- Simba SC kuachana na makipa wake wote kuelekea msimu mpya wa 2025/26 ikiwa ni tetesi ambazo zinaendelea.
- Air Manula anatajwa kuwindwa na mabosi wake wa zamani Azam FC ambao huenda wakamchukua bure kwa kuwa mkataba wake unagota mwisho.
- Camara kipa namba moja wa Simba SC amewekwa kwenye mtego akiboronga kwa mara nyingine Thank You itakuwa juu yake.
Simba SC kuachana na makipa wake wote kuelekea 2025/26 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku wakiwa na mpango wa kuwaacha nyota zaidi ya watano kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni kumalizika kwa mikataba yao, benchi la ufundi kutoridhishwa na viwango vyao taarifa zinaeleza hivyo.

Taarifa zinaeleza kuwa kwenye upande wa makipa, Simba SC inahesabu zakuanza upya kwa kuachana na makipa wake wote waliopo kwenye kikosi hicho licha ya uwezo walionao kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimekuwa zikielezwa. Kumekuwa na mvutano mkubwa kuhusu kuwaacha makipa hao ama wabaki hivyo ripoti ya benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids itaamua.
Moussa Camara kipa namba moja
Moussa Camara, kipa namba moja wa Simba SC ambaye ni kinara kwenye hati safi ndani ya ligi msimu wa 2024/25 anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuachwa na mabosi wa Simba SC kutokana na makosa ambayo yamekuwa yakiigharimu timu kwenye mechi muhimu.

Soma hii: Usajili mpya Yanga balaa! Sowah, Bada, Chikola kwenye Yanga mpya
Taarifa zinaeleza kuwa sakata lake kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga SC bado halijagota mwisho kwa kuwa fukuto bado linaendelea na kipimo chake kitakuwa kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili inayotarajiwa kuchezwa Juni 25 2025.
Licha ya kukusanya hati safi 17 kwenye ligi bado anatajwa kufanya makosa yakujirudia akiwa uwanjani jambo ambalo liliifanya Simba SC kupoteza Kombe la Shirikisho Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya RS Berkane ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Hivyo ambacho kinatazamwa kwa sasa ni mwendelezo kwenye mechi ambazo zimebaki ndani ya ligi msimu wa 2024/25 ambao unatarajiwa kugota mwisho Juni 25 2025 baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi na utafungwa rasmi baada ya fainali ya CRDB Federation Cup.
Ally Salim kipa namba mbili wa Simba SC

Soma hii:Wachezaji wa Simba SC watakao achwa msimu wa 2025/26
Ally Salim kipa namba mbili wa Simba SC ambacho kinatajwa kumuondoa hapo ni kukwama kuongezeka ubora wake. Licha ya kuwa hapo kwa muda mrefu ndani ya Simba SC kiwango chake kimekuwa kikipanda na kushuka pengine ni kutokana na kutopewa nafasi mara kwa mara kikosi cha kwanza.
Kwenye ligi msimu wa 2024/25 ni mechi mbili kati ya 27 alikaa langoni na alifanikiwa kuondoka na hati safi huku mechi 25 langoni alikaa kipa namba moja Mousa Camara. Mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Black Stars alipofungwa mabao 2 aliwashtua mabosi wa Simba SC ambao walikuwa wanaamini kipa huyo bado yupo imara.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ulisoma Simba SC 1-3 Singida Black Stars na mshindi alikuwa Singida Black Stars ambaye anakwenda fainali kucheza na Yanga SC.
Makosa ambayo aliyafanya yamewagawa mabosi Simba SC wengine wanahitaji kuona kijana huyo anaendelea kubaki hapo huku wengine wakiamini ni muda sahihi kumruhusu kwenda kupata changamoto nyingine.
Hussen Abel kipa namba tatu Simba SC
Kipa huyu ambaye aliibuka Simba SC akitokea KMC hajawa kwenye ubora kwa muda kutokana na kukosa nafasi kuanza kikosi cha kwanza huku akikwama kabisa kucheza mchezo wa ligi kwa msimu wa 2024/25 ambao ushindani wake ni mkubwa.

Abel kutopata kwake nafasi kunatoa ruhusa kwa Simba SC kuachana naye ili akalinde kiwango chake kwa kwenda katika timu nyingine ambazo zinahitaji huduma yake licha ya mabosi wengine Simba SC kudaiwa kuwa bado wanaamini akipewa nafasi atafanya vizuri.
Aishi Manula kipa wa Simba SC

Isome hii:Aishi Manula anaondoka Simba SC, Fei Toto atajwa Yanga SC
Wengi hupenda kumuita Air Manula, Aishi Manula kipa mwenye uwezo mkubwa kwenye kuokoa hatari na kutimiza majukumu yake akiwa kwenye mechi za ushindani. Hajawa kwenye ubora ndani ya 2024/25 kutokana na kile ambacho kilielezwa na uongozi wa Simba SC kwamba nyota huyo hayupo fiti kwa asilimia 100.
Katika msimu wa 2024/25 wakati Simba SC ikiwa imecheza jumla ya mechi 27 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Air Manula hajapata nafasi yakukomba hata dakika moja katika uwanja kutimiza majukumu zaidi ya kuishia kwenye mchezaji wa akiba na sio mechi zaidi ya tano.
Taarifa zinaeleza kuwa Manula ambaye mkataba wake unatarajiwa kugota mwisho msimu wa 2024/25 utakapoisha hajaitwa kuongezewa mkataba wala mazungumzo hayajaanza kufanyika na mabosi wa Simba SC ikiwa ni tafsiri kwamba hatakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2025/26.
Ni Azam FC wanatajwa kuwa kwenye mpango wa kuinasa saini ya kipa Air Manula ambaye aliongeza mkataba wa miaka mitatu ndani ya Simba SC unaotarajiwa kugota mwisho 2025 hivyo atasepa ndani ya kikosi cha Simba SC bure ikiwa hataongezewa mkataba.
Ayoub Lakred
Ayoub Lakred kwa msimu wa 2024/25 alianza na majanga kwenye maandalizi ya msimu mpya baada ya kupata maumivu kambini.Ni Camara aliletwa kuchukua mikoba yake hajaonekana uwanjani kwenye mechi za ushindani ndani ya msimu wa 2024/25 anatajwa kuwa huenda akakutana na Thank You.

