Yanga kupeleka Kombe la ubingwa wa ligi ya NBC IkuluAli Kamwe (-)
  • Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB, Yanga yaifanyia Singida Umafia mzito.
  • Fainali hii inatarajiwa kupigwa Jumapili ya Juni 29 na kufikia kilele cha mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB 2024/25.
  • Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Desemba 29, 2024 na Singida kukubali kipigo cha mabao 5-0

Ni Umafia mzito! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo kuelekea mchezo wa Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB ambayo imepangwa kupigwa Jumapili ya Juni 29, uongozi wa Yanga umeficha muda ambao kikosi chao kimeondoka Dar es Salaam siku ya leo Ijumaa. Hii ikiwa sehemu ya mbinu za kivita kwao kushinda mchezo wa Fainali.

Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB moto utawaka Zanzibar

Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB
Uwanja wa New Amaan Complex

Mara baada ya kuikanda Simba SC mabao 2-0 na kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Bara juzi Jumatano, uongozi wa Yanga sasa nguvu zote wamezielekeza katika kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Black Stars siku ya Jumapili pale kenye Uwanja wa New Amaan Complex.

Licha ya mabadiliko ya siku ya mchezo, ambao hapo awali ulipaswa kupigwa kesho Jumamosi ya Juni 28, na kupelekwa keshokutwa Juni 29, mwaka huu lakini sehemu kubwa ya uratibu wa mchezo huo hazijabadilika ambapo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar saa 2:15 usiku.

Mchezo huu wa fainali katika msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa kivumbi cha soka, ambapo timu hizi mbili zitapigania taji la pili kwa ukubwa, thamani na umuhimu nchini Tanzania huku timu hizo zikitajwa kuwa na vikosi bora.

SOMA HII PIA: Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP/ Pacome na Jean Ahoua kitaumana

Safari ya Yanga SC kufika fainali ilikuwaje?

Pacome vs Simba SC
Kiungo wa Yanga, Pacome

Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo huku wakitetea na Kombe hilo la CRDB, wameonyesha kiwango cha juu katika michuano msimu huu ambapo katika hatua ya nusu fainali, walikutana na JKT Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ushindi huo unaonyesha ubora wa kikosi cha Yanga chini ya kocha Miloud Hamdi, ambaye ameweza kuunda timu imara inayocheza soka la kuvutia na kushambulia kwa kasi na kuwa na wastani msuri wa kufunga mabao.

SOMA HII PIA: Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mchongo huu wa ubingwa Yanga

Safari ya Singida Black Stars wamefikaje fainali

Singida Black Stars ambao ni wageni katika fainali hii, walifanya maajabu katika mchezo wa nusu fainali kwa kuifunga Simba SC mabao 3-1, magoli ya Singida yalifungwa na Jonathan Sowah (17′) na  Emmanuel Keyekesh (35′ na 48′)

Ushindi huu unaonyesha uwezo mkubwa wa Singida Black Stars, ambao wamejijengea jina la kuwa timu ngumu kupambana nayo chini ya kocha wao mpya ambaye ameleta mabadiliko makubwa katika timu, akiwafanya wachezaji wake kuwa na ari na nidhamu ya hali ya juu.

Mchezo wa Fainali Yanga wako nyumbani kikanuni

CHUMA CHA TATU !!!!!! Emanuel Keyekeh anatufungia chuma cha tatu Simba SC Singida Black Stars Jonathan Sowah Emanuel Keyekeh #Inawezekana #CRDBFederationCup ( )
Wachezaji wa Singida Big Stars wakishangilia ushindi dhidi ya Simba

Fainali ya CRDB Confederation Cup Yanga SC vs Singida Black Stars inatarajiwa kuwa kivumbi cha soka kwelikweli, Yanga SC wakiwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa, wanatarajiwa kuwa na faida ya uwanja wa nyumbani kikanuni na nguvu ya mashabiki wao ambao wanapatikana kwa wingi Zanzibar.

Hata hivyo, Singida Black Stars hawatakuwa na hofu yoyote, kwani wameonyesha uwezo wa kushinda dhidi ya vigogo wa soka nchini Tanzania. Mfano halisi ukiwa mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Simba SC.

Utabiri wa Matokeo

Ingawa Yanga SC wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uzoefu wao na ubora wa kikosi chao, Singida Black Stars wameonyesha kuwa wanaweza kushinda dhidi ya timu yoyote. Hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua na wenye ushindani mkubwa.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajia kuona burudani ya soka safi na la kuvutia kutoka kwa timu hizi mbili, hasa kutokana na ujuzi na ufundi ambao kila upande umeonyesha msimu huu.

Ilibaki kidogo Fainali iyayuke

Siku chache zilizopita mchezo huu ulibaki kidogo uote mbawa kama ilivyo msemo wa waswahili kuwa ‘Kitumbua kimeingia mchanga’ hii ni baada ya kudorola kwa mahusiano kati ya uongozi wa Yanga na wale wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.

Hii ni baada ya Yanga SC kupitia kwa Ofisa habari wao, Ali Kamwe kubainisha kuwa hawatacheza mchezo huo mpaka watakapopewa hela ya ubingwa wa msimu uliopita wa mashindano haya ambapo waliweka wazi kudai misimu mitatu iliyopita ya mashindano hayo.

Ikumbukwe Yanga ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo, ambapo imetwaa taji hilo mara nne na msimu huu wamefanikiwa kutinga kwenye fainali yake ya tano baada ya kuwafungashia virago JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0.

Shinda mamilioni na kindege cha SportPesa

Ukiwa mteja wa Kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa unayo nafasi ya kushinda mamilioni kupitia mchezo wa kindege ‘Aviator’. Cheza kwa kubonyeza hapa chini.

Hitimisho

Fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Confederation Cup kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars ni tukio muhimu katika historia ya soka nchini Tanzania, hasa kwa msimu huu wa mashindano ambao umekuwa na mafanikio makubwa kwa timu zote mbili.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.