- Tetesi usajili ligi Kuu ya NBC 2025/26 ni habari na bidhaa ya moto sokoni kwa sasa.
- Hii ni baada ya Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/25 kumalizika rasmi, huku Yanga wakiibuka mabingwa.
- Listi ya mastaa wanaotajwa kupigwa panga na Yanga ni pamoja na Kennedy Musonda na Jonathan Ikangalombo.
Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa 2024/25 imemalizika rasmi na sasa habari kubwa kwenye vijiwe vya soka ni kuhusu tetesi za usajili, ambapo kila timu inatambia mastaa wapya wanaotaka kuwasajili na wale wanaopigwa panga, kuhusu mabingwa watetezi Yanga, tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26 wanaoondoka Yanga wameanza kutajwa.

Kuhusu tetesi za usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26, Aziz Ki afungua milango wanaoondoka

Ikumbukwe mapema kabla ya kufungwa kwa msimu Yanga ilimruhusu staa wake, Stephanie Aziz Ki kuondoka ambapo ameuzwa kwenye kikosi cha Wydad Casablanca ya Morocco. Aziz anatajwa kuuzwa Wydad kwa dau la dola za Marekani 350,000.
SOMA HII PIA: Yanga SC kupeleka kombe la ubingwa wa ligi ya NBC Ikulu
Musonda, Ikangalombo wapitiwa na panga

Mara baada ya Aziz Ki taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, timu hiyo imefikia makubaliano ya kuachana na mastaa wao wawili kiungo Mkongomani, Jonathan Ikangalombo na straika Mzambia Kennedy Musonda.
Jonathan Ikangalombo Kapela ameondoka Yanga baada ya kudumu jangwani kwa miezi sita tu, sababu kubwa ikiwa ni winga huyo kupafomu chini ya kiwango alichotarajiwa na mabosi zake kuonyesha, hivyo mabosi wa Yanga wameamua kumpa mkono wa kwa heri.
Kuhusu Musonda na Yanga wameachana Rasmi. Mkataba wa Musonda mwenye umri wa miaka 30 na Yanga umeisha na mchezaji huyo ameondoka jangwani kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine
Musonda atakumbukwa na wananchi kwa mchango wake mkubwa, ikiwemo bao moja alilofunga katika ushindi wa kihistoria wa mabao 5-1 dhidi ya Simba msimu uliopita wa 2023/24. Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamina Mkapa Dar es Salaam.
Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Wakati ukiburudika na makala hii, unayo nafasi ya kufurahi zaidi kwa kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.
Kocha Yanga pia anaondoka
Licha ya kuiongoza Yanga katika mafanikio makubwa msimu huu akiipokea timu katikati ya msimu, inaelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha wao, Miloud Hamdi na wako kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya.
Akiwa na kikosi hiko Miloud ameiongoza timu hiyo kushinda mataji matatu ambayo ni Ligi Kuu Bara, maarufu Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Kombe la Muungano.
Mshine mpya za Yanga hizi hapa
Ukiachana na Panga hilo ambalo linaendelea ndani ya kikosi cha Yanga, timu hiyo pia imetajwa kuanza kujiimarisha kwa kushusha mashine mpya kwa ajili ya msimu ujao. Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kwa karibu ni staa wa Ivory Coast, Mohamed Doumbia na Celestin Acua.
Doumbia tayari yuko Tanzania na alionekana akifuatilia mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Dodoma ambayo ilifanyika visiwani Zanzibar. Ukiachana na Doumbia, macho ya uongozi wa Yanga pia yanafuatilia kwa karibu nyota, Célestin Ecua.
Hawa hapa wameongeza mikataba mipya Yanga

Mlinzi wa kati wa Yanga na nahodha msaidizi wa kikosi hiko Dickison Job, ameongeza mkataba wa miaka miwili kubaki Yanga. Inaelezwa Job amegomea ofa kutoka kwa vilabu vingine ili kubaki jangwani na tayari ameongeza miaka miwili. Kıla kitu kimekamilika na mkataba umesainiwa.
Pacome, Maxi kimeeleweka Yanga, kwa mujibu wa mchambuzi, Hans Raphael amesema tayari Yanga wamemalizana na viungo, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli kwenye mchakato wa kusaini mikataba mipya kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.
SOMA HII PIA: Pacome wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC vita yao waliimaliza kibabe/ MVP kazi ipo
Ishu ya Aucho
Kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho taarifa kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, mpaka sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Yanga na Aucho. Ikumbukwe mkataba wa Yanga na Aucho unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Ishu ya Diakite kama mrithi sahihi wa Aucho

Kufuatia uwezekano wa kuachana na Aucho, mchambuzi Hans ameendelea kusema Yanga wanaiwinda saini ya kiungo wa ulinzi wa Djoliba AC, Daba Diakite raia wa Mali ambaye ni bidhaa ya moto kwa sasa Africa na Yanga wanamuona ni mrithi sahihi wa Khalid Aucho.
Kiungo huyo amebakiza mkataba wa mwezi mmoja na Djoliba, hivyo mwezi ujao huenda akaondoka kama mchezaji huru. Inaelezwa msimu uliopita Manchester Utd walituma scout wao kumtazama Diakite, Benfica Lisbon nao walifanya hivyo na huku Africa Kaizer Chiefs na De Tunis wanamtaka kiungo huyo.
Diakite anawataka Yanga kuweka kipengele cha kumuuza mara moja endapo atapata ofa nzuri ya Ulaya. Wakala wa Diakite anajuana sana na viongozi wa Yanga na kwa miaka ya hivi karibuni Yanga walisajili wachezaji wake wanne tofauti.
SOMA HII PIA: Yanga SC waifunika Dar kwa Paredi la Ubingwa la Kihistoria 2024/25/ Watinga Ikulu/ SportPesa yatajwa
Hitimisho
Kipindi cha usajili ni miongoni mwa ratiba muhimu kwa maendeleo ya timu, hivyo ni vyema kila timu ikajipanga vizuri kuhakikisha inaboresha kikosi chake na kukifanya kuwa madhubuti kuelekea msimu mpya wa 2025/26,ambao unatabiriwa kuwa na ushindani mkubwa kulinganisha na msimu huu.


