pekee. Sare ni katika mechi mbili walipogawana pointi mojamoja. Wananchi wanapewa nafasi kubwa ya kupata matokeo licha ya kwamba KMC nao wapo imara kusaka ushindi.

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi
Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

Yanga SC vs KMC mchezo wa moto huu
Wababe hawa Yanga SC vs KMC wanapokutana pointi husakwa kwa nguvu na magoli yanafungwa. Wananchi wamekuwa imara katika eneo la ushambuliaji huku wakusanya mapato wakiwa kwenye kasi ndogo. Mara ya mwisho walipokutana msimu wa 2024/25 ubao ulisoma KMC 1-6 Yanga SC.
Katika msimamo Yanga SC ipo nafasi ya 4 ikiwa na pointi 7. KMC ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 3. Mechi ambazo wamecheza KMC ni 5, ushindi mchezo mmoja na kupoteza mechi 4.
H2H
14/02/2025, KMC 1-6 Yanga SC.
29/09/2024, Yanga SC 1-0 KMC.
17/02/2024, KMC 0-3 Yanga SC.
23/08/2023, Yanga SC 5-0 KMC.
22/02/2023, KMC 0-1 Yanga SC.
26/10/2022, Yanga SC 1-0 KMC.
19/03/2022, Yanga SC 2-0 KMC.
10/04/2021, Yanga SC 1-1 KMC.
25/10/2020, KMC 1-2 Yanga SC.
12/10/2020, KMC 1-0 Yanga SC.
02/12/2019, Yanga SC 1-1 KMC.
10/03/2019, Yanga SC 2-1 KMC.
25/10/2018, KMC 0-1 Yanga SC.
Katika mechi 13 za ligi, ushindi kwa wageni KMC ni kwenye mechi 1, sare 2. Wenyeji Yanga SC walipata ushindi kwenye mechi 10. Itafahamika nani atacheka baada ya dakika 90 Novemba 9,2025.
Mechi 5 za Yanga SC zilizopita
Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji.(Ligi ya NBC)
Septemba 30,2025-Mbeya City 0-0 Yanga SC (Ligi ya NBC).
Silver Strikers FC 1-0 Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.
Yanga SC 2-0 Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025
Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar, Oktoba 28 2025, Uwanja wa KMC, Complex.
SOMA HII: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 NBC Premier League, CAF

Mechi 5 zilizopita za Tanzania Premier League kwa KMC
17/09/2025, KMC 1-0 Dodoma Jiji FC
23/09/2025, KMC 0-1 Singida Black Stars
27/09/2025, Tanzania Prisons 1-0 KMC
18/10/2025, KMC 0-3 Mbeya City
25/10/2025, Fountain Gate FC 1-0 KMC
Kikosi cha Yanga SC kinachotarajiwa kuanza dhidi ya KMC FC

Mlinda mlango
Djigui Diarra
Mabeki
Israel Mwenda
Zimbwe Jr
Dickson Job
Bakari Nondo
Viungo
Duke Abuya
Maxi Nzengeli
Mohamed Doumbia
Offen Chikola
Edmund John
Mshambuliaji
Dube
Kikosi cha KMC kinachotarajiwa kuanza dhidi ya Yanga SC
Fabien Mutombora
Juma Shemvuni
Hance Masoud
Rashid Chambo
Erick Mwijage
Juma Mwita
Redemtus Mussa
Abdallah Said
Ahmed Pipino
Ibrahim Nindi
Kelvin Tondi
Hitimisho
Yanga SC vs KMC ni mtego kwa kila timu kuvuna pointi tatu kutokana na ushindani uliopo. Mabingwa watetezi wanapewa nafasi kubwa kushinda mchezo kulingana na matokeo yao wanapokutana. Je wakusanya mapato watakubali kupoteza ili waendelee kuburuza mkia ama watajinasua? Matokeo yote utayapata hapa.

