- Yanga SC vs Dodoma Jiji FC live, ni zaidi ya mchezo wa ligi kwa Yanga bali ni maandalizi ya mchezo mkubwa dhidi ya Simba.
- Kituo kinachofuata kwa Yanga ni dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba mchezo utakaopigwa Juni 25, mwaka huu.
- Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Desemba 24, 2024 na Dodoma Jiji FC kukubali kipigo cha mabao 5-0.
Baada ya kusimamisha mnara wa 5G mkoani Mbeya Wanachi wanarudi uwanjani leo Jumapili kwenye mchezo wa Yanga SC vs Dodoma Jiji FC live Zanzibar, ambao unakuwa mchezo wa mzunguko wa 29 kwao, huku kituo kinachofuata kikiwa ni mchezo wa dabi ya Kariakoo dhidi ya watani zao Simba uliopangwa kupigwa Juni 25, mwaka huu.
Yanga SC vs Dodoma Jiji FC live, ngoma kupigwa Zanzibar

Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia majira ya 10:00 jioni. Mech zote za leo zinatarajiwa kupigwa saa 10:00 jioni, ambapo huu ni utaratibu wa Ligi mbalimbali duniani ili kuepusha uwezekano wa upangaji wa matokeo.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB sasa kupigwa Juni 29, Zanzibar 28/06/2025
Yanga vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara
Mpaka sasa Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB, wameonyesha kiwango cha juu katika michuano ya msimu huu ambapo wanaongoza msimamo wa ligi na pointi zao 73 walizokusanya kwenye michezo 28 ya ligi.
Makusanyo hayo ya pointi yanaonyesha na kuthibitisha ubora wa kikosi cha Yanga chini ya kocha Miloud Hamdi, ambaye ameweza kuunda timu imara inayocheza soka la kuvutia na kushambulia kwa kasi na kuwa na wastani mzuri wa kufunga mabao.
Kocha Yanga atoa tamko zito

Kuelekea katika mchezo huo kocha mkuu wa Yanga, Miloud amesema: “Tumejiandaa vizuri sana kwenye huu mchezo dhidi ya Dodoma Jiji. Tulicheza vizuri sana dhidi ya Tanzania Prisons ugenini, hivyo Wachezaji wangu wana morali nzuri.
“Hatujaja Zanzibar kuvinjari, tumekuja kusaka alama tatu. Hakuna namna, tunahitaji alama tatu na sio kitu kingine, kila timu inayocheza na sisi wanakuja kwa nguvu kujaribu kupata alama tatu. Wapinzani wetu wanatukamia sana hivyo kila mchezo nauchukulia kwa tahadhari na umakini mkubwa.
“Nina kikosi kipana sana, sina wasiwasi na wachezaji wangu. Tunauchukulia mchezo wa Dodoma Jiji kwa umakini mkubwa sana. Kama tunataka kushinda ubingwa tunapaswa kuweka akili yetu yote kwenye mchezo wa hapo kesho”
Naye kip awa Yanga, Aboutwalib Mshery kwa niaba ya wachezaji amesema: “Mechi ya Dodoma sio mechi rahisi, ni mechi ngumu kwa sababu wao pia wamejiandaa. Hatuchezi kushinda magoli mengi, tunacheza kupata alama tatu. Idadi ya magoli inatokana na hali yenyewe ya mchezo.
“Nina imani kubwa kuwa tutapata matokeo mazuri, sina mashaka na mashabiki wa Young Africans hapa Zanzibar. Tunajua namna gani wanaipenda timu yao. Mara kadhaa baadhi yao wanatoka Zanzibar kuja Bara kutazama mechi, ni matumaini yangu pia wataujaza Uwanja wa Amaani na kutupa hamasa ya kutosha kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu. Wananchi karibu sana.”
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC mbali na mchezo wa Kariakoo Dabi Juni 25 2025 wana vita nyingine
Kituo kinachofuata ‘Kariakoo Dabi’ Yanga SC vs Simba SC na fainali CRDB

Mara baada ya mchezo wa leo Yanga watasalia na michezo miwili kumaliza msimu ambapo mchezo unaofuata ni ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba SC maarufu Kariakoo Dabi Juni 25 na kufuatiwa na mchezo wa Fainali ya Kombe la CRDB juni 29, mwaka huu.
Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB
Fainali ya CRDB Confederation Cup Yanga SC vs Singida Black Stars inatarajiwa kuwa kivumbi cha soka kwelikweli, Yanga SC wakiwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa, wanatarajiwa kuwa na faida ya uwanja wa nyumbani na nguvu ya mashabiki wao.
Hata hivyo, Singida Black Stars hawatakuwa na hofu yoyote, kwani wameonyesha uwezo wa kushinda dhidi ya vigogo wa soka nchini Tanzania. Mfano halisi ukiwa mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Simba SC.
Hii ilibaki kidogo iyayuke

Siku chache zilizopita mchezo huu ulibaki kidogo uote mbawa na kuyayuka kama ilivyo msemo wa waswahili, hii ni baada ya kudorola kwa mahusiano kati ya uongozi wa Yanga na wale wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.
Hii ni baada ya Yanga SC kupitia kwa Ofisa habari wao, Ali Kamwe kubainisha kuwa hawatacheza mchezo huo mpaka watakapopewa hela ya ubingwa wa misimu mitatu iliyopita ya mashindano hayo ambayo wanaidai.
Ikumbukwe Yanga ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo, ambapo imetwaa taji hilo mara nne na msimu huu wamefanikiwa kutinga kwenye fainali yake ya tano baada ya kuwafungashia virago JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0.
SOMA HII PIA: Ufungaji bora Kariakoo Dabi kesi kumalizwa 2024/25/ Jean Ahoua, Clement Mzize kwenye kasi
Shinda Bilioni ya SportPesa Supa Jackpot
Unaweza kujishindia zaidi ya Bilioni 1 ya SportPesa Supa Jackpot kwa kubonyeza picha hii chini

Hitimisho
Ni wazi ratiba ya Yanga inaonekana kuwabana kwani wana michezo mitatu muhimu ndani ya siku 7 tu, lakini hii ni nafasi nyingine kwao kuweza kuthibitisha ubora na upana wa kikosi chao katika kufanya mabadiliko ya wachezaji.

