- Tetesi usajili ligi Kuu NBC 2025/26 zinazidi kushtua watu kutokana na majina makubwa yanayotajwa sokoni.
- Listi ya mastaa wanaotajwa kupigwa panga na Yanga inazidi kuongezeka ambapo Mzambia, Clatous Chama naye inatajwa limempitia.
- Ukiachana na Panga la moto, Yanga pia imetajwa kuanza kushusha mashine mpya akiwemo straika Ecua.
Ukurasa wa msimu wa Ligi Kuu 2024/25 umemalizika na sasa habari kubwa kwenye vijiwe vya soka ni kuhusu tetesi za usajili Ligi Kuu NBC 2025/26, ambapo kila timu inapambana kufanya maboresho ya vikosi vyao kwa kusaini mastaa wapya, na kuachana na walioshindwa kutetea nafasi zao.
Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Wakati ukihabarika na makala hii, kumbuka unayo nafasi ya kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.
Huko Yanga Chama ‘Out’, straika mpya huyu hapa

Kuhusu mabingwa watetezi Yanga wanaendelea kuhusishwa na taarifa mbalimbali huku taarifa kubwa ya hivi karibuni ni kuhusiana na kuachana na kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chama na kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast, Celestin Ecua.
SOMA HII PIA: SportPesa yaipa Yanga SC Milioni 262.5: Makombe matano yatajwa
Ishu ya Chama
Licha ya kuondoka kwa Mburkinabe, Stephanie Aziz Ki aliyejiunga na Wydad Casablanca ya Morocco, Chama ameendelea kukosa nafasi ndani ya kikosi cha Yanga na taarifa za kuaminika ambazo zimetolewa na mchambuzi, Hans Raphael ni kuwa uongozi wa Yanga umefikia maamuzi ya kuachana na nyota huyo.
Ikumbukwe mapema kabla ya kufungwa kwa msimu Yanga ilimruhusu staa wake, Stephanie Aziz Ki kuondoka ambapo ameuzwa kwenye kikosi cha Wydad Casablanca ya Morocco. Aziz anatajwa kuuzwa Wydad kwa dau la dola za Marekani 350,000.
Wengine wanaoondoka Yanga Musonda, Ikangalombo na kocha Miloud

Ukiachana na ishu ya Chama, taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, timu hiyo imefikia makubaliano ya kuachana na mastaa wao wengine wa ushambuliaji ambao ni kiungo Mkongomani, Jonathan Ikangalombo na straika Mzambia Kennedy Musonda.
Musonda na Yanga wameachana Rasmi. Mkataba wa Musonda mwenye umri wa miaka 30 na Yanga umeisha na mchezaji huyo ameondoka jangwani kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.
Musonda atakumbukwa na wananchi kwa mchango wake mkubwa, ikiwemo bao moja alilofunga katika ushindi wa kihistoria wa mabao 5-1 dhidi ya Simba msimu uliopita wa 2023/24. Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamina Mkapa Dar es Salaam.
SOMA HII PIA: Tetesi usajili ligi Kuu ya NBC 2025/26 wanaoondoka Yanga hawa hapa
Kuhusu Ikangalombo
Jonathan Ikangalombo Kapela ameondoka Yanga baada ya kudumu jangwani kwa miezi sita tu, sababu kubwa ikiwa ni winga huyo kupafomu chini ya kiwango alichotarajiwa na mabosi zake kuonyesha, hivyo mabosi wa Yanga wameamua kumpa mkono wa kwa heri.
Kocha Yanga naye safari inamhusu, atimkia Misri
Licha ya kuiongoza Yanga katika mafanikio makubwa msimu huu akiipokea timu katikati ya msimu, inaelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha wao, Miloud Hamdi anayetajwa kutimkia Misri na wako kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya.
Akiwa na kikosi hiko Miloud ameiongoza timu hiyo kushinda mataji matatu ambayo ni Ligi Kuu Bara, maarufu Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Kombe la Muungano.
Mshine mpya za Yanga hizi hapa
Ukiachana na Panga la moto ambalo linaendelea ndani ya kikosi cha Yanga, timu hiyo pia imetajwa kuanza kujiimarisha kwa kushusha mashine mpya kwa ajili ya msimu ujao. Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kwa karibu ni staa wa Ivory Coast, Mohamed Doumbia na Celestin Ecua.
Doumbia tayari yuko Tanzania na alionekana akifuatilia mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Dodoma ambayo ilifanyika visiwani Zanzibar. Ukiachana na Doumbia, macho ya uongozi wa Yanga pia yanafuatilia kwa karibu nyota, Célestin Ecua ambaye msimu uliopita Ecua alifunga goli 15 na assists 12.
Hawa hapa wameongeza mikataba mipya Yanga

Mlinzi wa kati wa Yanga na nahodha msaidizi wa kikosi hiko Dickison Job, ameongeza mkataba wa miaka miwili kubaki Yanga. Inaelezwa Job amegomea ofa kutoka kwa vilabu vingine ili kubaki jangwani na tayari ameongeza miaka miwili. Kıla kitu kimekamilika na mkataba umesainiwa.
Pacome, Maxi kimeeleweka Yanga, kwa mujibu wa mchambuzi, Hans Raphael amesema tayari Yanga wamemalizana na viungo, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli kwenye mchakato wa kusaini mikataba mipya kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.
SOMA HII PIA: Timu tano zilikuwa na maajabu ya sabasaba | Yanga SC na Simba SC zatuma ujumbe maalumu
Hitimisho
Kipindi cha usajili ni miongoni mwa ratiba muhimu kwa maendeleo ya timu, hivyo ni vyema kila timu ikajipanga vizuri kuhakikisha inaboresha kikosi chake na kukifanya kuwa madhubuti kuelekea msimu mpya wa 2025/26, ambao unatabiriwa kuwa na ushindani mkubwa kulinganisha na msimu huu.

