CECAFA ZawadiCECAFA Zawadi
  • Tanzania 2-1 Senegal CECAFA 2025 Arusha, meza ilipinduliwa kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
  • Mechi hizo ilikuwa ni maalumu kwa maandalizi ya CHAN 2024 na mchezo wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 2 2025.
  • FA atoa neno kuhusu ubingwa, Kocha Mkuu, Morocco abainisha walichokipata kwenye mashindano hayo dakika 180.

Tanzania 2-1 Senegal mchezo wa CECAFA 2025 ambao ulishirikisha timu tatu. Mchezo huo ulichezwa Julai 27 2025 Uwanja wa Black Rhino, Arusha. Haya ni maandalizi kuelekea CHAN 2024 na mchezo wa ufunguzi unatarajiwa kuchezwa Agosti 2 2025, Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo wa ufunguzi Tanzania itacheza na Burkina Faso.

Marubani mwanzo wa wiki wanaanza na mamilioni

Paisha ndege mwanzo wa wiki uvune mamilioni sasa. Rahisi sana wakati kindege kinapaa mkwanja unaingia wakutosha. Cheza Aviator upate mgao wako.

Aviator banner

Kwenye mchezo huo wa CECAFA mabao ya Tanzania yalifungwa na Sopu dakika ya 53 kwa mkwaju wa penati. Bao la ushindi lilifungwa na Ibrahim Bacca dakika ya 56. Ikumbukwe kwamba Tanzania ilianza kufungwa dakika ya 8 kupitia kwa Mapathe Mbdoji dakika ya 8.

Morocco Head Coach
Morocco, Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Soma hii: Simba SC yashtua na fumbo la jezi namba 6 ni Feisal au udhamini?

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Black Rhino kwenye msako wa pointi tatu muhimu. Tanzania ilikusanya jumla ya pointi sita katika mashindano hayo. Kwenye pointi sita zote zilibebwa kibindoni kwa kuwa mechi zote mbili ilishinda.

Kocha wa Tanzania, Hemed Morocco

“Tunamshukuru Mungu tumemaliza mechi salama. Kwa asilimia 80 nadhani tumekuwa imara ila kuna sehemu ambazo tunapaswa kuzifanyia kazi. Tuna siku nne za maandalizi kufanyia kazi mapungufu ambayo yametokea.

“Kuna sehemu ambazo tunapaswa kuzifanyia kazi ili kuwa bora. Bado kuna mambo ambayo hayajakaa vizuri katika baadhi ya maeneo. Tunaendelea kujipanga kuhakikisha kuwa tunashiriki mashindano. Kwenye mchezo wetu wa Agosti 2 tunaamini tutakuwa tuko vizuri,” alisema Morocco.

Msikie Dickson Job beki wa Tanzania

Job Stars (-)
Job Dickson akiwa kwenye majukumu ya Taifa.

Soma hii: Taifa Stars hiyo AFCON 2025, Mama awapa tano

Job ambaye ni beki alibainisha kuwa mashindano ya CECAFA yalikuwa na ushindani mkubwa. Mechi ambazo walicheza zimewapa nguvu kuelekea katika mashindano ya CHAN. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa.

“Tunaamini kwamba tunakwenda kupambana kwenye mechi zetu zijazo. Kwa kufanya vizuri kwenye mashindano yaliyoisha inatupa nguvu kuwa kwenye mwendelezo huo. Tunawaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika mchezo wetu wa kwanza, Agosti 2 Uwanja wa Mkapa,”.

Kete ya kwanza kwa Tanzania

Mchezo wa kwanza ulichezwa Julai 2 2025 ilikuwa Tanzania 1-0 Uganda. Bao la ushindi lilifungwa na Iddy Nado dakika ya 14 ya mchezo. Bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

CECAFA Cup ni maandalizi ya CHAN 2024

 CECAFA Cup yalikuwa ni mashindano maalumu kwa ajili ya kuwa tayari kuelekea katika michuano ya CHAN. Timu tatu zilishiriki mashindano hayo. Tanzania ilitupa kete yake kwenye mchezo wa kwanza Julai 22 dhidi ya Uganda.

