Zimbwe JrZimbwe Jr

Mohamed Hussen Zimbwe Jr nahodha wa Simba SC amefuta utambulisho wake jambo lililowashtua mashabiki. Beki huyu chaguo mkataba wake umeisha baada ya msimu wa 2024/25 kutamatika. Kwenye ukurasa wake rasmi wa Instgram uliokuwa unamtambulisha kuwa ni mchezaji wa Simba SC kaliondoa jina hilo huku akitajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC.

Zimbwe Tuzo
Zimbwe na tuzo ya kuwa kwenye kikosi bora ndani ya 2023/24. Source: Simba SC.

Soma hii: Baada ya Conte Yanga SC yatua kwa Tshabalala wa Simba SC Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Vuna mamilioni leo hii

Vuna mamilioni leo hii kwa kucheza Aviator. Rahisi sana unachotakiwa kufanya kupaisha kindege. Wakati unapaa unavuna mkwanja wako na mgao ni kila siku.

SEO Banner LV

Zimbwe kwa msimu wa 2024 alikuwa ni chaguo la kwanza la Fadlu. Beki huyo tegemeo utambulisho wake uwanjani ni jezi namba 15. Hapa tunakuletea rekodi zake kwa msimu wa 2024/25 namna hii:-

Mechi mbili za Ngao ya Jamii

Ngao ya Jamii 2024/25. Mabingwa walikuwa ni Yanga SC waliopata ushindi mbele ya Azam FC. Simba SC mwanzo wa msimu ilipishana na taji la kwanza. Licha ya kushindwa kutwaa taji hilo Zimbwe alikuwa ni chaguo la kwanza kwenye mechi zote mbili.

Mabadiliko ya kusaka mshindi wa Ngao ya Jamii yalianza, timu nne za juu zilianzia hatua ya nusu fainali. Timu iliyomaliza nafasi ya kwanza ilicheza na ile iliyomaliza nafasi ya tatu, iliyomaliza nafasi ya pili ilicheza na iliyomaliza nafasi ya nne. Coastal Union ilikuwa nafasi ya nne na ya pili ilikuwa ni Azam FC.

Kariakoo Dabi ilipochezwa Agosti 8 2024 ikiwa ni hatua ya nusu fainali. Yanga SC 1-0 Simba SC ikiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii, Uwaja wa Mkapa Zimbwe alianza kikosi cha kwanza. Katika mchezo huu Simba SC ilipoteza. Ilikwenda kucheza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na Coastal Union.

Mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu ulichezwa Agosti 11 2024. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Coastal Union. Zimbwe alianza kikosi cha kwanza na Simba SC ilipata ushindi.

Ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC 2024/25

Zimbwe v Fountain Gate
Zimbwe kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate NBC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC 1-0 Kagera Sugar ni mchezo wa mwisho 2024/25

Simba SC imecheza jumla ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Zimbwe ni mechi 27 alipata nafasi yakucheza akikosekana kwenye mechi tatu pekee ambazo ni dakika 270.

Katika mechi hizo 27 ambazo alicheza alikomba dakika 1,817. Alihusika kwenye mabao manne kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC kwenye ligi. Ni pasi tatu za mabao alitoa huku akifunga bao moja katika mechi za ushindani.

Zimbwe na penati ndani ya uwanja

Simba SC msimu wa 2024/25 ni namba moja kwa timu iliyopata penati nyingi. Baada ya mechi 30 ni penati 13 ilipata. Katika penati hizo 12 zilijaa kwenye nyavu na moja iliokolewa na mlinda mlango.

Wapigaji wa penati kwa Simba SC ni wachezaji wawili. Leonel Ateba na Jean Ahoua. Ateba alipiga penati 7, alifunga penati sita na alikosa moja dhidi ya Namungo FC. Jean Ahoua alifunga penati 6 katika mapigo yake yeye hakukosa penalti.

Ni Zimbwe huyu alikuwa mchezaji wa kwanza kusababisha penalti ndani ya Simba SC. Ilikuwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Ilikuwa Septemba 29 2024.

Salmin Hoza dakika ya 60 alimchezea faulo Zimbwe ndani ya 18. Mwamuzi wa kati alikuwa ni Omary Mdoe aliamuru adhabu ya penati. Mpigaji wa kwanza alikuwa ni Jean Ahoua aliyefunga bao la ushindi kwenye mchezo huo.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Dodoma Jiji 0-1 Simba SC. Pointi tatu zilikuwa ni mali ya Simba SC. Hivyo penati ya Zimbwe ilikuwa ni sababu ya Dodoma Jiji kupoteza.

Mechi ambazo alikosekana

Zimbwe alikosekana kwenye mechi tatu za ligi. Ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex ilikuwa Novemba 6 2024. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 4-0 KMC FC. Mchezo wa pili ilikuwa Novemba 22 2024, Pamba Jiji FC 0-1 Simba SC.

Mchezo wa tatu ilikuwa Coastal Union 0-3 Simba SC, Machi Mosi 2025. Ni mechi moja Simba SC ilikuwa nyumbani na mechi mbili ugenini. Kwenye msako wa pointi tisa ambazo Zimbwe alikosekana zote zilipatikana kwa ushindi na mabao 8 Simba SC ilifunga.

Mohamed Hussen
Mohamed Hussen na Ateba kwenye anga la kimataifa 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC 1-1 RS Berkane ya Morocco yatwaa ubingwa wa CAF Mei 25 2025

Pasi zake za mabao na timu aliyoifunga

Alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo dhidi ya Tabora United, Uwanja wa KMC Complex. Ilikuwa Agosti 18 2024 alimpa Valentino Mashaka. Pasi ya pili alitoa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Desemba 21 2024, pasi ya tatu alitoa kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Machi 14 2025.

Bao pekee alilofunga ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Unioni. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex ilikuwa ni Oktoba 4 alipachika bao dakika ya 25 kwa mguu wa kulia. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Coastal Union.

Hitimisho

Simba SC ni timu namba mbili kufungwa mabao machache kwenye ligi. Zimbwe kashuhudia wakifungwa mabao 13. Katika anga la kimataifa Simba SC iligotea hatua nafasi ya pili, Kombe la Shirikisho Afrika ilifungwa mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane.

image
Share this: