- Ratiba ya Yanga SC msimu kwenye NBC Premier League na CAF Champions League
- Matokeo ya Yanga SC 2025/26, mchezo wa kwanza kwenye ligi walishinda magoli 3-0 Pamba Jiji.
- Wiliete SC 0-3 Yanga SC ushindi mkubwa katika anga la kimataifa ugenini
Matokeo ya Yanga SC kwenye mechi walizocheza 2025/26 ni aina mbili pekee. Kwenye mechi sita, ushindi ni mechi tano, sare ya bila kufungana dhidi ya Mbeya City. Bado Romain Folz Kocha Mkuu wa Yanga SC hajaonja Ladha ya kupoteza.
SOMA HII: Yanga SC 0-0 Mbeya City NBC Premier League | Highligts, Romain Folz kibarua kigumu
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Matokeo ya Yanga SC katika mechi zao

Hapa tunakuletea matokeo ya Yanga SC inayofundishwa na Kocha Mkuu Romain Folz katika mechi zao walizoshuka uwanjani. Kuna mechi za kirafiki, Ligi Kuu Bara ya NBC na Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa ligi.
Septemba 12,2025 – Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki). Mfungaji alikuwa ni Celestin Ecua dakika ya pili. Mchezo ulichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Septemba 16, 2025 – Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii). Goli la ushindi lilifungwa na Pacome Zouzoua. Mchezo ulichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Septemba 19, 2025 – Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika). Magoli yalifungwa na Aziz Andambwile, Edmund John na Prince Dube.
Septemba 24,2025 – Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC). Magoli yalifungwa na Kouma, Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya.
Oktoba 27,2025 -Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika). Wafungaji walikuwa ni Aziz Andambwile na Pacome.
Septemba 30,2025-Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC).
SOMA HII: Uchambuzi wa Yanga SC vs Simba SC itakayochezwa Septemba 16 | H2H, vikosi, matokeo, wafungaji

Uimara wa Yanga SC 2025/26

Yanga SC imekuwa imara katika eneo la ulinzi. Kwenye mechi sita ambazo ilishuka uwanjani haijaruhusu kufungwa goli. Mlinda mlango namba moja ni Djigui Diarra. Kipa huyu tuzo ya mchezaji bora ndani ya NBC kwa Septemba. Ilitokana na mechi mbili za ligi kutofungwa. Safu ya ulinzi inaongozwa na beki Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakari Nondo.
Kwenye eneo la kufunga katika mechi 6, safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imefunga magoli 10. Mchezaji mwenye magoli mengi katika hatua ya awali CAF Champions League ni Aziz Andambwile akiwa nayo mawili.
Mechi zijazo za Yanga SC kwenye Ligi ya NBC 2025/26

Yanga SC vs Mtibwa Sugar, Oktoba 29 2025, Uwanja wa KMC, Complex.
Yanga SC vs KMC FC, Novemba 4 2025, Uwanja wa KMC Complex.
Coastal Union vs Yanga SC, Desemba 10 2025, Uwanja wa Mkwakwani.
Yanga SC vs Simba SC, Desemba 13 2025, Uwanja wa Mkapa
Yanga SC vs Dodoma Jiji FC, Uwanja wa KMC Complex, Februari 18 2026.
SOMA HII: Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 | Vikosi, H2H, utabiri, milioni 15 zakunjwa

Mechi za Ligi ya CAF Champions League 2025/26
Silver Strikers FC vs Yanga SC CAF Champions League, Oktoba 18, 2025 Uwanja wa Bingu, Malawi.
Yanga SC vs Silver Strikers FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 25, 2025.
Hitimisho
Matokeo ya Yanga SC yanatokana na jitihada za wachezaji na mbinu za benchi la ufundi katika uwanja wa mazoezi. Kutokana na uwepo wa wachezaji wapya kumekuwa na mabadiliko ya kikosi cha kwanza mara kwa mara. Kouma ingizo jipya amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli kwenye ligi msimu wa 2025/26.
Bonyeza hapa chini na ujishindie mamilioni kwa kucheza SportPesa Supa Jackpot 17


