- Gaborone United 0-1 Simba SC, ndivyo ubao umesoma huko Botswana.
- Licha ya ushindi huo, habari kubwa kuwahusu Wanamsimbazi ni Je, Kocha Fadlu Davis anaondoka Simba SC?
- Hii ni baada ya utata mzito kuibuka, huku uongozi wa Simba SC ukitoa tamko zito
Achana na ushindi mwembamba ambao wameupata dhidi ya Gaborone United kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Taarifa ambayo imekuwa gumzo kubwa kutoka unyamani ni je, kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC? Makala hii inakuja na majibu mazito ikiwemo tamko la uongozi wa Wanamsimbazi.
SOMA HII PIA: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC anatajwa Raja Casablanca, Maxi, Farid Mussa kuondoka
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Wachambuzi waibua mazito, kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC?
Sakata la kuondoka kwa Fadlu Simba kwa kiasi kikubwa limechochewa na taarifa mbalimbali za wachambuzi wa soka. Hapa tunajadili baadhi ya taarifa hizo:
Hans Raphael

“Kuanzia jana (Ijumaa), Simba SC walianza kutafuta kocha mpya wa kurithi mikoba ya Fadlu. Ukweli ni kwamba Fadlu amegoma kubadilisha msimamo wake, kuna uwezekano mkubwa baada ya mechi leo ikatoka taarifa kwa umma. Usiku wa kuamkia Leo Raja Casablanca wametimua kocha wao, huku Fadlu akitarajiwa kuchukua mikoba yake. Simba Tayari wameanza kujiandaa na maisha mapya bila Fadlu.
“Kuhusu habari za Fadlu kuhitajika na vilabu mbali mbali Africa zilikuwepo tangu msimu jana na ofa zilitumwa za kutosha, ila Fadlu alikataa kwa sababu alikuwa na furaha msimbazi.
“Baada ya Dabi ya juzi baadhi ya Viongozi wa Simba na mashabiki walimtia pressure, matusi na lawama za kutosha. Ndipo Fadlu akabadili msimamo wake na kuanza kusikiliza ofa za nje. Binafsi ni shabiki mkubwa na Fadlu na ningetamani abaki, ila watu wamemtishia sana baada ya kupoteza dabi na yeye ameona ni bora kusikiliza ofa za nje.”
SOMA HII ZAIDI: MO Dewji aibua jambo Simba SC| Fadlu Davids kwenye majukumu makubwahttps://blog.sportpesa.co.tz/2025/07/17/mo-dewji-aibua-jambo-simba-sc/
Ibrahim Maestro
kwa mujibu wa Mwandishi Mkongwe, Maestro wa EFM amesema: “Kumekuwa na mvutano ya majaaliwa ya fadlu ndani ya Simba SC. Kocha haamini vipigo vya Yanga vinatokana na Kiufundi, analalama kuwa Wachezaji aliowataka wameenda kwa Mpinzani. Kingine amesema pia anaumizwa na miundombinu ya Uwanja wa mazoezi wa Simba, hivyo machache kati ya mengi ni kuwa mwalimu kwasasa anataka kuondoka.”
Saleh Jembe

Kwa mujibu wa mwandishi, Saleh ni kuwa Fadlu ameshikilia msimamo kuwa anataka kuondoka, lakini ametoa ofa kwa Simba kuwa ataendelea na kazi kwa siku mbili. Hii ina maanisha atakuwa kwenye benchi katika mechi ya kwanza ya Caf Champions League dhidi ya Gaborone United. Uongozi umefanya juhudi kubwa Ikiwa ni pamoja na kumuongezea maslahi. Lakini wapi, kashikilia msimamo wake na haelezi sababu ya msingi.”
SOMA HII PIA: Simba SC yamtambulisha mrithi wa Zimbwe Jr 2025/26 Naby Camara/ Orodha ya wachezaji wapya hii hapa
Jemedari Said

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameamua kuachana na klabu hiyo. Fadlu analalamikia mazingira ya kazi, ni kama ana hofu ya usalama kitu ambacho ameshindwa kuweka wazi moja kwa moja. Viongozi wa Simba SC wamejitahidi kumbembeleza abadilishe msimamo wake huo, lakini amekataa katakata. Rais wa heshima wa klabu, Mohamed Dewji amemaliza mbinu za kumbembeleza Fadlu ikiwemo kumuongeza mshahara wake.
“MO amemtaka, Fadlu aseme anataka aongezwe kiasi gani (Open Check), lakini Fadlu anasema ameshafanya maamuzi ya kuondoka na harudi nyuma. Viongozi wa Simba wamemuachia yeye Fadlu ndiyo aamue kama ni kuvunja mkataba basi avunje, na aje autangazie umma kwamba ameamua kuondoka klabuni hapo. Mwanzo Fadlu alitaka wafikie makubaliano ya pande zote mbili, Simba wamekataa hilo wanajiondoa kuonekana wamemfukuza.
“Inasemekana klabu ya nyumbani kwao Afrika Kusini ya Kaizer Chiefs ndiyo imempagawisha, baada ya kumpa ofa kubwa ya mshahara wa dola za Kimarekani 80,000/. Raja Casablanca pia inatajwa kwenye mbio za kumrejesha Kocha huyo, ambaye kabla ya kuja Simba alikuwa huko. Yuko na timu Francis Town, lakini amefanya maamuzi ya kuondoka, na alitaka hata huko Francis Town asiende aishie Gaborone tu.
Hitimisho: Tamko la uongozi wa Simba SC

Kufuatia taarifa za kocha Fadlu Davis kuondoka Simba SC kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika, Simba nao kupitia kwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wao, Ahmed Ally akilisemea hilo amesema: “Focus yetu kubwa ni mchezo wetu dhidi Gaborone United, kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika mchezo huo. Mwalimu Fadlu na Benchi lake lote wapo kazini, kuhakikisha tunapata matokeo mazuri Insha Allah. Kwa sasa Wana Simba tujielekeze kwenye kutafuta ushindi.”

