- CAF Champion League imeanza kwa kishindo mabingwa wa Tanzania wakipata ushindi mnono ugenini.
- Wiliete SC 0-3 Yanga SC magoli maridhawa kutoka kwenye miguu ya Wanajangwani ukurasa ukifunguliwa na Aziz Andambwile akiwa nje ya 18.
- Prince Dube alifanya majaribio sita kimataifa mikono ya kipa wa Wiliete SC ilikuwa imara katika kuokoa hatari licha ya kupoteza mchezo.
Wiliete SC 0-3 Yanga SC ushindi mnono kwa wawakilishi wa Tanzania wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa 11 de Novembro Septemba 19 2025. Ushindi huo unawafanya Wanajangwani kutembea kifua mbele wakiwa ugenini.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Kuna mamilioni yanakusubiri sasa hivi rubani bora. Ni rahisi sana kuyavuna ni kupitia Kindege cha SportPesa. Cheza Aviator upate mgao wako.

Wiliete SC 0-3 Yanga SC magoli yote haya hapa

Yanga SC iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 31 kufunga goli la kwanza. Ni kupitia kwa kiungo Aziz Andambwile. Goli hilo alifunga akiwa nje ya 18 kwa mguu wake wa kulia likamshinda mlinda mlango wa Wiliete.
Dakika 45 Wiliete walikuwa kwenye jitihada kurudisha goli hilo walikwama. Mikono ya kipa wa Yanga SC, Djigui Diarra ilikuwa imara katika kuokoa hatari. Ulinzi ulikuwa unaimarishwa chini ya nahodha Bakari Mwamnyeto.
Soma hii: Yanga SC watachuana na vijana wa Angola Wiliete SC CAF Champions League 2025
Edmund John alipachika goli la pili dakika ya 71akitumia pasi ya Maxi Nzengeli. Prince Dube alipachika goli la tatu dakika ya 79 akitumia pasi ya Ecua.
Mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano kimataifa
Kadi ya kwanza ya njano kwenye mchezo alionyeshwa mchezaji wa Yanga SC dakika ya 75. Anaitwa Duke Abuya. Huyu anakuwa mchezaji wa kwanza kwa Yanga SC kuonyeshwa kadi ya njano kimataifa.
Wachezaji waliofanyiwa mabadiliko
Maxi Nzengeli aliingia dakika ya 59 akichukua nafasi ya Clement Mzize. Doumbia alitoka aliingia Edmund John. Pacome alipata maumivu pia alitoka dakika ya 70 nafasi yake ilichukuliwa na Celestin Ecua.
Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliingia dakika ya 75 akichukua nafasi ya Ladack Boka. Aziz alitoka nafasi yake ilichukuliwa na Balla Conte
Super Sub
Wachezaji waliongia kipindi cha pili kwa Yanga SC walikuwa katika ubora. Maxi alitoa pasi moja ya goli na Ecua naye alitoa pasi ya goli. Edmund John yeye alifunga goli na alianzia benchi kipindi cha kwanza.
Waliopewa majukumu ya mipira ya faulo na kona

Kwa Yanga SC mpigaji wa kwanza wa faulo alikuwa ni Mohamed Doumbia. Huyu alipiga dakika ya tatu haikuleta goli kwa Yanga SC ikiwa ni faida kwa wapinzani. Kiungo huyo alipewa jukumu la kupiga kona dakika ya 19. Ecua alipewa jukumu la kupiga faulo dakika ya 88.
Baada ya Doumbia kutoka majukumu ya kupiga kona yalikuwa yakibadilishwa. Edmund John alipiga kona dakika ya 66. Pacome alipiga kona dakika ya 69.
Kituo kinachofuata Yanga SC vs Wiliete SC
Baada ya ushindi ugenini kituo kinachofuata kwa Yanga SC watakuwa Uwanja wa Mkapa katika mchezo wa ligi. Mchezo wa marudiano dhidi ya Wiliete SC unatarajiwa kuchezwa Septemba 27 2025. Wanajangwani mchezo ujao wakilinda ushindi wanasonga mbele hatua ya pili.
Soma hii: Wiliete SC vs Young Africans SC CAFCL: ‘LIVE’, vikosi, H2H, Utabiri, Yanga Yatua Angola kibabe
Septemba 24 Yanga SC itakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Pamba Jiji, Uwanja wa Mkapa. Ikiwa itafuzu hatua inayoafuata itakutana na mshindi kati ya mechi ya Elgeco Plus ya Madagascar na Silver Strikers ya Malawi. Mechi ijayo itakuwa katika raundi ya pili kusaka nafasi kutinga hatua ya makundi.
Prince Dube mashuti 6 goli moja
Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC alikomba dakika 90 na alifanya majaribio zaidi ya sita. Dakika ya 5 jaribio lake liliokolewa na mlinda mlango. Dakika ya 7 Dube alifanya jaribio la pili. Dakika ya 21 Dube kwa mara nyingine alifanya jaribio ambalo liliokolewa na kipa. Dakika ya 39 Dube alifanya jaribio lingine likaokolewa na kipa wa Wiliete SC Agustino Kalougha. .
Clement Mzize nafasi za dhahabu

Clement Mzize alikosa nafasi yakufunga dakika ya 7 akiwa ndani ya 18 kwa jaribio la pigo la kichwa. Dakika ya 13 Mzize akiwa ndani ya 18 jaribio lake lilikwenda nje ya lango. Kazi haikuwa ndogo uwanjani kwa Mzize ambaye alikuwa akipewa pasi za upendo na Pacome.
Dakika ya 28 Mzize akiwa ndani ya 18 jaribio lake la mguu wa kushoto linakwenda nje ya lango. Alipewa pasi kutoka kwa Doumbia. Mzize katika harakati za kuokoa hatari alipata maumivu dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Hitimisho
Wiliete SC 0-3 Yanga SC ni mchezo uliokuwa na kasi kubwa. Vijana wa Jangwani walikuwa wakishambulia bila kuchoka huku Wiliete SC wakiwa katika kazi ya kujilinda. Mchezo wa pili utaamua mshindi ambaye atasonga mbele hatua inayofuata.


