Mpanzu Misri (-)Mpanzu Misri (-)
  • Elie Mpanzu winga mwenye spidi akiwa uwanjani yupo kambini Misri kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26 akizima tetesi zilizokuwa zinaeleza kuwa ataondoka.
  • Simba SC ilibaki kidogo kumkosa Mpanzu ambaye alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za watani zao wa jadi Yanga SC.
  • Mpanzu ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids akiwa na uwezo wakufunga magoli mazuri na kutengeneza pasi za magoli.

Elie Mpanzu Kibisawala ni Simba SC 2025/26 akizima zile tetesi za kupigiwa hesabu na Yanga SC. Elie anacheza nafasi zaidi ya mbili uwanjani winga na mshambuliaji na mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia. Msimu wa 2024/25 aliandika rekodi tamu kwenye magoli na pasi za magoli jambo lililomuongezea thamani sokoni.

Vuna mamilioni sasa hivi na Aviator

Muda ni wako sasa rubani makini kuvuna mamilioni. Rahisi sana unachotakiwa kufanya ni kucheza Aviator ushinde mkwanja wako. Kuna mgao wa mamilioni kila siku unakusubiri.

Aviator banner

Mpanzu rekodi zake katika Ligi Kuu Bara ya NBC

Mpanzu v Mashujaa
Elie Mpanzu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Mpanzu atua kwa kishindo Misri, Simba watoa tamko zito

Katika Ligi Kuu Bara inayodhamiwa na NBC 2024/25 Mpanzu alikuwa chaguo la kwanza. Licha ya kuwa ni ingizo jipya dirisha dogo la usajili. Alicheza jumla ya mechi 17 kati ya 30 ambazo Simba SC ilicheza msimu uliopita.

Rekodi zinaonyesha kuwa alitumia jumla ya dakika 1,239. Alifunga mabao manne na kutoa pasi tatu za mabao. Alihusika kwenye mabao 7 kati ya 69 ambayo yalifungwa na Simba SC kwenye ligi.

Simba SC ilikuwa ni timu namba mbili kufunga mabao mengi ndani ya ligi. Kwenye msimamo pia Simba SC ilimaliza ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 78. Timu namba moja ni Yanga SC iliyofunga jumla ya mabao 83.

Hizi hapa timu ambazo alizifunga Mpanzu

Alifungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex ilikuwa ni Februari 11 2025. Alipachika bao hilo dakika ya 44 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18.

Alipachika bao la pili kwenye mchezo dhidi ya Azam FC. Ilikuwa ni Februari 24 2025. Bao hilo alipachika dakika ya 25 kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18.

Mpanzu vs KenGold
Mpanzu dhidi ya KenGold mchezo wa ligi 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC hawa wachezaji wakuchungwa Juni 15 2025

Mpanzu alipachika bao la tatu kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji. Mchezo huo ulichezwa Machi 14 2025, Uwanja wa KMC Complex.Ni dakika ya 15 Mpanzu alifunga bao hilo kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18.

Kete yake ya nne ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya KenGold. Mpanzu alifunga bao dakika ya 22 akiwa nje ya 18. Ni mguu wa kulia alitumia ilikuwa Juni 18 2025. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia kwa kuwa mabao yote manne kafunga kwa kutumia mguu huo.

Mpanzu kwenye anga la kimataifa

Ellie Mpanzu kwenye mechi za kimataifa alikuwa kwenye ubora wake. Ni Kombe la Shirikisho Afrika Simba SC ilikuwa inapeperusha bendera ya Tanzania. Ilicheza fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Kwenye mechi zote ambazo alikuwa anapewa nafasi ya kuanza Mpanzu alikuwa akitimiza majukumu yake kwa umakini. RS Berkane walifanya kazi kubwa kumzuia ugenini na nyumbani. Simba SC iligotea nafasi ya pili kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane katika fainali.

Robo fainali alifunga goli la kiwango

Katika mchezo dhidi ya Al Masry hatua ya robo fainali, Uwanja wa Mkapa Mpanzu alifunga goli la kiwango. Bao hilo alifunga akiwa nje ya 18 liliwanyanyua mashabiki wa Simba SC waliokuwa wakisaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali. Goli la pili lilifungwa na Steven Mukwala akitumia pasi ya nahodha Mohamed Hussen ambaye amesajiliwa na Yanga SC.

Simba SC ilipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Al Masry. Kwa kuwa mchezo wa kwanza walipoteza kwa kufungwa magoli 2-0 ikawa ni 2-2. Mshindi alipatikana kwa mikwaju ya penati, Simba SC 4-1 Al Masry. Ikawa ni safari kwa Simba SC kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Nusu fainali kwa Simba SC

Ellie Mpanzu
Ellie Mpanzu winga wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Soma hii: Ellie Mpanzu hauzwi Simba SC, RS Berkane kunyonyolewa

Mpanzu alikuwa mchezaji muhimu katika mechi za kila hatua ikiwa ni ile ya nusu fainali dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini. Kwenye mechi zote mbili ambazo ni dakika 180 Simba SC haikufungwa. Wakiwa nyumbani Uwanja wa New Amaan walipata ushindi wa goli 1-0.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza kiungo Jean Ahoua alifunga bao pekee la ushindi. Licha ya Ahoua kufunga kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 alikosa nafasi ya wazi kufunga goli dakika ya 90. Nafasi hiyo ya dhahabu alitengenezewa na winga Ellie Mpanzu.

Ugenini dhidi ya Stellenbosch FC Mpanzu alikomba dakika 86. Nafasi yake ilichukuliwa na beki Che Malone ambaye alikuwa nje kwa muda. Dakika 4 zilikuwa maalumu kumrejesha Che Malone kwenye ubora baada ya kutoka kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.

Che Malone kwa msimu wa 2025/26 hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC. Beki huyo amepata changamoto nyingine katika Klabu ya USM Alger ya Algeria. Tayari ameanza maandalizi ya msimu mpya akiwa na timu yake mpya.

Hitimisho

Mpanzu bado yupo Simba SC kwa msimu wa 2025/26. Kuripoti kwake kambini kuanza maandalizi ya msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mchezaji huyo amekuwa ni mhimili kwa Simba SC katika eneo la kuipa uhai timu katika kushambulia na kutuliza timu inapokuwa haina mpira.

image
Share this: