- Yanga SC waifunika Dar kwa Paredi la Ubingwa la Kihistoria 2024/25, SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Yanga SC watajwa.
- Yafunga 2024/25 na mataji matano kwenye kabati, msafara wao ulikuwa ni balaa mashabiki wengi kila kona.
- Wakomba milioni 100 kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussen Ali Mwinyi.
Yanga SC waifunika Dar kwa Paredi la Ubingwa la Kihistoria lililofanyika Juni 30 2025. Mashabiki wa Yanga SC walijitokeza kutoka kila kona kuungana na msafara huo na funga kazi ilikuwa makao makuu ya Yanga SC, Jangwani Dar. Viongozi na wachezaji walikuwa kwenye furaha ya juu wakikamilisha msimu wakiwa na mataji matano kabatini.
Umilionea unakuita sasa kwa kupaisha kindege
Paisha kindege sasa uvune mamilioni. Muda wa kuwa milionea ni sasa kwa kuwa kuna mgao kila siku. Cheza sasa ushinde.


Safari ya Zanzibar na mataji kwa Yanga SC
Juni 29 2025, Yanga SC ilitwaa taji la CRDB Federation Cup kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex. Taji hilo lilikuwa ni la tano kwa msimu wa 2024/25. Ikumbukwe kuwa walitoka kucheza Kariakoo Dabi dhidi ya Simba SC na kupata ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Mkapa, Juni 25 2025.

Soma hii: Jean Ahoua kubeba tuzo kiatu cha ufungaji bora 2024/25
Walirejea Dar, Juni 30 2025 na kufanya Parade la Kihistoria ambalo lilianzia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kuanzia saa 4:00 asubuhi liligota mwisho saa majira ya saa tatu usiku. Vituo ambavyo Parade la Kihistoria la Yanga SC iliyotwaa makombe matano msimu wa 2024/25 ilikuwa ni AirPort Terminal 1, Tazara, Keko, Karume, Msimbazi kwa watani zao wa jadi Simba SC na Jangwani.
Jangwani kulikuwa na shughuli ya burudani miongoni mwa wasanii waliowapa burudani Wananchi ni Mbosso Khan anayetamba na wimbo wake wa Aviola na alitambulishwa kuwa Mwananchi rasmi. Mbosso aliwashukuru Yanga SC na mashabiki kwa kumpokea. Aliwapa burudani Wananchi waliojitokeza kwa wingi.
Huyu hapa Rais wa Yanga SC aitaja SportPesa

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC asilimia ndogo kubaki
Rais wa Yanga SC, Hersi Said ameweka wazi kuwa mafanikio ambayo wanayapata yanatokana na ushirikiano mkubwa kwa kila mmoja. Injinia aliwataja wachezaji na benchi la ufundi. Mbali na mashabiki ambao wamekuwa ni mstari wa mbele aliwataja na wadhamini wakuu wa Yanga SC amba oni SportPesa.
“Mashabiki wamekuwa nasi bega kwa bega ni muhimu kuwashukuru. Benchi la ufundi likiongozwa na Miloud Hamdi. Wadhamini wetu SportPesa wamekuwa na mchango mkubwa kwetu kufika hapa hakika tunatambua umuhimu wao.”
Fainali ya Zanzibar dhidi ya Singida Black Stars
Katika mchezo wa funga kazi msimu wa 2024/25, Yanga SC ilicheza Zanzibar. Huo ulikuwa ni mchezo wa fainali CRDB Federation Cup dhidi ya Singida Black Stars. Yanga SC 2-0 Singida Black Stars baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Singida Black Stars fainali ya kibabe
Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Duke Abuya dakika ya 39. Abuya alitumia mpira uliotemwa na kipa baada ya Israele Mwenda kufanya jaribio akiwa ndani ya 18. Kiungo huyo rai awa Kenya alipachika bao hilo kwa pigo la mguu wa kushoto.
Bao la pili lilipachikwa na Clement Mzize. Ilikuwa ni dakika ya 49 ya mchezo mshambuliaji huyo mzawa alipachika bao hilo. Ni pasi ya Maxi Nzengeli aliitumia kuwanyanyua mashabiki wa Yanga SC.
Mataji matano ya Yanga SC Ikulu ya Zanzibar

Soma hii: Yanga SC kupeleka kombe la ubingwa wa ligi ya NBC Ikulu – SportPesa Tanzania
Mataji matano ambayo Yanga SC imeyatwaa msimu wa 2024/25 yamefika Ikulu ya Zanzibar. Wakiwa Ikulu ya Zanzibar Yanga SC walipewa zawadi ikiwa ni sehemu ya kutambua mafanikio ambayo wamefikia. Ipo wazi kwamba Yanga SC imefunga msimu kwa mafanikio katika upande wa mataji.
Rais wa Klabu ya Yanga SC, Iniinia Hersi Said alimkabidhi makombe matano Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali Mwinyi. Hayo yote yalifanyika katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Zanzibar Juni 30 na walipotoka huko Yanga SC walifanya paredi la Kihistoria Dar.
Mataji hayo matano ambayo Yanga SC imetwaa ni Kombe Toyota Cup hili walichukua nchini Afrika Kusini, Ngao ya Jamii, Muungano Cup, Ligi Kuu Bara ya NBC na CRDB Federation Cup. Ligi ni pointi 82 wanazo wakiwa nafasi ya kwanza.CRDB Federation Cup fainali walishinda dhidi ya Singida Black Stars.
Taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi , Mawasiliano, Ikulu Zanzibar, Ragey Mohamed Juni 30 2025 ilieleza kuwa Rais Mwinyi aliwapa Yanga SC zawadi ya shilingi milioni 100 kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa ambayo wamepata Yanga SC, 2024/25.
Rais Mwinyi ameishukuru Yanga SC kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya Tanzania kupitia kampeni ya Visit Zanzibar na ameeleza kuwa klabu hiyo kuchagua baadhi ya mechi kucheza Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na Wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.
Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi alimkabidhi Rais Mwinyi medali maalumu ya michuano ya CRDB pamoja na jezi ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, (NBC Premier League). Kikosi cha Yanga SC mbali na mchezo dhidi ya Singida Black Stars kucheza Zanzibar mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji walicheza huko. Ni ushindi wa mabao 5-0 walipata Yanga SC katika mzunguko wa pili.