Neno la Waziri wa Habari na Michezo

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma maarufu kwa jina la FA amebainisha kuwa timu ya Tanzania ipo vizuri. Hayo alisema mara baada ya Tanzania kupata ushindi dhidi ya Uganda. Mwinjuma amesema kwenye mpira wa miguu lolote linaweza kutokea.

“Timu ipo tayari sijaona timu nyingi zikishiriki.Ila kwa timu ambazo zimeshiriki Uganda na Senegal nit imu nzuri. Kwa sasa tuna nafasi kitwakimu kuchukua ubingwa huu.

“Kupata matokeo mbele ya Uganda, Senegal hapo unaona kwamba tumechukua CHAN ya huku Karatu. Bado CHAN 2024 ya Afrika nzima ambayo tunakwenda kushiriki. Tuna nafasi kubwa kuchukua kombe hili kuliko wakati wowote ule ila kwenye mpira lolote linaweza kutokea,”.

Timu zilishiriki mashindano hayo

Timu tatu zilishiriki mashindano hayo kwa ajili ya kuwa fiti kuelekea CHAN. Tanzania, Uganda na Senegal. Tanzania kwenye mechi zake zote mbili ilipata ushindi.

Ratiba ilikuwa namna hii

Tanzania vs Uganda, alasiri saa 9:00 ilikuwa siku ya Jumanne, Julai 22. Uganda vs Senegal ilikuwa Julai 24. Tanzania vs Senegal ilikuwa Julai 27 mechi zote zilichezwa saa 9:00 alasiri.

Kikosi cha Tanzania dhidi ya Uganda

Feisal vs Uganda
Feisal akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Soma hii: Feisal kucheza Simba SC Yanga SC au Azam FC Ligi Kuu NBC 2025/26? Ishu yake iko hivi

Yakoub Suleiman alianza langoni, Shomary Kapombe, Pascal Msindo, Dickson Job huyu alikuwa nahodha wa mchezo. Ibrahim Abdulla, maarufu kwa jina la Bacca.

Ahmed Pipino, Mudathir Yahya, Idd Nado. Feisal Salum, Nassoro Saadun, Abdul Suleiman maarufu kwa jina la Sopu hawa walianza kikosi cha kwanza. Mchezo wa kwanza Tanzania ilishinda.

Wachezaji wa akiba walikuwa Aishi Manula, Lusajo Mwaikenda, Wilson Nangu, Vedastus Masinde, Ellias Lawi, Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Shekhan Khamis, Ibrahim Ahmada, Jimmy Simba. Clement Mzize, Mishano Michael hawa walianzia benchi.

Kikosi cha Tanzania dhidi ya Senegal mashindano ya CECAFA

Hussen Masalanga, Shomary Kapombe, Mohamed Hussen Zimbwe Jr alikuwa nahodha wa mchezo. Dickson Job. Ibrahim Abdulla, maarufu kwa jina la Bacca.

Yusuph Kagoma, Mudathir Yahya, Idd Nado. Feisal Salum, Ibrahim Ahmada, Abdul Suleiman maarufu kwa jina la Sopu hawa walianza kikosi cha kwanza. Mchezo wa kwanza Tanzania ilishinda.

Wachezaji wa akiba walikuwa Aishi Manula, Yakoub Suleiman, Ahmed Pipino, Lusajo Mwaikenda, Wilson Nangu, Vedastus Masinde, Ellias Lawi, Pascal Msindo Shekhan Khamis, Jimmy Simba. Clement Mzize, Mishano Michael hawa walianzia benchi.

Hitimisho

Nchi tatu zitashirikiana katika kuandaa mashindano ya CHAN ambayo huwahusisha wachezaji wa ndani. Uganda, Kenya na Tanzania utakapocheza mchezo wa ufunguzi Agosti 2 2025 dhidi ya Burkina Faso. Uganda Uwanja wa Taifa zitachezwa mechi 12 kama itakavyokuwa kwa Uwanja wa Taifa wa Tanzania.

KenGold FC vs Simba SC 'live'
Share this: