Shomar KapombeShomar Kapombe
  • Ligi ya Mabingwa Afrika mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (CAF) yanaanza kurindima katika hatua za awali.
  • Gaborone United vs Simba SC huu utachezwa Jumamosi ya Septemba 20 Uwanja wa Francistown.
  • Simba SC itamkosa beki kisiki Abdulazak Hamza ambaye alipata maumivu kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC.

Gaborone United vs Simba SC Septemba 20 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utacheza ikiwa ni hatua ya awali. Uwanja wa Francistown utawaka moto wababe hawa wakiwa uwanjani. Tayari msafara wa wekundu wa Msimbazi umeshawasili nchini Botswana kwa maandalizi ya mwisho.

Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi

Ni muda wa kuvuna mamilioni sasa hivi kwa mchongo wa maana. Rahisi sana kwako rubani ukipaisha Kindege cha SportPesa. Cheza Aviator sasa upate mgao wako.

image

Gaborone United vs Simba SC Ahmed Ally aunguruma

Gaborone United vs Simba SC
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Droo ya Caf Champions League 2025/26

Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC amebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo. Maandalizi ambayo wanayafanya wanaamini watapata matokeo mazuri. Ameweka wazi kuwa hakuna timu yakubeza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunamshukuru Mungu tumewasili salama hapa Gaborone. Wapinzani wetu hapa tulipo ndio makao makuu yao. Mechi yetu imepelekwa katika mji Francistown ambako ndipo mchezo utapigwa.

“Kwanza tunapaswa kuwaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa sio timu yakubeza. Ni mpinzani ambaye tumeona kwamba nguvu yake ipo katika eneo lipi. Tumejua kwamba ipo kwenye eneo la ushambuliaji.

“Lakini inabidi utambue kwamba hii ni Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika mashindano haya hakuna ambaye anakubali kufanya vibaya. Nguvu ya michuano ya Afrika haina mwenyewe popote timu inafanya vizuri.

“Tunatakiwa kuwa makini na kufanya kila tunachoweza kuwadhoofisha tukiwa nyumbani kwao. Ikiwa itakuwa hivyo mechi ya Dar itapunguza presha kutoafuta matokeo kwetu.

“Mpaka sasa tunafanya maandalizi sisi wenyewe, mratabu wa timu alishatangulia. Hatujaingia kwenye mamlaka ya Gaborone United. Tukiwa mikononi mwao tutajua kipi ambacho kimekwenda sawa na kipi ambacho hakijaenda sawa. Kuhusu hali ya hewa ni tulivu inatupa nafasi sisi yakucheza na kupata matokeo kwenye mchezo wetu ujao.

H2H

Septemba 20 2025 wanatarajiwa kukutana Gaborone United vs Simba SC. Mchezo wa pili unatarajiwa kuwakutanisha wababe hawa ni Septemba 28 2025, Tanzania.

Hiki hapa kikosi cha Simba SC

Wachezaji 23 wapo kwenye Botswana kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa. Ni makipa watatu, mabeki 6 huku kukiwa na viungo 11. Washambuliaji wapo watatu kwenye orodha hiyo.

Makipa

Moussa Camara, Yakoub Suleiman na Alexender Erasto.

Mabeki

Shomari Kapombe, Anthony Mligo. Rushine De Reuck, Wilson Nangu, Naby Camara.

Viungo

Yusuph Kagoma, Allasane Kante, Kibu Dennis, Ellie Mpanzu. Ladack Chasambi, Mzamiru Yassin, Neo Maema. Joshua Mutale, Jean Ahoua, Daud Semfuko Morice Abraham.

Washambuliaji

Steven Mukwala, Seleman Mwalimu, Jonathan Sowah.

Ahmed Ally amewataja wachezaji watakaokosekana kwa Simba SC

Hamza (-)
Hamza beki wa Simba SC ambaye atakosekana Septemba 20 katika mchezo wa CAF. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC 1-0 Simba SC: Highlights, magoli yote, h2h – Ngao ya jamii 2025

Ahmed amesema: “Abdluzak Hamza beki huyu alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC. Nyota huyu alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo wetu uliopita.

“Hamza anaendelea na matibabu na aliumia vibaya. Mchezaji mwingine ni Mohamed Bajaber anaendelea na matibabu. Niweke sawa kwamba huyu tulimsajili akiwa na majeraha na alipewa muda ili kurejea kwenye ubora. Naye hatujasafiri naye ili aendelee kupata matibabu.

Kuhusu kupoteza mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC

Profesa Pacome
Pacome nyota wa Yanga SC ambaye alifunga goli la ushindi dhidi ya Simba SC. Source: Yanga SC.

Soma hii: Goli la Pacome Zouzoua ni offside au onside? | Wachambuzi wajibizana Edo Kumwembe vs Jemedari – SportPesa Tanzania

 Ahmed amesema: “Ni kweli tumetoka kwenye mchezo mgumu na hatujapata matokoe mazuri kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii. Kwa mpambanaji huwezi kukubali kukosa vitu vyote viwili. Tumepoteza Ngao ya Jamii hiyo inatuongezea nguvu kupambana kwa ajili ya mechi zetu zijazo. Haijatunyong’onyesha. Haijatuondolea pawa hivyo bado tupo kwenye ushindani,” amesema Ahmed kupitia Azam TV.

Kikosi cha Gaborone United

Mlinda mlango ni Thabo Motswagole. Viungo ni :-Sheikh Seasy, Thatayaone Kgamanyange, Lebogang Ditsele, Nikolay Pantey, Karabo Phiri. Washambuliaji ni Thomas Chideu, Thabo Maponda, Mpho Kgaswane. Mabeki ni Ivan Kamberipa, Mathusi Jonhson, Alford Velaphi, Omphile Ramoagi, Thato Kebue, Tshepo Maikano, Thabang Khuduga.

Kuhusu Gaborone United

Gaborone United inashiriki Ligi Kuu ya Botswana. Ni miongoni mwa timu ambazo zimeanza vema msimu wa 2025/26. Baada ya mechi nne za ligi ilipata ushindi katika mechi tatu na kutoshana nguvu katika mchezo mmoja.

Uimara wake upo katika eneo la ushambuliaji. Kwenye mechi nne za ligi rekodi inaonyesha kuwa ni mabao 10 ilifunga. Umri wa wachezaji wake wengi ni kati ya miaka 29.

Hitimisho

Gaborone United vs Simba SC Septemba 20 itakuwa moto. Wababe hawa wawili wanasaka nafasi kutinga hatua ya makundi. Zitakuwa dakika 90 ugenini kwa Mnyama na Gaborone United wanatarajiwa kuwa ugenini Septemba 28 Tanzania.

image
Share this: