mechi za Simba SC 2025/26Kibu D Mkandaji (-)
  • Simba SC kwenye NBC Premier League 2025/26 ilifungua pazia kwa ushindi wa magoli 3-0 Fountain Gate.
  • Mechi za Simba SC 2025/26 CAF Champions League, NBC Premier League ni moto wa kuotea mbali.
  • CAF Champions League imeandika rekodi ya kutinga hatua ya makundi ikiwa kundi gumu kusaka tiketi ya robo fainali.

Mechi za Simba SC 2025/26 ni moto wa kuotea mbali mara baada ya timu hiyo kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Dimitar Pantev mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids anawapa mbinu za ushindi vijana wa Msimbazi. Novemba 8 2025 meneja huyo anatarajiwa kusimama kwenye mchezo wa ligi kwa mara ya kwanza.

SOMA HII: Matokeo ya Simba SC 2025/26 NBC, CAF Champions League

Unasubiri nini? Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini.

image

Mechi za Simba SC 2025/26 matokeo yalikuaje?

mechi za Simba SC 2025/26
Wachezaji wa Simba SC wakishangilia moja ya goli kwenye mechi yao msimu wa 2025/26. Source: Simba SC.

Huu ni msimu mpya huku mechi za Simba SC 2025/26 zikiwa ni miongoni mwa zile ambazo zinafuatiliwa kwa ukaribu kitaifa na kimataifa. Rekodi zinaoyesha kuwa kwenye mechi 8, ilipoteza mchezo mmoja dhidi ya Yanga SC katika Kariakoo Dabi. Sare ni kwenye mechi mbili. Ushindi ilikuwa kwenye mechi 5.

Haya hapa matokeo kwa mechi za Simba SC 2025/26

Simba SC 3-0 Fountain Gate FC
Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC. Source: Simba SC.

Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.

Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Nsingizini Hotspurs 0-3 Simba SC, Oktoba 19 2025, CAF Champions League.

Simba SC 0-0 Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025, CAF Champions League.

SOMA HII: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025

image

Ratiba ya mechi zijazo kwa Simba SC

Simba SC ilikuwa na mchezo wa ligi ambao ulipangwa awali kuchezwa Oktoba 30,2025 dhidi ya TRA United. Mchezo huo haukuchezwa baada ya ligi kusitishwa. Sababu kubwa ya ligi kusitishwa kwa muda ilikuwa ni changamoto za kiuendeshaji zilizotokana na sababu za kiusalama na miongozo yake ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB), Novemba 4.

JKT Tanzania vs Simba SC, Novemba 8 2025, Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo, NBC Premier League.

Yanga SC vs Simba SC, Desemba 13, 2025, Uwanja wa Mkapa, NBC Premier League.

Simba SC vs Mashujaa FC, Februari 19, 2026, Uwanja wa KMC, Complex Dar.

Vinara wa ufungaji wa magoli Simba SC

Mpanzu atua kwa kishindo Misri
De Reuck beki wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Ligi Kuu Bara

Rushine De Reuk magoli 2 alifunga goli moja mchezo dhidi ya Fountain Gate na Namungo FC.

Jean Ahoua goli 1

Chamou Karabou goli 1

Seleman Mwalimu goli 1

Jonathan Sowah goli 1

Wafungaji Ligi ya Mabingwa Afrika

Ellie Mpanzu goli 1

Jean Ahoua goli 1

Wilsons Nangu goli 1

Kibu Dennis magoli 2

SOMA HII: Simba SC 1-1 Gaborone United CAF Champion League

image

Mabao ya kufungwa

Katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC baada ya mechi mbili haijafungwa. Imekusanya jumla ya pointi sita kwa ushindi kwenye mechi mbili.

Idadi ya magoli ambayo imefunga kwenye ligi ni 6 katika Ligi ya Mabingwa Afrika ni magoli 5. Kipa namba moja ni Moussa Camara ambaye alipata maumivu mchezo dhidi ya Gaborone United. Kipa namba mbili ni Yakoub Suleman ambaye yupo fiti kwa sasa.

Katika anga la kimataifa, Simba SC baada ya kucheza mechi nne imeruhusu goli moja. Ni dhidi ya Gaborone United. Mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kundi la Simba SC Ligi ya Mabingwa Afrika

Kundi D

ES Tunis ya Tunisia

Simba SC kutoka Tanzania

Petro Luanda ya Angola

Stade Malien ya Mali

Hitimisho

Mechi za Simba SC 2025/26 zimekuwa na ushindani mkubwa na matokeo ya mwanzo yamekuwa hayatabiriki kulingana na ushindani uliopo. Katika mechi za kimataifa ugenini mnyama amekuwa akipata matokeo mazuri lakini nyumbani hajapata ushindi. Kutakuwa na mechi tatu nyumbani baada ya kutinga hatua ya makundi je rekodi hiyo itavunjwa?

Share this: