Fabrince Ngoma (-)Fabrince Ngoma (-)
  • Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 kupitisha panga kwa wachezaji, wapya wengine kusajiliwa ndani ya timu.
  • Kupoteza Kariakoo Dabi mara tano Yanga SC vs Simba SC, tamko latolewa, Ahmed Ally atoa kauli ya kishujaa.
  • Fabrince Ngoma, Joshua Mutale, Aishi Manula kwenye orodha ya watakaokuwa nje ya Simba SC msimu ujao wa NBC Premier League.

Simba SC kuelekea msimu wa 2025/26 kupitisha panga kwa wachezaji ili kuleta wengine wapya. Taarifa zinaeleza kuwa kwa sasa wachezaji sita huenda wakaondoka ndani ya kikosi hicho cha Simba SC. Miongoni mwa wachezaji hao ni Aishi Manula ambaye mkataba wake wa miaka mitatu unafika kikomo, Fabrince Ngoma, Joshua Mutale, Hussen Kazi.

Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi

SEO Banner LV

Ni rahisi sana ujue kuvuna mamilioni. Paisha kindege sasa uvune mamilioni. Kila siku kuna mgao zamu yako ni leo, sasa hivi.

Air Manula (-)
Air Manula kipa namba tatu wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga – SportPesa Tanzania

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids mara baada ya kumalizika mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga SC aliweka wazi kuhusu maboresho ya timu. Kocha huyo alibainisha kuwa ni muhimu kupata wachezaji wenye uzoefu na bora kupambania malengo ya timu hiyo. Ikumbukwe kwamba matokeo kwenye mchezo Juni 25 2025 ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC.

Hizi hapa rekodi za Fadlu

Rekodi zinaonyesha kuwa Fadlu Davids baada ya kuongoza mechi 30 ni ushindi kwenye mechi 25. Simba SC iliambulia sare mechi 3 na ilipoteza mechi 2. Mechi hizo mbili ni Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC.

Fadlu
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC asilimia ndogo kubaki

Kwenye mzunguko wa kwanza ilikuwa Simba SC 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili, Yanga SC 2-0 Simba SC. Ni mabao matatu Simba SC imefungwa huku Yanga SC ikiwa haijafungwa. Dakika 180 kwa Simba SC mlinda mlango alikuwa Moussa Camara.

“Tulikuwa na msimu wenye ushindani mkubwa na kwa kiasi chake tumefikia malengo. Licha ya kutokufurahia yale ambayo yametokea. Kushindana na Yanga SC tukiwa na wachezaji ambao bado wanazidi kuimarika inatupa nguvu kujipanga zaidi kwa wakati ujao.

“Tutazungumza na uongozi kuona namna yakufanya maboresho katika kikosi. Ninawapongeza mashabiki kutokana na kuwa nasi kwenye kila hatua. Kila mmoja ninamshukuru,” alisema Fadlu kupitia Azam Tv.

Hawa hapa mabingwa wa ligi 2024/25

Mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25 ni Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi. Pointi zao kibindoni ni 82 ambazo wamekusanya. Safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 83.

 Simba SC nafasi ya pili pointi 78 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 69. Ukuta wa Simba SC umeruhusu mabao 13 na ule wa Yanga SC ukiruhusu mabao 10.

Tamko la Simba SC hili hapa

Med Ally
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC 2-0 Singida Black Stars fainali ya kibabe

Juni 27 zikiwa zimepita siku mbili tangu Simba SC ipoteza mbele ya Yanga SC, Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba SC alitoa tamko. Ally aliweka wazi kuwa baada ya kupoteza mchezo huo hakuwa na nguvu na alipopata nguvu akarejea kuzungumza. Ipo wazi kuwa Simba SC ilikosa kombe na pointi tatu mbele ya Yanga SC.

“Nianze na pole kwa Wanasimba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususani ligi kuu ya NBC. Wana Simba tuepuke presha za wanaotuaminisha tumefeli kupita kiasi.

 “Ni kweli hatujapata ubingwa lakini sote ni mashahidi kuwa timu yetu imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma na hilo ndio lilikua lengo letu kutengeneza timu ya ushindani.

“Msimu huu tumefanikiwa kucheza Fainali ya CAF ambayo tumeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 31.Msimu huu ubingwa wa ligi umeamuliwa na dakika 45 za kipindi cha pili cha mechi ya mwisho, wakati msimu uliopita tulipigania nafasi ya tatu.

“Pointi tulizofikisha msimu huu hatujawahi kufikisha kwa miaka minne iliyopita. Tulipotoka na tulipo ni tofauti sana, mwangaza wa mafanikio hauko mbali yetu. Si mara ya kwanza Simba SC kukaa miaka minne bila Ubingwa. Tushakaa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017 lakini tulijipanga 2018 tukachukua kwa miaka minne mfululizo.

Kupoteza mara 5 Kariakoo Dabi

Mutale vs Mwenda
Mutale vs Mwenda mchezo wa Kariakoo Dabi 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC asilimia ndogo kubaki

“Kupoteza mara 5 mfululizo dhidi ya Mtani kusitufanye tukajidharau. Madrid amepoteza El Classico nne dhidi Barcelona tena kwa vipigo vikali lakini katu huwezi kuwaona wanajitukana.

“Sio mfano wa kujivunia lakini lazima tukubali nyakati hizi hutokea kwenye mpira. Pamoja na ukubwa wote Manchester United wanaenda mwaka wa 13 bila ubingwa. Sitaki kutoa mfano wa Arsenal.

“Mifano hii itupe taswira kuwa hatuko peke yetu kwenye mapito ya namna hii na hata hawa wanaocheka sasa yapo magumu waliyopitia. Ombi langu wangu Wana Simba, tuwape nafasi viongozi wetu wafanye tathmini na baada ya hapo watupe muongozo tunaendaje mbele kuipambania Simba yetu.

“Heshima yetu itarudi kwa kushikamana na kusimama pamoja. Nguvu Moja,” alimaliza Ally kuandika kupitia ukurasa wa Instagram.

Hitimisho

Simba SC msimu wa 2024/25 imeambulia patupu. Ilitinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika ikagotea nafasi ya pili. RS Berkane alitwaa ubingwa kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-1. Katika CRDB Federation Cup iligotea hatua ya nusu fainali katika ligi ni nafasi ya pili kwenye msimamo.

SEO Banner LV
Share this: