- Abraham Morice aliwavuruga wapinzani mwanzo mwisho katika kutimiza majukumu yake.
- Simba SC 1-1 Gaborone United kwenye CAF Champion League 2025/26.
- Licha ya matokeo ya sare, Simba SC wataweza kwenda raundi ya pili kwenye mashindano haya.
Simba SC 1-1 Gaborone United ndio matokeo rasmi ya CAF Champion League 2025/26. Simba SC walitangulia kwa kufunga goli la kwanza kupitia mchezaji Jean Ahoua dakika 45. Wapinzani wao Gaborone United waliweza kusawazisha kwenye kipindi cha pili kupitia kwa Ditsele. Mchuano huu mkali ulifanyika kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa. Simba SC wamefaulu kufika raundi ya pili ya michuano hii.
SOMA HII: Elie Mpanzu Kibisawala ni Simba SC 2025/26/ Rekodi na magoli / Dili lake Yanga SC
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni
Muda ni sasa kwako rubani kuvuna mamilioni sasa hivi. Rahisi sana bila tabu hata kidogo. Cheza Aviator sasa upate mgao wako.

Matukio muhimu yaliyotokea kwenye mechi ya Simba SC vs Gaborone United

Kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa ushindani ulikuwa mkubwa na mwisho Simba SC 1-1 Gaborone United CAF Champion League. Wenyeji Simba SC walianza kupata goli dakika ya 45 kupitia kwa Jean Ahoua. Goli hilo lilifungwa kwa mkwanju wa penati.
Ni Morice Abraham winga aliyekuwa na siku nzuri kazini alisababisha penati hiyo. Pasi ya Ellie Mpanzu ilikutana na Jonathan Sowah, jaribio lake dakika ya 44 likaokolewa na kipa wa Gaborone. Tayari Morince alikuwa ndani ya 18 akachezewa faulo na mwamuzi Mohamed Mussa akamuru ipigwe penati.
Simba SC ilikamilisha dakika 45 ikiwa imepiga mashuti mawili langoni. Katika hayo ni moja lilikuwa goli. Huku Gaborone United wakipiga mashuti matatu yaliyookolewa na Mussa Camara.
Goli la Gaborone United lilifungwa dakika ya 70 kwa mkwaju wa penati. Chamou beki wa Simba SC alisababisha penati hiyo katika harakati za kuokoa. Ni Lebogang Ditsele alifunga dakika ya 57 ya mchezo kipindi cha pili.
SOMA HII: SportPesa Goal Rush washindi 26 Septemba -1 Oktoba 2025 hawa hapa
Kadi za njano kwenye mchezo wa CAF

Mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano alikuwa Alford Velaph wa Gaborone United. Dakika ya 29 ilikuwa. Faulo mchezaji alichezwa Morice Abraham.
Kwa upande wa Simba SC Jonathan Sowah alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 50. Chamou dakika ya 56. Mchezaji mwingine ni Moussa Camara alionyesha kadi ya njano dakika ya 71.
Wachezaji waliofanyiwa mabadiliko

Soma hii: Simba SC 1-0 Gaborone United CAF Champion League 2025
Jean Ahoua hakukomba dakika 90 katika mchezo. Dakika 72 alitoka nafasi yake ilichukuliwa na Joshua Mutale. Ellie Mpanzu alitoka dakika ya77 nafasi yake ilichukuliwa na Kibu Dennis. Camara ambaye ni kipa alipata maumivu na alikwama kuendelea nafasi yake ilichukuliwa na Yakuob Suleman.
Ahoua kwenye mchezo wa leo hakuwa katika siku nzuri kazini. Nafasi mbili za dhahabu alikwama kuujaza mpira nyavuni. Miongoni mwa hizo ilikuwa kipindi cha pili baada ya kuwatoka mabeki na kumpiga chenga kipa. Shuti lake lilikwenda nje kidogo ya lango.
Thabo Maponda aliingia dakika ya 45 kwa Gaborone United akichukua nafasi ya Sheikh. Mchezaji huyu aliongeza hatari kubwa kwa upande wa Gaborone. Katika mchezo wa kwanza alianza kikosi cha kwanza na mchezo wa pili alianzia benchi.
Morice Abraham alikuwa katika ubora
Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Morice Abraham alikuwa katika ubora. Kwenye mchezo wa leo dakika 90 alifanya kazi yake kwa umakini. Ni mchezaji aliyechezewa faulo zaidi ya tatu na wachezaji wa Gaborone United. Ikumbukwe kwamba ni yeye alisababisha penati kwa Simba SC.
Je Simba SC atachuana na nani kwenye msururu ujao?
Baada ya ushindi wa jumla ya magoli 2-1 dhidi ya Gaborone United, Simba SC inasonga hatua inayofuata. Itakutana na Nsingizini Hotspurs ya Eswatini. Mchezo wa kwanza itakuwa ugenini kisha ule wa pili utachezwa Dar.
Hitimisho
Matokeo haya ya Simba SC 1-1 Gaborone United kwenye Champion League yalikuwa yakukata na shoka. Makocha wote wawili waliweza kutoshana mbinu kwa kuenda sare. Kupitia goli moja kwenye msururu wa kwanza, Simba SC wataweza kuendelea kwenye raundi nyingine ya mashindano haya.


