Pacome MasterPacome Master
  • Mchezo wa kwanza kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara utachezwa Uwanja wa Mkapa.
  • Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 2025 mechi ya kisasi na kulinda rekodi kwa wababe hawa wawili uwanjani.
  • Romain Folz kuongoza jahazi wachezaji wakitoka kukunja milioni 15 za ushindi anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga SC vs Pamba Jiji FC mchezo wa kwanza kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26. Timu hizi mbili zinakwenda kukutana rekodi zikionyesha kuwa msimu wa 2024/25 Pamba Jiji ilishindwa kufurukuta nje ndani kwa kufungwa kwenye mechi za ligi. Wapinzani wa Yanga SC wapo Dar kwa maandalizi ya mwisho huku Wanajangwani nao wakiendelea kuwavutia kasi wapinzani.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni

Ni muda wako sasa kupaisha Kindenge cha SportPesa uvune mamilioni. Ni rahisi sana na inawezekana kabisa. Unachotakiwa kufanya ni kucheza Aviator upate mgao wako.

image

Yanga SC vs Pamba Jiji FC Septemba 24 2025 vita ya mbinu uwanjani

Nashon wa Pamba Jiji
Kelvin Nashon nyota wa Pamba Jiji na wachezaji wengine watakaoikabili Yanga SC. Source: Pamba Jiji.

Roman Folz anatarajiwa kupanga ramani ya ushindi kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa ligi kati ya Yanga SC vs Pamba Jiji FC. Kocha huyo ambaye mchezo uliopita wa kimataifa mbinu zake zilijibu kwa ubao kusoma Wiliete SC 0-3 Yanga SC anatarajiwa kuwa kwenye benchi. Ikumbukwe kwamba baada ya ushindi huo Yanga SC imevuna milioni 15 ikiwa ni zawadi ya goli la mama kimataifa walikabidhiwa rasmi Septemba 22 2025.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC vita ya ubingwa bado inaendelea

Francis Baraza huyu atakuwa kwenye benchi la ufundi la Pamba Jiji. Kocha huyu ni muumini wa kushambulia bila kuogopa. Mchezo wake wa kwanza wa msimu alikuwa ugenini dhidi ya Namungo FC uliochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Mbinu za makocha hawa wawili zinatarajiwa kuamua matokeo ndani ya dakika 90. Ni kwa mara ya kwanza wanakutana makocha hawa wote wawili kila mmoja akiwa ni mpya. Uwanja wa Mkapa utashuhudia burudani makini kutoka kwa timu zote mbili.

Kikosi cha Yanga SC vs Pamba Jiji FC

Dickson Job (-)
Dickson Job beki wa Yanga SC nahodha msaidizi wa Jangwani. Source: Yanga SC.

Djigui Diarra, Israel Mwenda, Ladack Boka,Dickson Job, Ibrahim Bacca, Aziz Andambilwe, Clement Mzize, Duke Abuya, Mohamed Doumbia na Pacome Zouzoua.

Wachezaji wa akiba

Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari, Zimbwe Jr, Assinki, Balla Conte, Mudathir Yahya, Celestine Ecua, Edmund John na Maxi Nzengeli.

Kikosi cha Pamba Jiji vs Yanga SC

Yona Amosi, Ibrahim Abraham, Mathew Tegisi, Shassiri Nahimana, Abdoulaye Kunambi, John Ben, Shaphan Siwa, James Mwashinga, Kelvin Nashon, Abdallah Kheri.

Wachezaji wa akiba

Abdulmajid Mangalo, Michael Samamba, Saleh Masoud, Najim Mussa, Samuel Antwi, Mohamed Camara, Hassan Kibailo, Dennis Richard, Emmanuel Charlse, Henry Msabila.

Matokeo ya mechi zilizopita

Yanga SC ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wiliete katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwenye mchezo huu Yanga SC ilikuwa ugenini. Tayari Angola na tayari imesharejea Tanzania.

Yanga SC itaingia uwanjani ikiwa imetoka kupata ushindi ugenini. Mbali na mchezo huo wakiwa ugenini katika mchezo dhidi ya Simba SC ilishinda. Huo ulikuwa ni Ngao ya Jamii ulichezwa Septemba 16 2025. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC.

Soma hii: Wiliete SC 0-3 Yanga SC Caf Champions League 2025

Kwenye mechi mbili mfululizo ambazo ni ngumu Wanajangwani wamekuwa katika ushindi.Wachezaji na benchi la ufundi wamekuwa katika kicheko. Wanapewa nafasi kubwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo licha ya kwamba Pamba Jiji FC nao wanahitaji ushindi.

Wapinzani wao Pamba Jiji walikuwa ugenini kwenye mchezo wa ligi. Septemba 18 2025 walikuwa Uwanja wa Majaliwa. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Namungo FC 1-1 Pamba Jiji.

Kwenye mchezo huo Pamba Jiji walianza kufunga goli la uongozi dakika ya 19. Staphan Siwa anaingia kwenye rekodi ya kuwa mfungaji wa kwanza ndani ya Pamba Jiji FC. Kwa sababu huu ulikuwa ni mchezo wa kwanza msimu wa 2025/26.

Licha yakupachika goli dakika ya 19 bado safu ya ulinzi ilikosa umakini. Katika dakika za lala salama waliruhusu nyavu kutikiswa. Ni Abdulaziz Shahame dakika ya 90+7 alipachika goli la kuweka usawa.

H2H

Zimbwe Jr (-)
Zimbwe Jr wa Yanga SC anatarajiwa kuwa miongoni mwa kikosi dhidi ya Pamba Jiji Uwanja wa Mkapa. Source: Yanga SC.

Mechi mbili za ligi msimu wa 2024/25 Yanga SC ilipata ushindi zote. Katika dakika 180 msako wa pointi 6 zilibaki Jangwani. Hivyo Wananchi walikuwa na asilimia 100 ya kupata pointi mbele ya Pamba Jiji FC.

Oktoba 3 2024 ilikuwa Yanga SC 4-0 Pamba Jiji FC, mchezo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex. Februari 28 2025 Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC. Jumla mabao 7 Pamba Jiji FC ilifungwa na Yanga SC. Timu hiyo kutoka Mwanza katika dakika 180 safu ya ushambuliaji ilikwama kupata goli mbele ya wapinzani wao.

Wanakwenda kukutana kwa mara ya kwanza ndani ya msimu mpya. Yanga SC ni mabingwa watetezi wa ligi. Pamba Jiji FC hesabu zao itakuwa ni kuvunja rekodi ya kupoteza nje ndani.

Hitimisho

Yanga SC vs Pamba Jiji FC ni mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa na mashabiki wa mpira. Mchezaji anayetajawa kuwa na hatari zaidi Yanga SC ni Pacome ambaye ni kiungo. Pamba Jiji wao mchezaji tegemeo ni Kelvin Nashon.

image
Share this: