- Macho ya wanasoka Tanzania inadokolea ushindi wa Yanga SC walivonyowacharaza Dodoma Jiji magoli 5 kwa bila.
- Simba SC itawaka moto kwenye kasi ya kuutafuta ubingwa wakiwa nafasi ya pili na pointi 78 tofauti ya pointi moja kibindoni.
- Kariakoo Dabi, Juni 25 kuamua nani atakuwa nani baada ya dakika 90 kugota mwisho kwa wababe hao wawili.
- Mechi ya Yanga SC vs Dodoma Jiji FC imetoka kua 5-0, Simba SC watoboa kweli?
Msimu Yanga SC wamevuragana mechi mbili, ambayo hivi maajuzi- Dodoma walisagwa tano kwa bure. Historia inanyesha kua, Yanga waishia kuifunga Dodoma Jiji Fc kwa mara tisa. Ushindi wa hivi maajuzi, si geni. Tazama jinsi Simba SC walio nafasi ya pili ya msimamo wa ligi namba nne kwa ubora Afrika, watakavyo endelea baada ya Yanga SC vs Dodoma Jiji FC kutokea 5-0.

Soma hii: Yanga SC kwenye mtihani kutinga fainali Muungano 2025
Mechi ya Yanga SC vs Dodoma Jiji FC (5-0) ya Ligu Kuu ya NBC : Simba SC wanasubiri mechi
Ushindi kwenye mchezo wa mzunguko wa 30 ambao ulipatikana kwa Yanga SC unawafanya wafikishe jumla ya pointi 79. Simba SC kibindoni ni pointi 78 kwa kuwa walipata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Juni 22 2025, kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa New Amaan, Dodoma Jiji waliacha pointi tatu mzima baada ya dakika 90 kugota mwisho. Dakika nne pekee ziliwatosha Yanga SC kufungua ukurasa wa mabao kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.
Kiungo Clatous Chama alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 4 akitumia pasi ya Clement Mzize, Duke Abuya alipachika bao la pili dakika ya 50 akitumia pasi ya Chama, Ibrahim Bacca alipachika bao la tatu dakika ya 62 akitumia pasi ya Maxi Nzengeli.
Joash Onyango beki wa Dodoma Jiji katika harakati za kuokoa hatari iliyopigwa na Farid Mussa dakika ya 90+4 alijifunga bao la nne kwenye mchezo huo na Maxi Nzengeli alikamilisha kamba ya tano dakika ya 90+7 akitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo.

Soma hii: Tuzo ya ufungaji bora vita yake inazidi kuchangamka
Huyu hapa Ali Kamwe wa Yanga SC
Ali Kamwe, Ofisa habari wa Yanga SC ameweka wazi kuwa pointi tatu ambazo walizipata mbele ya Dodoma Jiji zilikuwa na umuhimu mkubwa. Mbali na kupata ushindi wa mabao 5-0 kilichokuwa kinatafutwa kimepatikana.

“Tulikuwa tunatafuta ushindi yaani pointi tatu muhimu kwenye mchezo. Kuhusu ushindi wa mabao 5 hilo hatuangalii kwa ukaribu sana kikubwa ni pointi tatu ambazo tumepata hilo lipo wazi na tunafurahia ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wetu ujao” asisitiza Ali Kamwe.
Kamwe aendelea kusema “mchezo wetu ujao dhidi ya Simba SC ni muhimu, mashabiki wajitokeze kwa wingi. Huu ujanja ambao wenzentu wanaufanya sisi tumetoka huko siku nyingi na tunaujua. Mashabiki jitokezeni kwa wingi kununua tiketi kwa kuwa mchezo huu unamaamuzi ya ubingwa.” Simba wanakibarua kikubwa kupata ule ushindi watakavyo cheza.
Yanga SC na Simba SC wote ni wakali
Yanga SC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba SC wote ni wakali kwenye kushinda mechi zao. Hivyo moto utawaka wakikutana wababe hawa uwanjani. Kila timu haijapoteza mchezo kwenye raundi za hivi karibuni. Katika raundi ya 29 Yanga SC ilipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Tanzania Prisons ikiwa ugenini.

Soma hii: Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC dakika 180 wapigwa nje ndani
Wakati Yanga SC ikipata ushindi ugenini dhidi ya Tanzania Prisons, Simba SC ilipata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya KenGold kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na raundi ya 30 walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa KMC Complex.
Mchezo uliopita kwa Yanga SC, raundi ya 30 Juni 22 2025 ubao wa Uwanja wa New Amaan ulisoma Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji. Katika mchezo huo bao la ufunguzi lilifungwa na Clatous Chama dakika ya nne akitumia pasi ya Clement Mzize.
Yanga SC ni timu namba moja kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 79 inakwenda kukutana na timu namba mbili ambayo ni Simba SC ikiwa na pointi 78 zote zimecheza mechi 29 ndani ya ligi. Pacome Zouzoua ni miongoni mwa viungo waliohusika kwenye mabao mengi katika kikosi cha Yanga SC akiwa kahusika kwenye mabao 20 kati ya 81 ambayo yamefungwa na Yanga SC.
Ni mabao 11 kafunga, alifunga mabao mawili mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine na katika mchezo huo Juni 18, Clatous Chama alipachika bao moja dakika ya 35 akitokea benchi. Kiungo huyo alianza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji.
Simba SC mkali wa mabao ni Jean Ahoua ambaye kafunga mabao 16 na pasi 9 akihusika kwenye mabao 25 kati ya mabao 69 yaliyofungwa na timu hiyo namba mbili kufunga mabao mengi ndani ya ligi. Ahoua alianza katika kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Juni 22 2025 hakukomba dakika zote 90. Wakali hawa ndani ya dakika 180 hakuna timu iliyofungwa wala kupoteza pointi tatu muhimu.

Soma hii: Simba SC 1-0 Kagera Sugar ni mchezo wa mwisho 2024/25
Juni 25 2025, Jumatano mchezo wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu muhimu. Mshindi wa mchezo wa Dabi ana uhakika asilimia 100 kuwa bingwa. Simba SC chaguo lake ili awe bingwa ni lazima ashinde huku Yanga SC akipata sare ama kushinda anakuwa bingwa.

