- Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB inatarajiwa kupigwa Jumapili ya Juni 29, tofauti na Juni 28 iliyotangazwa awali.
- Fainali hii ni kilele cha mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB maarufu (FA), kwa msimu 2024/25.
- Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa Desemba 29, 2024 na Singida kukubali kipigo cha mabao 5-0
Mnara wa 5G umesoma kwa wakubwa Simba, Yanga na Azam kwenye Ligi Kuu Bara, lakini habari kubwa ni mechi ya Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB ambayo sasa imepangwa kupigwa Jumapili ya Juni 29 ikiwa ni mabadiliko madogo kutoka Juni 28 tarehe ya awali.
Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali CRDB ngoma kupigwa Zanzibar

Licha ya mabadiliko ya siku ya mchezo, lakini sehemu kubwa ya uratibu wa mchezo huo hazijabadilika ambapo unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar kuanzia majira ya saa 2:15 usiku.
Mchezo huu wa fainali katika msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa kivumbi cha soka, ambapo timu hizi mbili zitapigania taji la pili kwa ukubwa, thamani na umuhimu nchini Tanzania huku timu hizo zikitajwa kuwa na vikosi bora.
SOMA HII PIA: Mechi Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28 2025: Wananchi wasisitiza ‘Dawa ya deni ni kulipa’
Safari ya Yanga SC fainali ilikuwaje?
Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe hilo la CRDB, wameonyesha kiwango cha juu katika michuano msimu huu ambapo katika hatua ya nusu fainali, walikutana na JKT Tanzania na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Ushindi huo unaonyesha ubora wa kikosi cha Yanga chini ya kocha Miloud Hamdi, ambaye ameweza kuunda timu imara inayocheza soka la kuvutia na kushambulia kwa kasi na kuwa na wastani msuri wa kufunga mabao.
Safari ya Singida Black Stars kufuzu fainali

Singida Black Stars ambao ni wageni katika fainali hii, walifanya maajabu katika mchezo wa nusu fainali kwa kuifunga Simba SC mabao 3-1, magoli ya Singida yalifungwa na Jonathan Sowah (17′) na Emmanuel Keyekesh (35′ na 48′)
Ushindi huu unaonyesha uwezo mkubwa wa Singida Black Stars, ambao wamejijengea jina la kuwa timu ngumu kupambana nayo chini ya kocha wao mpya ambaye ameleta mabadiliko makubwa katika timu, akiwafanya wachezaji wake kuwa na ari na nidhamu ya hali ya juu.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya CRDB, H2H Ngoma kupigwa Zanzibar 28/06/2025
Mchezo wa Fainali

Fainali ya CRDB Confederation Cup Yanga SC vs Singida Black Stars inatarajiwa kuwa kivumbi cha soka kwelikweli, Yanga SC wakiwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa, wanatarajiwa kuwa na faida ya uwanja wa nyumbani na nguvu ya mashabiki wao.
Hata hivyo, Singida Black Stars hawatakuwa na hofu yoyote, kwani wameonyesha uwezo wa kushinda dhidi ya vigogo wa soka nchini Tanzania. Mfano halisi ukiwa mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Simba SC.
Utabiri wa Matokeo
Ingawa Yanga SC wanapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na uzoefu wao na ubora wa kikosi chao, Singida Black Stars wameonyesha kuwa wanaweza kushinda dhidi ya timu yoyote. Hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua na wenye ushindani mkubwa.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania wanatarajia kuona burudani ya soka safi na la kuvutia kutoka kwa timu hizi mbili, hasa kutokana na ujuzi na ufundi ambao kila upande umeonyesha msimu huu.
Ilibaki kidogo Kitumbua kiingie mchana

Siku chache zilizopita mchezo huu ulibaki kidogo uote mbawa kama ilivyo msemo wa waswahili kuwa ‘Kitumbua kimeingia mchanga’ hii ni baada ya kudorola kwa mahusiano kati ya uongozi wa Yanga na wale wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.
Hii ni baada ya Yanga SC kupitia kwa Ofisa habari wao, Ali Kamwe kubainisha kuwa hawatacheza mchezo huo mpaka watakapopewa hela ya ubingwa wa misimu mitatu iliyopita ya mashindano hayo ambayo wanaidai.
Ikumbukwe Yanga ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo, ambapo imetwaa taji hilo mara nne na msimu huu wamefanikiwa kutinga kwenye fainali yake ya tano baada ya kuwafungashia virago JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0.
SOMA HII PIA: Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC dakika 180 wapigwa nje ndani/ Kariakoo Dabi inakuja
Hitimisho
Fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Confederation Cup kati ya Yanga SC vs Singida Black Stars ni tukio muhimu katika historia ya soka nchini Tanzania, hasa kwa msimu huu wa mashindano ambao umekuwa na mafanikio makubwa kwa timu zote mbili.
Shinda zaidi ya Bilioni ya Supa Jackpot kwa kubonyeza hapa chini


