Sopu na ZidaneSopu na Zidane
  • Yanga SC vs Simba SC vita ya ubingwa bado inaendelea ndani ya msimu wa 2024/25 mpaka watakapokutana Juni 25 2025.
  • Yanga SC ni bingwa mtetezi anaongoza ligi akiwa na pointi 79 anafuatiwa na Simba SC nafasi ya pili pointi 78.
  • Fountain Gate na Tanzania Prisons zitacheza mchezo wa mtoano, Kagera Sugar na KenGold zimeshuka daraja mazima.

Yanga SC vs Simba SC vita ya ubingwa bado inaendelea mpaka watakapokutana Juni 25 2025. Matokeo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara raundi ya 30 yana maajabu, katika viwanja 8 ni Uwanja wa Lake Tanganyika pekee dakika 90 zilikuwa ngumu kwa wababe hao kufungana huku kwenye viwanja 7 mabao yakifungwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Sure Boy vs Dodoma Jiji
SureBoy vs Dodoma Jiji Juni 22 2025. Source: Yanga SC.

Soma hii:Yanga SC vs Simba SC mbali na mchezo wa Kariakoo Dabi Juni 25 2025 wana vita nyingine

Yanga SC na Namungo FC wakiwa nyumbani walishusha nyundo ya 5G kwa wapinzani. Namungo FC ilishinda dhidi ya KenGold ambayo imeshuka daraja na Yanga SC ilishinda dhidi ya Dodoma Jiji ambayo ina uhakika wa kushiriki ligi msimu wa 2025/26.

 Simba SC ikiwa nyumbani ilifunga mchezo wa mwisho kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar ambayo imeshuka daraja. Haya hapa matokeo ya raundi ya 30 Juni 22 2025 yakifungwa mabao 26 namna hii:-

Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji

Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ambao ulichezwa Uwanja wa New Amaan. Katika mchezo huo Yanga SC walifungua ukurasa wa mabao dakika ya nne ya mchezo na kufunga ukurasa wa mabao dakika ya 90.

Duke Abuya (-)
Duke Abuya vs Dodoma Jiji, Juni 22 2025. Source: Yanga SC.

Soma hii: Yanga SC vs Dodoma Jiji FC live Zanzibar, vikosi, H2H, kituo kinachofuata Yanga vs Simba – SportPesa Tanzania

Ni Clatous Chama alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 4 akitumia pasi ya Clement Mzize, Duke Abuya alipachika bao la pili dakika ya 50 akitumia pasi ya Chama, Ibrahim Bacca alipachika bao la tatu dakika ya 62 akitumia pasi ya Maxi Nzengeli.

Beki wa kati wa Dodoma Jiji katika harakati za kuokoa hatari iliyopigwa na Farid Mussa dakika ya 90+4 alijifunga bao la nne kwenye mchezo huo na Maxi Nzengeli alikamilisha kamba ya tano dakika ya 90+7 akitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo.

Simba SC 1-0 Kagera Sugar

Mukwala- Duchu
Mukwala, Duchu na Ngoma nyota wa Simba SC kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Juni 22 2025. Source: Simba SC.

Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani ndani ya dakika 90 kwa wababe hawa kukutana ndani ya uwanja. Juma Kaseja Kocha Mkuu wa Kagera Sugar alitumia uzoefu wake kuwazuia Simba SC ndani ya uwanja licha yakupoteza baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba SC 1-0 Kagera Sugar, bao la ushindi lilifungwa na Steven Mukwala dakika ya 17. Mukwala alitumia pasi ya Duchu ambaye alipokea mpira kutoka kwa Jean Ahoua kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

Fountain Gate 2-3 Azam FC

Fountain Gate yenye Ofisa Habari Issa Mbuzi haijawa na mwendo mzuri mzunguko wa pili. Mchezo wake uliopita wa mzunguko wa 29 ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani Tanga. Funga kazi ya raundi ya 30 ilipoteza dhidi ya matajiri wa Dar, Azam FC.

Screenshot------------------sportpesa-co-tz

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa ulisoma Fountain Gate 2-3 Azam FC ni Mokono alipachika bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati, Kidemile alipachika bao la pili kwa Fountain Gate. Mabao ya Azam FC yalifungwa na Zidane dakika ya 3, Shiga alijifunga dakika ya 23 na bao la ushindi lilifungwa na Sopu dakika ya 90+2 kwa mkwaju wa penati.

Fountain Gate itacheza mchezo wa play off msimu wa 2024/25 kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi kwa msimu wa 2025/26. Ikiwa itapoteza kwenye dakika 180 za play off itakuwa imemaliza mwendo ndani ya ligi. Itashiriki Championship kusaka tiketi yakurejea ndani ya ligi kwa mara nyingine.

Namungo FC 5-0 KenGold

Kagere tuzo
Kagere tuzo raundu ya 30 dhidi ya KenGold. Source: Namungo.

Soma hii: Ufungaji bora Kariakoo Dabi kesi kumalizwa 2024/25

Namungo FC 5-0 KenGold mabao yalifungwa na Medie Kagere dakika ya 07 na 29, Hassan Kabunda dakika ya 41, Erasto Nyoni dakika ya 45, Saleh Karabaka dakika ya 90+1. Kagere alichaguliwa kuwa mchezaji bora baada ya mchezo kugota mwisho.

Singida Black Stars 3-3 Tanzania Prisons

Ubao wa Uwanja wa Liti ulisoma Singida Black Stars 3-3 Tanzania Prisons, mabao ya Pokou 43, Tchakei dakika ya 45 na Jonathan Sowah dakika ya 47.Mabao ya Tanzania Prisons yalifungwa na Ismail dakika ya 63 mkwaju wa penati na dakika ya, 76 kwa penati, Haruna Chanongo dakika ya 84.

Pamba Jiji 1-1 KMC FC

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Pamba Jiji 1-1 KMC FC ni Mathew Tegis alifunga kwa Pamba Jiji dakika ya 34 na Redemtus Musa alifunga kwa KMC. Wababe hawa waligawana pointi mojamoja kwenye mchezo huo

Coastal Union 1-1 Tabora United

Wagosi wa Kaya walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ukisoma Coastal Union 1-1 Tabora United ni Lukas Kikoti alifunga dakika ya 90 kwa mkwaju wa penati na Mwanengo alipachika bao kwa Tabora United dakika ya 53. Tabora United mchezo wake uliopita mzunguko wa 29 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 5-0 Tabora United.

Mashujaa 0-0 JKT Tanzania

Lake Tanganyika imefunga raundi ya 30 ubao ukisoma Mashujaa 0-0 JKT Tanzania. Viwanja saba dakika 90 zilikamilika kwa wababe kufungana ndani ya uwanja, ngoma ilikuwa nzito Lake Tanganyika hakukuwa na bao ambalo lilifungwa baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Msimu wa 2024/25 unatarajiwa kukamilika rasmi Juni 25 2025 kwa wababe wawili kukutana. Ni Kariakoo Dabi mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni, Yanga SC vs Simba SC. Mshindi kwenye mchezo huu atakuwa bingwa wa msimu. Ikiwa watagawana pointi bingwa atakuwa ni Yanga SC.

Share this: