- CAF Champions League inatarajiwa kuunguruma wikiendi hii kwa mechi kali kuchezwa.
- Simba SC vs Nsingizini Hotspurs ni Jumapili ya Oktoba 19 2025 itachezwa Uwanja wa taifa wa Somhlolo-Eswatin.
- Wajue wachezaji wa Simba SC na Nsingizini Hotspurs ambao ni hatari wakiwa uwanjani.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League mchezo wa kwanza wa mashindano kwa Dimitar Pantev. Mrithi wa mikoba ya Fadlu Davids mbinu zake zinatarajiwa kutumika ugenini. Oktoba 19,2025 katika Uwanja wa taifa wa Somhlolo-Eswatin wababe hao wawili watakutana.
SOMA HII: Kuelekea Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champion League 2025
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Unaweza kuwa mshindi wa mamilioni ya SportPesa sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kucheza kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League ni hatua gani?

Huu ni mchezo wa mtoano na mshindi wa jumla atatinga hatua ya makundi. Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 24, 2025. Kila timu ina wachezaji hatari wanaopaswa kuchungwa.
Matokeo ya mechi 6 za Simba SC
Oktoba Mosi 2025, Simba SC 3-0 Namungo FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Septemba 28 2025, Simba SC 1-1 Gaborone United, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 25 2025, Simba SC 3-0 Fountain Gate mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Septemba 20 2025, Gaborone United 0-1 Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Septemba 16 2025, Yanga SC 1-0 Simba SC, Ngao ya Jamii.
Septemba 10 2025, Simba SC 2-0 Gor Mahia mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
SOMA HII: Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League | Goli la Ellie Mpanzu, kadi nyekundu

Matokeo ya mechi 6 za Nsingizini Hotspurs

Nsingizini Hotspurs 1-0 Simba Bhora, ilishinda kwa penalti 4-2, Septemba 28,2025 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba Bhora 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 21 2025, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Black Bulls 1-0 Nsingizini Hotspurs, Septemba 19,2025, mchezo wa kirafiki.
Sidvwashini United 0-5 Nsingizini Hotspurs, Mei 25 2025, mchezo wa MTN Premier League.
Nsingizini Hotspurs 2-1 Rangers Shiselweni, Mei 17 2025, MTN Premier League.
Mbabane Highland FC 2-1 Nsingizini Hotspurs, MTN Premier League, Mei 11 2025.
Wachezaji wakuchungwa kikosi cha Simba SC

Jean Ahoua
Licha yakutokuwa kwenye mwendelezo bora katika mechi zake bado ni imara. Ahoua katika mchezo uliopita dhidi ya Gaborone United Ligi ya Mabingwa Afrika alifunga goli kwa mkwaju wa penati. Kiungo mwenye kipaji akiongeza juhudi atakuwa hatari zaidi.
Ellie Mpanzu
Goli la ugenini dhidi ya Gaborone United lilifungwa na Ellie Mpanzu. Winga mwenye kasi akiwa uwanjani. Wapinzani wanapaswa kumtazama kwa ukaribu.
Morice Abraham
Hapendi kukata tamaa mapema. Spidi kwenye miguu na uwezo wa kujaribu ni asili yake. Akipewa nafasi ni mchezaji wa kuchungwa uwanjani.
Kibu Dennis
Kwenye eneo la matumizi ya nguvu huyu amekuwa imara. Bado hajawa fiti asilimia 100 lakini ni mchezaji wakuchungwa akipewa nafasi.
Rushine
Rushine De Reuck ni beki wa Simba SC. Amekuwa na hatari katika kufunga na kulinda ngome yao. Wapinzani wanapaswa kumtazama kwa umakini akiwa uwanjani.
SOMA HII: Gaborone United Vs Simba SC: ‘Live’ CAF Champions League 2025, Botswana

Wachezaji wa kuchungwa kikosi cha Nsingizini Hotspurs
Shabalala
Khanyakweze Shabalala ni kipa wa timu ya Nsingizini Hotspurs ya Eswatini. Uimara wake langoni huenda ukawa kikwazo kwa Simba SC na uimara kwao. Ni raia wa Eswatini amekuwa akiitwa mara kwa mara katika timu ya taifa ya Eswatini.
Neliswa Dlamini
Neliswa Dlamini huyu ni kiungo mshambuliaji mwenye nguvu akiwa uwanjani. Ni kijana mdogo mwenye miaka 21. Simba SC wanapaswa kumtolea jicho kutokana na wepesi wake katika kufuata hatari.
Thunehile Mavuso
Thunehile Mavuso huyu ni mshambuliaji ambaye ni tegemeo katika kikosi. Ni mzaliwa wa Eswatin ana uwezo wa kucheza kwa umakini katika eneo la kiungo mshambuliaji.
Swizwe Khumalo
Swizwe Khumalo huyu ni mshambuliaji machachari. Kwenye mchezo dhidi ya Mbabane Swallow alifunga goli kali. Hivyo sio mchezaji wa kumpa nafasi kwenye eneo la 18.
Nkosingiphile Shongwe
Nkosingiphile Shongwe. Huyu ni beki wa kutegemewa. Amekuwa akiitwa katika timu ya taifa ya Eswatin. Muhimu Simba SC wakamuangalia kwa umakini kwenye mchezo ujao.
H 2 H
Nsingizini Hotspurs vs Simba SC, Oktoba 19, 2025.
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs, Oktoba 24,2025.
Hitimisho
Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champions League ni mechi kali inayosubiriwa kwa shauku kubwa. Mnyama anapewa upato kuibuka na matokeo mazuri ugenini. Licha ya chapuo hilo bado Nsingizini Hotspurs sio wakubeza kutokana na uimara walionao.
Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17


