- Dakika 90 Yanga SC yampa kichapo Kocha, Fadlu Davis wa Simba SC na kubeba taji.
- Pacome Zouzoua aipa Yanga SC bao moja la kipekee la ushindi dhidi ya Simba SC kwenye Ngao ya Jamii.
- Yanga SC 1-0 Simba SC, ndivyo ubao wa matokeo ulivyosoma, huu unakuwa ushindi wa 6 mfululizo kwa Yanga SC katika mchezo wa dabi dhidi ya Simba SC.
Ubishi kwisha! Baada ya tambo za muda mrefu, hatimaye ubao wa Uwanja wa Benjamin Mkapa umesomeka Yanga SC 1-0 Simba SC. Bao pekee la kiungo Zouzoua Pacome limefanikiwa kuipa Yanga ubingwa mwingine wa Ngao ya Jamii. Hii inakuwa rekodi mpya ya Dabi ya Kariakoo, ambapo Yanga wamefanikiwa kushinda mechi 6 mfululizo.
SOMA HII ZAIDI: Uchambuzi wa Yanga SC vs Simba SC itakayochezwa Septemba 16 | H2H, vikosi, matokeo, wafungaji
Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu
Bado hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.

Matokeo ya Simba vs Yanga 2025 yalikuwaje?

Yanga SC waliweza kuichapa Simba SC bao moja kwa nunge kwenye fainali ya Ngao ya Jamii. Kupitia bao la Pacome alilofunga dakika ya 54. Wekundu wa Msimbazi walipoteza nafasi kadhaa za kupata bao, huku Djigui Diarra akilinda lango kwa ustadi mkubwa.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC vita ya ubingwa bado inaendelea/ Timu zilizoshuka, matokeo raundi ya 30
Wachezaji waliotisha kwenye Kariakoo Dabi 2025

Miongoni mwa wachezaji walioonyesha ubabe kwenye mechi hii walikuwa ni: Pacome Zouzoua, Djigui Diarra, Rushine De Reuck na Mohamed Doumbia. Kupitia wachezaji hawa fainali ilionyesha kuwa na upinzani mkubwa.
Hans apagawa na Doumbia
Mchambuzi wa michezo, Hans Raphael akimuelezea, Doumbia baada ya mechi aliandika: “Quality,Quality,Quality. Niliwaambia huyu Jamaa ni Superstar. Anaitwa Mohamed Doumbia (26), ukipenda muite “Midfield Pimper”. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kucheza kwenye maeneo finyu,kupiga mashuti ya mbali yenye usahihi.
“Pamoja na hayo, Doumbia ana akili ya kutengeneza nafasi kwa wengine. Hii ndio maana halisi ya mchezaji mwenye X-factor. Ni Kweli Pacome kafunga bao la ushindi, Diarra kafanya Saves muhimu, ila kwangu mimi Doumbia ndo Man Of the Show.
“Kipindi cha kwanza Yanga walikosa ubunifu, uthububu na ile pasi ya mwisho ya kuifungua safu ya ulinzi ya Simba. Kipindi cha pili kocha wa Yanga SC Folz, akaona siyo kesi na kumwambia Doumbia zama ndani na hapo kila kitu kilibadilika. Pacome, Mzize, Maxi na Ecua wakaanza kupewa pasi za upendo kwenye maeneo hatari.
“Kitu kingine nimegundua Doumbia ni “Pressing machine” jamaa ana-press, kwanza ana akili sana. Halafu akiiba mali anaachia pasi ya upendo. Top Top Top Midfielder.”
Yanga SC vs Simba SC h2h, Wananchi waendeleza uteja kwa Mnyama

Kipigo cha Simba SC leo kinakuwa cha 6 katika mechi za mfululizo wa hivi karibuni. Huku rekodi ikionyesha Yanga wamekuwa na wastani mzuri zaidi. Wababe hao wa Kariakoo katika rekodi ya hivi karibuni wamekutana mara 32, Yanga SC wameshinda mechi 13, Simba SC wameshinda mechi 7 pekee, huku mechi 12 zikienda sare.
Rekodi za matokeo ya mechi zilizopita za fainali za Yanga SC vs Simba SC:
2017- Simba SC 5-4 Yanga SC, mshindi alipatikana kwa penati, baada ya kutofungana kwenye muda wa kawaida.
2021- Yanga SC 1-0 Simba SC.
2022- Yanga SC 2-1 Simba SC.
2023- Simba SC 3-1 Yanga SC, mshindi alipatikana kwa penati. Baada ya kutofungana.
Vikosi vya Yanga SC na Simba SC

Yanga SC 1-0 Simba SC, hivi hapa vikosi vilivyoanza kwenye hesabu ya nyota 11 wa kila timu;
Yanga SC
Djigui Diarra, Israel Mwenda, Chadrack Boka, Ibrahim Baka, Dickson Job, Aziz Andambwile, Maxi Nzengeli, Duke Abuya, Prince Dube, Zouzoua Pacome na
Simba SC
Moussa Camara, Shomari Kapombe, Naby Camara, Abdalazak Hamza, Allasane Kante, Kibu Denis, Yusuph Kagoma, Steven Mukwala, Jean Ahoua na Elie Mpanzu.
SOMA HII PIA: Kizungumkuti Yanga SC vs Simba SC Kariakoo Dabi/ Mechi ipo au haipo?
Hitimisho
Yanga SC 1-0 Simba SC ndio matokeo halisi kwenye mechi fainali ya Ngao ya Jamii. Huu utakuwa bingwa wao wa 9 kwenye mashindano haya. Hii inawafanya Wananchi kuingia kwenye rekodi ya kuwa miongoni mwa timu zilizoshinda ubingwa huu mara nyingi zaidi.

