Conte na Ali KamweConte na Kamwe
  • Maxi aungana na Pacome Yanga SC: Tetesi wanaofuata kutambulishwa hawa hapa mziki bado unashushwa.
  • Maxi ameongeza mikataba ya miaka miwili kusalia ndani ya Yanga, hivyo anatarajia kumaliza mkataba mwaka 2027.
  • Taarifa kutoka Yanga SC zimethibitisha kuwa Wananchi hawajamaliza mziki kuna mashine hizi zinasubiri utambulisho.

Baada ya kutangaza mastaa wapya watatu wa kigeni akiwemo Balla Conte na watatu wazawa. Uongozi wa Yanga SC umeendelea na ujenzi wa kikosi chao ambapo sasa wametangaza kumalizana na kiungo wao pendwa Maxi Nzengeli. Mastaa hao sasa wanaungana na Mudathir na Pacome ambao tayari waliongeza mikataba.

‘Kindege’ cha SportPesa kinakupa Mamilioni cheza sasa

Huku ukiendelea kuhabarika na makala hii, unasubiri nini? Shinda mamilioni sasa kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

image

Pacome, Maxi, Abuya mpaka 2027 wananchi watamba tabu ipo palepale

Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli

Viungo Maxi na Abuya wote wameongeza mikataba ya miaka miwili kuendelea kusalia ndani ya Yanga. Hivyo mastaa hao wanatarajia kumaliza rasmi mikataba yao mwaka 2027. Kufuatia taarifa hiyo mashabiki wa Yanga SC wameonekana kufurahia hatua hiyo huku wakiwatambia wapinzani kuwa tabu iko palepale.

SOMA HII PIA: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2025/26 | Vita yao na Simba SC balaa zito

Wengine walioongezewa mikataba Yanga mpaka sasa

Mpaka sasa Yanga SC tayari imefanikiwa kuwaongezea mikataba baadhi ya mastaa wao kadhaa. Miongoni mwa mastaa hao ni Pamoja na nahodha wao msaidizi, Dickson Job, Kiungo Denis Nkane na Mudathir Yahya. Imeelezwa kuwa Yanga wanaendelea kufanya maboresho ya mikataba ya mastaa wengine.

Ambao wanaofuata kutambulishwa hawa hapa

Taarifa kutoka ndani ya Yanga pia zimethibitisha kuwa uongozi wa timu hiyo tayari umemalizana na mastaa wengine kadhaa kama ifuatavyo;

Andy Bobwa Boyeli

Vyanzo mbalimbali kutoka kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, zimethibitisha kuwa wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli. Boyeli mwenye umri wa miaka 24, amesajiliwa kutoka Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo. Mkataba huo ni wa kipindi cha mwaka mmoja na una kipengele cha mchezaji huyo kununuliwa mazima kwa gharama ya dola 100,000.

Boyeli alikuwa na wakati mzuri msimu wa 2022/23 akiwa na kikosi cha Power Dynamos ya Zambia. Akiwa na timu hiyo Boyeli alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa ligi ya Zambia baada ya kufunga magoli 18. Mafanikio hayo yalimfanya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP).

Mohamed Hussein ‘Tshabalala’

Maxi aungana na Pacome Yanga SC
TETESI Tshabalala kutua Yanga

Yanga na Tshabalala wamemalizana na kilichobaki ni Yanga kumtangaza staa huyo. Hii ni baada ya kuwepo mazungumzo ya muda mrefu kutoka kwa pande zote mbili. Tshabalala amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza Yanga.

Kufuatia hatua hiyo, Tshabalala amewaaga rasmi Simba na familia nzima ya timu hiyo kwa barua yake rasmi. Barua hiyo aliiweka katika kurasa za mitandao yake ya kijamii. Kama Sehemu ya kuheshimu mchango wa familia hiyo katika maisha yake kwa kipindi cha miaka 11 aliyodumu na kikosini.

SOMA HII PIA: Baada ya ‘Tshabalala’ na Conte Yanga SC yashusha straika Boyeli: Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Kikosi kipya kusukwa chini ya kocha mpya Msauzi, Roman Folz

Romain Folz
Romain Folz

Kikosi hiko kipya cha Wananchi kinakuja kuanza kusukwa na aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundowns Roman Folz. Kocha huyo ni miongoni mwa wakufunzi wenye wasifu mkubwa na uzoefu na sola la Afrika. Hali hii inaonekana kutarajiwa kuwapa faida Yanga katika kuunda kikosi kuelekea msiomu ujao wa 2025/26.

SOMA HII ZAIDI: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Folz kuanza na Pre-Season nzito

Kocha huyo anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga, kupitia kambi ya maandalizi kabla ya msimu ‘Pre-season’. Kuhusu wapi kambi ya timu hiyo itakuwa kwa ajili ya pre-season, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa tayari wamepokea mialiko kadhaa. Kati ya mialiko hiyo Yanga wamethibitisha mmoja tu, watakapoenda Rwanda kuwavaa Rayon Sports.

Hitimisho

Yanga inaonekana kudhamiria kuendelea pale ilipoishia msimu uliopita na Kwenda mbali zaidi kwenye kukusanya makombe. Hii inaweza kuonekana katika namna ambavyo wamefanikiwa kuzuia mastaa wao muhimu kuondoka. Mpaka sasa ni Aziz Ki pekee ndio staa muhimu wa Yanga ambaye ameondoka.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.