- Huyu ndiye Andre Silva ndugu wa Diogo Jota aliyefariki kwenye ajali katika tukio la kushtua Alhamisi usiku.
- André Silva alikuwa kiungo mshambuliaji wa Penafiel, akiichezea tangu 2023, na alikuwa mchezaji muhimu.
- Kufuatia msiba huo nadhoda wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameshindwa kujizuia akiandika maneno mazito.
Habari kubwa kwenye tasnia ya michezo ni Tanzia juu ya kifo cha mastaa wawili wa timu ya Taifa ya Ureno, Diogo Jota na mdogo wake Andre Silva. Wawili hao wamefariki kwa ajali ya gari nchini Uhispania usiku wa kuamkia jana Alhamisi. Wengi wanamfahamu Diogo staa wa Liverpool lakini ni wachache wanamfahamu Andre na Makala hii inamuelezea Andre.
Shinda mamilioni na ‘kindege’ cha SportPesa kwa kubonyeza link iliyo kwenye picha hapa

Kilichotokea usiku wa Alhamisi

Kwa mujibu wa baraza la manispaa ya Zamora, nchini Uhispania huduma za dharura zilipigiwa simu mara baada ya saa moja asubuhi eneo la A52, karibu Palacios de Sanabria. Zimeelezwa kuwa wazima moto walifika eneo ya ajali na kufanikiwa kuzima moto.
Taarifa zikatolewa kuwa, Diogo Jota na ndugu yake, André Filipe Teixeira da Silva, wameaga dunia kufuatia ajali ya gari nchini Hispania. Waliokuwa safarini kupitia eneo la Zamora (Sanabria) usiku wa mapema wa Alhamisi.
SOMA HII HAPA: Diogo Jota afariki kwa ajali akiwa na miaka 28/ Liverpool yatoa taarifa/ Ameacha mke na watoto
Chanzo cha ajali
Ripoti za mashuhuda na watu wa karibu na sehemu ilipotokea ajali hiyo zinasema ajali ilitokea kutokana na tairi kupasuka. Taarifa ya Maafisa wa Guardia Civil walisema: “Taarifa tulizozipata hadi sasa ni kwamba gari, ambalo lilikuwa Lamborghini, lilipata ajali ya barabarani na kutoka kwenye njia.
“Hii ilitokana na tairi kupasuka wakati linapita gari lingine. Tukio hilo lilitokea mapema saa 12:30 usiku wa kuamkia Alhamisi, katika manispaa ya Cernadilla mkoani Zamora. Gari lilizimwa na moto na ndugu hao wawili waliokuwepo wameaga dunia.”
André Silva ni nani? Huyu ndiye Andre Silva ndugu wa Diogo Jota
André Filipe Teixeira da Silva alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu akiwa kiungo wa kushambulia katika klabu ya Penafiel, inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Ureno. Hapo awali, alipitia mafunzo katika klabu ya Gondomar SC, kisha akajiunga na academi ya Porto.
Alipitia pia katika vikosi vya tiu za vijana za Paços de Ferreira, Famalicão, na Boavista kabla ya kurejea Gondomar. Mwishowe, alijiunga na Penafiel mwaka 2023, na akawa mchezaji wa kawaida akiwa amecheza mechi 62 zote (kombe na ligi), akifunga mabao 7 na kutoa pasi 8 za goli.
Umuhimu wa uhusiano kati ya ndugu hao

Ndugu hao wawili walikuwa karibu sana, walikuwa wakisafiri pamoja likizo, wakifanya mazoezi msimu wa mapumziko, na kusherehekea mafanikio binafsi. Mwezi uliopita, André alihudhuria harusi ya Diogo Sanabria. Diogo nyota wat imu ya taifa ya Ureno alifunga ndoa na Rute Cardoso Juni 22, mwaka huu na Familia hiyo ilikuwa na watoto watatu.
SOMA HII PIA: Newcastle United 1, Liverpool 2: The Merseyside Magic Continues
Watu wamchanganya Andre Silva wa RB Leipzig
Kufuatia kifo hicho baadhi ya watu wameshindwa kuwatofautisha Andre Silva mdogo wa Diogo Jota aliyefariki kwenye ajali na staa wa RB Leipzig (André Silva mwingine), huku baadhi yao wakituma salamu za rambirambi kwa nyota huyo.
Salamu za rambirambi
Kama sehemu ya uwasilishaji wa salamu za rambirambi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ureno, Pedro Proença, alisema: “Shirikisho la Mpira wa Miguu Ureno na mpira wa miguu mzima wa Ureno wanaomboleza vikali kifo cha Diogo Jota na André Silva, leo asubuhi, Hispania.
“Diogo Jota ana takribani mechi 50 alizotumikia timu ya taifa, alikuwa mtu mzuri sana, mchezaji aliyeheshimiwa na wenzake n ahata wapinzani wake, mwenye furaha ya kuambukiza na hakika alikuwa kielelezo ndani ya jamii.”
Ujumbe kutoka klabu ya Liverpool
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Liverpool FC walitoa taarifa iliyoeleza: “Tumehuzunika sana na kifo cha mshtuko cha Diogo Jota, 28, na ndugu yake André, baada ya ajali ya barabarani nchini Hispania. Tunaomba faragha kwa familia yao, marafiki, wachezaji wenza na wafanyakazi wa klabu husika.”
FC Porto yawalilia
FC Porto pia ilituma rambi rambi kupitia X (zamani Twitter): “FC Porto iko katika majonzi makubwa. Tunatuma rambi rambi zetu za dhati kwa familia na marafiki wa Diogo Jota na ndugu yake André Silva, ambaye pia alikuwa mmoja wa wachezaji wetu wa academy. Mapumziko mema.”
Paços de Ferreira ilisema: “Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Diogo Jota na André Silva. Wote wachezaji wa Mata Real, wakitupatia heshima. Wote walidhihirisha unyenyekevu, uwajibikaji na kujitolea sana kwa vilabu walivyochezea.”
Cristiano shindwa kuamini, aandika ujumbe mzito

Kufuatia msiba huo nadhoda wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameshindwa kujizuia akiandika maneno mazito kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram akionyesha kutoamini kilichotokea.
“Haiingii akilini, ni hivi punde tu tulikuwa pamoja kwenye Timu ya Taifa, hivi punde tu umeoa. Kwa familia yako, kwa mkeo na watoto wako, natuma rambirambi zangu na kuwaombea nguvu zote za dunia. Najua utakuwa nao daima. Pumzikeni kwa amani, Diogo na André. Tutawakumbuka daima.”
Hitimisho
Kifo cha Jota na Andre ni pigo kubwa kwa tasnia ya michezo hususani mpira wa miguu, hii ndiyo sababu salamu za Rambirambi zimeendelea kumiminika kutoka pande zote duniani, ambapo jamii ya michezo imeonyesha mshikamano wa pamoja kwa ajili ya kuifariji Familia yake wakiwemo Wazazi wao, mjane Rute, watoto wao watatu na familia ya soka.


