Nado Azam FCNado Azam FC
  • Mashindano ya kimataifa Afrika yanazidi kushika kasi huku upinzani ukizidi kuwa mkubwa kutokana na mamilioni ambayo yanatolewa.
  • CAF Confideratin Cup mbili kutoka Tanzania kazini kusaka ushindi ugenini kwenye anga la kimataifa.
  • Simba SC ikiwa imetoka kujeruhiwa kwenye kibarua kizito ugenenini bila ya uwepo wa beki wa kazi Hamza Jr

Kimataifa hakupoi ni mwendelezo wa dakika za msako wa ushindi Septemba 20 2025. Simba SC ya Tanzania ipo kwenye CAF Champion League. Klabu ya Azam FC na Singida Black Stars CAF Confideration Cup mbili kutoka Tanzania zitakuwa kwenye uwajibikaji. Timu zote hizi zipo katika hatua ya awali zitakuwa ugenini.

Vuna mamilioni na Kindege cha SportPesa

Ni mwendo wa kuvuna mamilioni ukiwa hewani na Kindege cha SportPesa. Rahisi sana kushinda na inawezekana. Cheza Aviator upate mgao wako sasa hivi.

image

CAF Confideration Cup mbili kutoka Tanzania kazini

CAF Confideration Cup mbili kutoka Tanzania
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Singida Black Stars. Source: Singida Black Stars.

Azam FC kutoka Tanzania na Singida Black Stars ni mbili CAF Confideration Cup kutoka Tanzania ambazo zitakuwa kazini. Azam FC itakuwa Uwanja wa taifa wa Juba kuvaana na El Merriekh Bentiu. Huu ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni hatua ya awali. Mchezo huu utachezwa Sudan ya Kusini saa 4:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Ibenge Kocha Mkuu wa Azam FC kuhusu wapinzani wao

Florent Ibenge Kocha Mkuu wa Azam FC ameweka wazi kuwa wanawatambua vema wapinzani wao. Kocha huyo amesema wanatambua watakuwa na mchezo mgumu ila wapo tayari. Aliongeza maandalizi waliyofanya yanawapa nguvu kuwakabili uwanjani.

“Tunajua kwamba El Merriekh nitimu kubwa na ina ushindani mkubwa. Tunatambua kwamba kuna wachezaji kutoka timu hiyo ambao wapo katika timu ya taifa. Tunajua kwamba tunakwenda kucheza na timu kubwa. Tuliona hasa michezo yetu iliyopita na namna ambavyo wanacheza. Wapinzani wetu wapo imara wakiwa na aina ya wachezaji tofauti.

Soma hii: Droo ya Caf Champions League 2025/26

“Hivyo tutaingia kwenye mchezo wetu tukitambua kwamba kuna uimara mkubwa kwa wapinzani wetu. Nahodha wangu anajua kwamba tuna mchezo mgumu. Aina ya wachezaji wao na namna ambavyo wanapambana. Tumaini letu ni kupata matokeo kwa kuwa tunakutana na timu ambayo ina vijana wajanja uwanjani,” amesema Ibenge.

James Akaminko nyota wa Azam FC

Kiungo mkabaji wa Azam FC, James Akamiko amebainisha kuwa wapo ugenini kwa ajili ya kazi. Akamiko aliongeza kwa kusema maandalizi ambayo wamefanya malengo makubwa ni kupata ushindi. Hivyo wanaamini wataingia uwanjani wakijiamini na kushirikiana kutafuta matokeo mazuri.

“Sudani Kusini ni nzuri siwezi kusema mengi kwa sababu hatujaja hapa kufurahia. Tunajua ambacho tumekifuata ni ushindi kwenye mchezo wetu ujao. Tumekuja kufanya kazi hivyo tupo hapa kwa ajili ya mechi na tunatazamia kutoa kilicho bora kwenye mechi yetu.”

Wachezaji wa Azam FC waliopo Sudan Kusini

Lameck Lawi
Lameck Lawi nyota wa Azam FC. Source: Azam FC.

Mbali na James Akaminko wachezaji wengine wa Azam FC waliopo huko ni Feisal Salum. Kiungo huyu anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa kuchungwa kuelekea mchezo wa kimataifa. Idd Suleman, Muhsin Imalima, Baraket Ihmid. Papa Diallo,Nassor Saadun, Zidane. Lameck Lawi nao wapo Sudan Kusini.

Singida Black Stars CAF Confideration Cup

Singida Black Stars inayofundishwa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi itakuwa kazini kwenye mchezo dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Uwanja wa Kigali Pele ikiwa ni hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika Septemba 20.

Hiki hapa kikosi kamili cha Singida Black Stars

Chama Rwanda
Chama Clatous na wachezaji wa Singida Black Stars nchini Rwanda. Source: Singida Black Stars.

Soma hii: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB, Ngoma kupigwa Zanzibar 28/06/2025

Metacha Mnata, Hussen Masalanga, Amas Obasogie, Kennedy Juma. Anthony Trabi, Mukrim Issa, Ande Koffi, Kelvin Kijili. Nickson Kibabage, Gadiel Michael, Morice Chukwu, Mohamed Damaro, Khalid Habib, Aboubakari Muhajiri huyu kutoka U 20.

Khalid Aucho, Idriss Diomande, Kwame Kekeyek, Marouf Tchakei, Clatous Chama, Deus Kaseke. Rashid Said, Lamin Jarjou,Andrew Phiri, Daud Mishamo, Elvis Rupia na Horso Muako.

Simba SC CAF Champions League

Simba SC kutoka Tanzania itakuwa na kazi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Ni mchezo wa hatua ya awali ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ambaye atakosa hudumu ya beki Hamza Jr aliyepata maumivu mchezo dhidi ya Yanga SC.

 Itakuwa ni Gaborone United vs Simba SC. Uwanja wa Francistown mchezo huu utachezwa. Saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba SC na historia yake kimataifa

Katika anga la kimataifa Simba SC ina historia nzuri. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 ilikuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika. Katika mashindano hayo ilicheza fainali.

Iliishia nafasi ya pili kwa kupoteza dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Mchezo wa kwanza ugenini ilipoteza kwa kufungwa magoli 2-0. Fainali ya pili Tanzania, walitoshana nguvu kwa kufungana goli 1-1 huku Joshua Mutale akifunga kwa Simba SC.

Mnyama anaingia akiwa na maumivu aliyopata katika mchezo uliopita dhidi ya Yanga SC. Ni goli 1-0 ilipoteza kwenye Kariakoo Dabi hivyo hasira zake zinatarajiwa kuwa katika anga la kimataifa. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Tanzania.

Kuna mamilioni kutoka CAF

Kuna mamilioni kutoka kwa waandaaji wa mashindano haya amba oni CAF. Timu zote ambazo zinashiriki hatua ya awali CAF zinapata dola 100,000 zaidi ya milioni 240. Kwa maana hiyo ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa kila hatua.

Hitimisho

CAF Confideration Cup mbili kutoka Tanzania zitakuwa kazini. Hizi ni mechi za maamuzi katika dakika 180. Mshindi wa mchezo wa mwisho anakata tiketi kusonga mbele hatua ya pili katika anga la kimataifa.

image
Share this: