- Pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26 linakwenda kufunguliwa huku ushindani ukitarajiwa kuwa mkubwa zaidi.
- Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara inafunguliwa upya kwenye mchezo wakukata na shoka Septemba 16 2025 Uwanja wa Mkapa.
- Zimbwe Jr beki wa kazi ndani ya Yanga SC kunogesha shughuli nzima kutokana na ubora wake na uzoefu alionao.
Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara inaanza upya. Hawa ni makipa chaguo la kwanza katika timu wanazotumikia. Djigui Diarra yupo kikosi cha Yanga SC na Moussa Camara ndani ya Simba SC wanatarajiwa kukutana Septemba 16 2025 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
Paisha Kindege cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Muda ni sasa kushinda mamilioni ukicheza mchezo wa Aviator. Ni rahisi sana kwa kila rubani kuvuna mamilioni. Cheza sasa upate mgao wako bila chenga.

Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara itakuwa wazi

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji
Kwenye kukusanya hati safi katika Kariakoo Dabi, kipa wa Simba SC Moussa Camara hakuwa na bahati. Djiguia Diarra kipa namba moja wa Yanga SC alimpoteza Moussa Camara wa Simba SC kila walipokutana. Dakika 270 zote shujaa alikuwa ni Diarra, hivyo kuelekea Kariakoo Dabi vita ya Djigui Diarra na Moussa Camara inaanza upya.
Hapa tunazungumzia mechi tatu ambazo watani wa jadi walikutana msimu wa 2024/25. Katika mechi hizo tatu moja ilikuwa ni Ngao ya Jamii. Mechi mbili ilikuwa ni Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC.
Vita ya Diarra na Camara kwenye ligi

Soma hii: Kariakoo Dabi mchezo wa watani wa jadi Yanga SC vs Simba mechi ipo Juni 15 2025
Kiujumla kwenye mechi za ligi msimu wa 2024/24 Camara alikuwa namba moja. Diarra alikuwa anafuata. Hii ilitokana na mechi ambazo alikaa langoni.
Camara alikusanya jumla ya hati safi 19 kibindoni. Camara alikaa langoni kwenye mechi 28 akifungwa mabao 13. Mechi mbili Ally Salim alikaa langoni kwa Simba SC na hakufungwa. Jumla Camara alitumia dakika 2,520 msimu wa 2024/25.
Diarra ni mechi 23 alikaa langoni alitumia dakika 2,070. Alikusanya hati safi 17 akifungwa mabao 8. Juni 22 2025 hakuwa langoni dhidi ya Dodoma Jiji, Aboutwalib Mshery alikaa langoni. Baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji.
Kariakoo Dabi vita yao wababe hawa
Katika Ligi Kuu Bara 2024/25 mechi zote mbili, nje ndani Simba SC ilipoteza. Simba SC 0-1 Yanga SC mchezo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 2025, goli lakujifunga Kelvin Kijili dakika ya 88.
Yanga SC 2-0 Simba SC mzunguko wa pili ilikuwa Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa. Magoli ya Pacome Zouzoua ambaye alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo na Clement Mzize. Kwenye mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 1-0 Simba SC ilikuwa Agosti 8 2024.
Diarra na mataji ndani ya 2024/25
Akiwa na uzi wa Yanga SC, Diarra alikuwa miongoni mwa walionyanyua makwapa kutwaa mataji. Yanga SC ilifungua pazia kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii, taji la NBC msimu wa 2024/25. Pia taji la CRDB Cup lipo mikononi mwao.
Kwenye ligi kulikuwa na ushindani mkubwa na tofauti yao ilikuwa ni pointi nne na watani zao wa jadi. Yanga SC ilikamilisha msimu ikiwa na pointi 82. Simba SC ilikamilisha msimu ikiwa na pointi 78.
Diarra na Camara wote wapo fiti

Soma hii: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC 2025/26
Makipa hawa wawili wote wapo fiti kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi Septemba 16 2025. Diarra alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Bandari FC. Kwa upande wa Camara naye alianza kikosi cha kwanza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia.
Wote wawili baada ya dakika 90 walitoka na hati safi. Septemba 10 2025 kilele cha Simba Day ilikuwa Simba SC 2-0 Gor Mahia. Septemba 12 2025 kilele cha Yanga Day ilikuwa Yanga SC 1-0 Bandari FC.
Bado wapo ndani ya timu zao wanatarajiwa kuanza kwa mara nyingine kwenye Kariakoo Dabi. Camara hajawa na bahati kwenye mechi kubwa kutokana na kukwama kukusanya hati safi. Diarra amekuwa shujaa mara zote wanapokutana jambo linaloongeza ushindani kwa wawili hawa.
Zimbwe Jr kunogesha shughuli yenyewe
Beki wa kushoto Mohamed Hussen Zimbwe Jr anatajwa kunogesha shughuli. Sababu kubwa ya Zimbwe kunogesha mchezo huo ni kuwatambua vema makipa wote, Camara na Diarra. Kabla ya kujiunga na Yanga SC alikuwa ndani ya Simba SC.
Hivyo miongoni mwa nyota ambao watakuwa wakifuatiliwa kwa ukaribu ni Zimbwe Jr. Hata kwenye utambulisho Yanga Day jina lake lilishangiliwa.Hii inatokana na uwezo alionao kwenye kuzuia na kufunga magoli pia.
Huyu hapa Zimbwe Jr :”Tamasha limeenda vizuri kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mashabiki wamejitokeza wengi na hii ni ishara kuwa huu ni mwanzo mzuri kuelekea katika msimu mpya.
“Kuna vipaji vingi ambavyo vipo ndani ya Yanga SC na nina amini kwamba nami nimeongezeka. Ninashukuru kwa kuwa nipo katika timu ambayo ina talent kubwa.
“Ninaona mbali zaidi kwa kuwa kila mchezaji anaipigania nembo ya timu nami nimeongezeka. Wananchi ninawapenda na nina amini tutakuwa kwenye kazi kubwa kwa ajili ya kufikia mafanikio,”.
Hitimisho
Kariakoo Dabi vita ya Diarra na Camara inaanza upya uwanjani Septemba 16. Kila mmoja anatarajiwa kuwa kazini kutimiza majukumu yake.Huu ni mchezo wa kufungua pazia la msimu wa 2025/26.


