- Usajili mpya Yanga balaa! Injinia kushusha vyuma tishio majina ya Sowah, Bada na Chikola yatajwa.
- Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), iko ukingoni ambapo timu zimesaliwa na mechi 2 au 3 tu.
- Za ndaani nyingine kutoka Yanga ni kuwa tayari wamemalizana na viungo, Pacome na Maxi.
Tetesi za usajili wa dirisha kubwa kuelekea msimu ujao wa 2025/26 zimezidi kupamba moto, ambapo huko Jangwani unaambiwa usajili mpya Yanga ni balaa! Tayari majina ya Straika, Jonathan Sowah, Arthur Bada na Offen Chikola wanatajwa kutua kuijenga Yanga mpya, huku Zouzoua Pacome, Maxi Nzengeli na nahodha wao Job wakiwa kwenye hatua za mwisho kusaini mikataba mipya.
Kuhusu usajili mpya wa Yanga huku Sowah, Bada kule Chikola

Ligi Kuu Bara (NBC Premier League), inaelekea ukingoni ambapo timu zimesaliwa na mechi 2 au 3 tu, huku dirisha kubwa la usajili likitarajiwa kufunguliwa rasmi baada ya ligi kuisha, kwa ajili ya timu mbalimbali kufanya maboresho ya vikosi vyao kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Yanga wameanza mapema mchakato wa kuboresha kikosi chao ambapo taarifa za uhakika zimeeleza wako katika hatua nzuri ya mazungumzo na baadhi ya mastaa akiwemo straika hatari wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah ambaye amefunga zaidi ya magoli 11.
Sowah aliyejiunga na Singida kupitia dirisha dogo la usajili la mwezi Januari anatajwa kuwa straika hatari zaidi nchini kwa sasa kutokana na kasi yake ya kutupia kambani, akifikisha zaidi ya mabao 10 katika kipindi cha nusu msimu tu, tofauti na anaoshindana nao.
SOMA HII PIA: Hatuchezi ya Yanga SC imehamia Simba SC kuelekea Juni 15, Mambo yazidi kuharibika
Sowah mwenyewe anaitaka Yanga
Katika nyakati kadhaa straika huyo amenukuliwa kuwa kwenye uhusiano wa karibu na mabosi wa Yanga hususani Rais wa timu hiyo, Hersi Said, hali ambayo inatoa matumaini makubwa kwa Yanga kumvalisha jezi ya Wananchi msimu ujao.
Taarifa ya kuaminika kutoka ndani ya Yanga iliyothibitishwa na mchambuzi, Hans Raphael imesema: “Yanga wako kwenye mazungumzo ya kina na nyota wawili wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah na Arthur Bada na kiungo wa Tabora United, Offen Chikola.
Kuhusu sakata la Mzize na Aucho

Taarifa nyingine ambayo imekuwa na moto kutoka ndani ya Yanga ni kuhusiana na Yanga kupokea ofa 3 zinazohitaji huduma ya straika wao, Clement Mzize ambazo ni JS Kabylie, Zamalek na Al Ittihad ya Libya huku ofa ya Zamalekh ikiwa ni kubwa kuliko.
Hii inakuja mara baada ya Yanga kufanya biashara ya kumuuza aliyekuwa kiungo wao, Aziz Ki kwa dola za marekani zinazokadiriwa kufikia 350k ambaye amejiunga na kikosi cha Wydad Athletic Club ya Morocco.
Lolote linaweza kutokea katika dili hili na huenda uongozi wa Yanga ukatoa taarifa rasmi ya kumuaga Mzize hivi karibuni, akiwa ni staa wa pili baada ya hivi karibuni kuagana na Mbukinabe, Aziz Ki aliyetimkia Wydad AC.
Kuhusu kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho taarifa kutoka ndani ya Yanga zimethibitisha kuwa, mpaka sasa hakuna mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Yanga na Aucho. Ikumbukwe mkataba wa Yanga na Aucho unaisha mwishoni mwa msimu huu.
SOMA HII PIA: Mechi namba 184 Yanga SC vs Simba SC ni pasua kichwa/ CEO Almasi Kasongo asimamishwa na Rais
Pacome, Maxi kimeeleweka Yanga, ishu ya Job na Simba iko hivi

Za ndaani nyingine kutoka kwa Wananchi ni kuwatayari Yanga wamemalizana na viungo, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli na wapo katika hatua za mwisho za kumalizana na nahodha wao, Dickson Job kwenye mikataba mipya.
Yanga wamefanya mazungumzo na Dickson Job ili kusaini mkataba mpya, mkataba wa Job na Yanga unamalizika rasmi mwishoni mwa msimu huu na Job ametaja ofa yake na Yanga wameomba muda wa kuichakata kabla ya maamuzi ya mwisho kufanyika.
Yanga wanamuona Job kama mchezaji muhimu kwenye kikosi chao na Job anaiheshimu Yanga na kuipa kipaumbele cha kwanza. Siku kadhaa zilizopita Simba waliulizia upatikanaji wake na wakaahidi kupeleka ofa yao ya kwanza baada ya fainali ya CAF, ameeleza Hans.
SOMA HII PIA: Mechi Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28 2025: Wananchi wasisitiza ‘Dawa ya deni ni kulipa’
Je, Diakite ni mrithi sahihi wa Aucho Yanga?

Kufuatia uwezekano wa kuachana na Aucho inaelezwa Yanga wanaiwinda saini ya kiungo wa ulinzi wa Djoliba AC, Daba Diakite raia wa Mali. Yanga wanamsaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21ili kuweza kuwa mbadala wa Aucho ikiwa wataachana nae.
Diakite amebakiza siku chache ndani ya mkataba wake wa sasa, hivyo huenda akaondoka kama mchezaji huru. Msimu uliopita Manchester Utd walituma scout wao kumtazama Diakite, Benfica Lisbon nao walifanya hivyo na huku Africa Kaizer Chiefs na De Tunis wanamtaka kiungo huyo.

