Rushine De Reuck kinara ufungajiRushine (-)
  • Oktoba 19 2025 Simba SC itakuwa ugenini katika mchezo wa raundi ya pili kimataifa.
  • Simba SC vs Nsingizini Hotspurs CAF Champion League 2025 mbinu za makocha kuamua ushindi.
  • Nsingizini iliwafungashia virago Simba Bhora mabingwa wa Zimbabwe, Simba SC iliwafungashia virago Gaborone United.

Anga la kimataifa zinahesabiwa siku kabla ya wababe kushuka uwanjani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Simba SC vs Nsingizini Hotspurs ni moja ya mchezo unaousubiriwa kwa shauku kubwa. Mshindi wa jumla katika hatua hii ya pili atatinga hatua ya makundi. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Oktoba 19 2025, Uwanja wa taifa wa Somhlolo.

SOMA HII: Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League | Goli la Ellie Mpanzu, kadi nyekundu

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Simba vs Nsingizini Hotspurs zimefikaje hapa?

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs
Hemed Morocco kocha aliyeivusha Simba SC hatua ya awali. Source: Simba SC.

Ilikuwa ni safari kwa kila timu katika mechi za hatua ya awali kusaka ushindi. Simba SC vs Ningizini Hotspurs zimepita katika njia hizo. Ushindi wa jumla katika mechi mbili umewapa tiketi kuwa walipo kwa sasa.

Simba SC ilikuwa chini ya kocha wa muda Hemed Suleman mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Hii ilitokana na Fadlu Davids kupata kazi Klabu ya Raja Casablanca. Fadlu aliongoza kikosi cha Simba SC katika mchezo wa ugenini.

Safari ya Simba SC ilikuwa namna hii

Ellie Mpanzu EM
Ellie Mpanzu nyota wa Simba SC aliyefunga goli ugenini. Source: Simba SC.

Septemba 20 2025 ubao wa Uwanja wa Obedi Itani Chilume ulisoma Gaborone United 0-1 Simba SC.

Septemba 28 2025, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba SC 1-1 Gaborone United.

Simba SC ilitinga hatua ya pili Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1. Goli la ugenini lililofungwa na Ellie Mpanzu lilikuwa na faida kwa Simba SC.Kwenye mchezo wa Uwanja wa Mkapa magoli yote mawili yalifungwa kwa mikwaju ya penati.

SOMA HII: Gaborone United Vs Simba SC: ‘Live’ CAF Champions League 2025, Botswana

image

Hii safari ya Nsiginzini Hotspurs

Makdla
Qhoqi, Kocha Mkuu wa Nsingizini Hotspurs. Source: Nzingizini.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Eswatini 2024/25 Nsingizini Hotspurs chini ya Kocha Mkuu, Mandla Qhogi safari yao ilianzia ugenini. Ni mabingwa wa Zimbabwe Simba Bhora walifungashiwa virago katika hatua ya awali. Ushindi wa jumla ya penalti 4-2 baada ya wote kufungana bao 1-1 katika kila mchezo.

Katika mchezo wa kwanza Septemba 21 2025 ilikuwa Simba Bhora 1-0 Nsingizini Hotspurs. Mchezo wa pili Septemba 28 2025 ilikuwa Nsingizini Hotspurs 1-0 Simba Bhora. Hivyo kila mmoja alikuwa mbabe nyumbani.

Katika mchezo ulioamua mshindi atakayetinga hatua ya pili, Nsingizini Hotspurs walipata goli dakika za jioni. Zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kukamilika katika muda wa nyongeza. Ilikuwa dakika ya 90+1 Nkosingiphile Shongwe alipachika goli ambalo likapelekea mshindi atafutwe kwa penalti.

Kwenye mapigo ya penalti ilikuwa Nsingizini Hotspurs 4-2 Simba Bhora hivyo wakafungashiwa virago jumlajumla mabingwa wa Zimbabwe. Simba Bhora wao jukumu lao ilikuwa ni kulinda ushindi waliopata nyumbani. Kazi ilikuwa ngumu wakakwama.

Matokeo mechi za kwanza kwenye ligi 2025/26

Timu hizi mbili tayari zimeanza kucheza mechi zao za kwenye ligi. Katika mechi za ufunguzi kila mmoja alivuna pointi tatu. Simba SC ilifungua pazia ikiwa nyumbani na wapinzani wao walikuwa ugenini.

Septemba 25 2025 Simba SC 3-0 Fountain Gate

 Oktoba 4 2025 Mbabane Highlanders 0-1 Nsigizini Hotspurs

SOMA HII: CAF Confideration Cup mbili kutoka Tanzania kazini Septemba 20 | Vikosi vya Azam FC na Singida Black Stars

image

Hitimisho

Simba SC vs Nsingizini Hotspurs ni mchezo wenye sura ya ushindani kimataifa. Simba SC itaanzia ugenini na kumalizia kazi nyumbani. Kwenye hatua ya mtoano hakuna mchezo mwepesi licha ya Simba SC kupewa nafasi kubwa kupata ushindi.

image
Share this: