- Jean Ahoua anaondoka Simba SC Feisal kurithi mikoba yake Msimbazi kwa msimu mpya wa 2025/26.
- Magoli yake na rekodi alizoandika 2024/25 Jean Ahoua zinatisha, alivunja rekodi zake mwenyewe.
- Ishu ya Feisal Salum mkali wa pasi za mwisho Bongo kuibukia Simba SC kuna kipengele.
Jean Ahoua anaondoka Simba SC kwenda kupata changamoto mpya ikielezwa kuwa Feisal Salum wa Azam FC huenda akarithi mikoba ikiwa mazungumzo yatafika hatua nzuri. Inaelezwa kuwa kuna ofa zaidi ya mbili mezani. Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na JS Kabylie ya nchini Algeria.
Kindege kinakupa mamilioni sasa hivi
Paisha Kindege cha SportPesa sasa hivi upate mamilioni. Ni rahisi sana na kuna mgao kila siku. Cheza Aviator sasa.

Sababu za Jean Ahoua kuwa kwenye rada

Soma hii:Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25
Miongoni mwa sababu kubwa zinazofanya Ahoua kuwa katika rada za timu mbalimbali ni uwezo wake katika kufunga magoli. Mbali na kufunga magoli Ahoua ni mzuri kwenye kutengeneza nafasi za magoli. Ikumbukwe kwamba ni kinara wa kufunga msimu wa 2024/25.
Ndani ya kikosi cha Simba SC, Ahoua alifunga magoli 16. Akiwa na magoli 16 Ahoua alitengeneza pasi 9 za magoli rekodi ambazo zinambeba. Ni mkali kwenye kufunga magoli ya kutengwa alifunga katika anga la kimataifa kwa pigo la faulo Uwanja wa New Amaan Complex dhidi ya Stellenbosch.
Mkataba wake na Simba SC

Soma hii: Pacome wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC vita yao waliimaliza kibabe
Nyota huyo alitambulishwa ndani ya ardhi ya Tanzania Julai 3 2024. Ni mkataba wa miaka miwili alisaini ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids. Kandarasi yake imesalia mwaka mmoja kumalizika.
Ahoua alitoka katika Klabu ya Stella Club d’Adjame. Alikuwa ni mchezaji wa nne kusajiliwa Simba SC. Ilianza na Lameck Lawi huyu masuala ya makubaliano na Coastal Union hajakwenda sawa akarejea kwenye timu yake. Joshua Mutale ambaye ni kiungo mshambuliaji na Steven Mukwala ambaye ni mshambuliaji hawa walianza kutambulishwa kabla ya Ahoua.
Avunja rekodi yake mwenyewe
Ahoua ndani ya Stella Club d’Adjame msimu wa 2023/24 rekodi zinaonyesha kuwa alifunga mabao 12. Mbali na kufunga mabao hayo 12 alitoa pasi 9 za mabao. Hivyo msimu mmoja alihusika kwenye jumla ya mabao 21.
Kutokana na mchango wake huo alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora 2023/24, (MVP). Rekodi hiyo kaivunja akiwa ardhi ya Tanzania kwa kuhusika kwenye mabao mengi. Ni mabao 16 alifunga na kutoa jumla ya pasi 9 za mabao. Hivyo msimu wa 2024/25 alihusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC.
Magoli yake 16 ndani ya ligi Ahoua

Soma hii: Simba SC yaipiga Pamba Jiji 5-1 Ligi Kuu Bara KMC Complex
Jean Ahoua ni kinara wa kucheka na nyavu ndani ya ligi ni kiungo mshambuliaji wa Simba SC Jean Ahoua. Nyota huyo kaufunga jumla ya mabao 16 ndani ya msimu wa 2024/25. Bao la 16 alifunga kwenye mchezo dhidi ya KenGold dakika ya 75.
Ahoua katengeneza jumla ya pasi 9 za magoli na kafunga magoli 16. Kahusika kwenye mabao 25 kati ya 69 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 78 baada ya mechi 30.
Katika magoli 16 ambayo kafunga, magoli 15 kafunga kwa mguu wa kulia. Goli moja alifunga kwa pigo la kichwa dhidi ya Pamba Jiji akitumia pasi ya Ellie Mpanzu. Magoli 6 alifunga kwa mikwaju ya penati.
Feisal atajwa kurithi mikoba

Soma hii: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?
Wakati Ahoua akitajwa kuwa anaondoka jina la Feisal Salum kiungo wa Azam FC linatajwa. Inaelezwa kuwa huenda mbeba mikoba ya kiungo huyo atakuwa Feisal. Taarifa zinaeleza kuwa kuna ugumu kumpata mchezaji huyo.
Simba SC ili wampate mchezaji huyo ni lazima wawe na bilioni 2. Jambo hilo linatajwa kuwa gumu kwa mabosi wa Simba SC. Ikumbukwe kwamba mchezaji huyo ana mkataba wa mwaka mmoja umesalia kuendelea kuwa mali ya Azam FC.
Ndani ya Ligi Kuu Bara ya NBC Feisal ni namba moja kwenye kutengeneza pasi za mwisho. Alitoa pasi 13 za magoli msimu wa 2024/25. Mbali na kutengeneza pasi hizo alifunga jumla ya magoli manne.
Magoli yake yote hayo alifunga kwa mguu wake wa kulia. Hivyo mguu wenye nguvu kwa Feisal ni ule wa kulia. Hiyo ni sawa na nyota wa Simba SC Jean Ahoua ambaye mguu wake wenye nguvu zaidi ni ule wa kulia.
Azam FC kuhusu Fei Toto
Thabit Zakaria, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Azam FC aliweka wazi Fei ni mali ya Azam FC. Zakaria alisema kuwa wanatambua kuna timu nyingi ambazo zinahitaji saini yake hilo linatokana na ubora. Aliongeza kuwa thamani ya mchezaji huyo ni kubwa ana anapaswa kuendelea kuwa hapo.
“Tupo kwenye maandalizi kwa msimu mpya. Tunawaambia mashabiki watulie kuna jambo kubwa linakuja. Taarifa za mpira huwa zinakuwa wazi na wajiandae kumshangilia Fei akiwa ndani ya Azam FC,”.
Hitimisho
Simba SC ipo sokoni kutafuta beki wa kushoto mara baada ya Mohamed Hussen Zimbwe Jr kuondoka. Ikiwa Ahoua ataondoka itakuwa na kazi nyingine kusaka kiungo mshambuliaji. Yote ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26.


