Makombe ya ubingwa YangaMakombe ya ubingwa Yanga
  • Kabla ya Ikulu, makombe 5 ya Yanga yatua mjengoni SportPesa kama sehemu ya shukrani kwa mdhamini Mkuu.
  • Yanga wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu yanayokaribia kufikia miaka 8 na Kampuni ya SportPesa.
  • Mkataba wa udhamini wa SportPesa umefanya Yanga kuvuna zaidi ya Bilioni 17.
  • Hii imefanya timu hiyo kuwa na jeuri ya kununua mastaa wakubwa kama Aziz Ki na Pacome.

Huku uongozi wa Yanga ukiweka wazimpango wao wa kupeleka makombe yao ya ubingwa mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu, sasa kabla ya Ikulu makombe 5 ya Yanga yatua mjengoni SportPesa kama sehemu ya kushukuru SportPesa ambao ni mdhamini Mkuu wa klabu hiyo.

Aviator banner

Kwanini makombe ya Yanga mjengoni SportPesa?

Mkataba Yanga SC na SportPesa
Mkataba Yanga SC na SportPesa

Uongozi wa Yanga wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu yanayokaribia kufikia miaka 8 na Kampuni ya SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Yanga. Miaka hiyo 8 inagawanyika katika vipindi viwili. Mkataba wa kwanza wa SportPesa na Yanga ulikuwa wa miaka mitano ambao ulimalizika mwaka 2022 ukiwa na thamani ya Bilioni 5.2

Mwaka 2022 SporPesa na Yanga ziliingia mkataba mwingine wa miaka mitatu wenye thamani ya Bilioni 12.33, ambapo kwenye kila msimu Yanga wamekuwa wakivuna kiasi cha Shilingi Bilioni 4 ambazo zimekuwa zikitumika kwa maendeleo ya timu hiyo.

SOMA HII PIA: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga

Shinda mamilioni na Kindege cha SporPesa

Ukienda kuburudika na kuhabarika kwa makala kali za SportPesa, unaweza kujishindia mamilioni kwa kucheza mchezo wa kindege ‘Aviator’ ya Kampuni ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

SportPesa yaongeza jeuri ya kuwasajili Pacome, Aziz Ki Yanga

Kutokana na mzigo huo mzito wa Pesa ambao Yanga wamekuwa wakiuvuta kutoka SportPesa, Wananchi wamekuwa na jeuri ya kushusha wachezaji bora kama Aziz Ki na Zouzoua Pacome, ambao wameifanya timu hiyo kutawala soka la Tanzania kwa misimu minne mfululizo.

Yanga wawashukuru wadhamini wao

Kabla ya Ikulu Makombe 5 ya Yanga yatua mjengoni SportPesa@tzsportpesa
Shukrani kwa mdhamini wetu mkuu @tzsportpesa

Mara baada ya mechi ya ushindi ya Yanga SC 2-0 Simba SC na wananchi kutangaza ubingwa wao wanne mfululizo wa Ligi Kuu Bara, Uongozi wa Yanga umezishukuru taasisi mbalimbali zilizochangia mafanikio hayo, huku jina la SportPesa likitajwa kwa herufi kubwa kutokana mchango mkubwa wa kifedha walioipa Yanga.

SOMA HII HAPA: Injinia Hersi anaondoka au bado yupo Yanga? Mwenyewe afunguka mazito ishu ya siasa

Ali Kamwe atoa tamko zito

Akizungumzia mpango huo, Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema: “Shukrani za kipekee ni kwa wachezaji wetu ambao walimwaga jasho na damu, benchi la ufundi wamejitoa kwa namna ya kipekee. Tunawapongeza pia wapinzani wetu wote 14 kwa kutupa ushindani wa kutosha.

“Tuna furaha kubwa sana msimu huu. Mtakumbuka pale uwanja wa KMC, Msemaji wa ‘Aviola’ alitangaza kuwa wao wanacheza mechi za Yanga. Ile kauli ilituamsha sana, wananchi Niwaambie ukweli, kauli ile ndiyo iliyokuwa kifo chao.

“Kubeba ubingwa ni jambo zuri, lakini aviola kutoka kapa ni furaha kubwa zaidi. Msimu huu tumepitia mengi sana kama Klabu. Lakini siri yetu ya mafanikio, Licha ya mawimbi makubwa ni umoja na mshikamano umetusaidia.

“Viongozi ambao tuliwaamini watusaidie kwenye nyakati ngumu wamefanikisha hilo na tumevuka salama. Bila kusahau mchango wa Viongozi wote wa Matawi, Mashabiki na Wanachama tunasema Asante sana.

“Kijana yoyote anayemaliza kidato cha nne mwaka huu basi atakuwa amepata fursa ya kushuhudia klabu ya Yanga ikishinda mataji manne mfululizo, tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia ushindi huu mkubwa.

Kuhusu kumshukuru Rais Samia

Viongozi wa Yanga na Rais Samia
Viongozi wa Yanga na Rais Samia

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia kwa uongozi wake thabiti kwa taifa letu. Usalama na amani umesaidia sisi kucheza mpira katika mazingira rafiki, Ubingwa huu ni zawadi kwa Mheshimiwa Rais. Tunalenga kupeleka ubingwa huu ikulu kuonesha kuwa tumeridhishwa sana na uongozi wake.”

SOMA HII PIA: Tetesi usajili ligi Kuu ya NBC 2025/26 wanaoondoka Yanga hawa hapa

Kuhusu Parade la ubingwa

Mara baada ya kuwa na msimu wa mafanikio, wakifanikiwa kushinda mataji matano kwa msimu wa 2024/25, uongozi wa Yanga Jumatatu iliyopita uliandaa msafara wa kusherehekea mafanikio hayo, msafara ambao ulikuwa gumzo jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Yanga SC walijitokeza kutoka kila kona kuungana na msafara huo na funga kazi ilikuwa makao makuu ya Yanga SC, Jangwani Dar, ambapo Viongozi na wachezaji walionekana kuwa kwenye furaha ya juu wakikamilisha msimu wakiwa na mataji matano kabatini.

Msafara waanzia Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa JK Nyerere

Pared
Pared

Mara baada ya kutoka Zanzibar, Yanga walirejea Dar, Juni 30 2025 na kufanya Parade la Kihistoria ambalo lilianzia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuanzia saa 4:00 asubuhi na kufikia tamati majira ya saa tatu usiku kwenye viunga vya Jangwani.

Vituo ambavyo Parade la Kihistoria la Yanga SC iliyotwaa makombe matano msimu wa 2024/25 ilikuwa ni AirPort Terminal 1, Tazara, Keko, Karume, Msimbazi kwa watani zao wa jadi Simba SC na Jangwani.

Jangwani kulikuwa na shughuli ya burudani miongoni mwa wasanii waliowapa burudani Wananchi ni Mbosso Khan anayetamba na wimbo wake wa Aviola na alitambulishwa kuwa Mwananchi rasmi. Mbosso aliwashukuru Yanga SC na mashabiki kwa kumpokea. Aliwapa burudani Wananchi waliojitokeza kwa wingi.

Hitimisho

Hatimaye msimu wa Ligi Kuu Bara umefikia tamati kwa Yanga kushinda ubingwa, huku Wananchi wakiishukuru SportPesa mdhamini kuu namfadhili wao, Ghalib Said Mohammed (GSM), na kujipanga kumzawadia ubingwa Rais Samia.

Aviator banner
SEO Banner LV
Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.