Kocha Simba FadluKocha Simba Fadlu
  • Hatuchezi ya Yanga SC imehamia Simba SC kuelekea Juni 15, hii ni baada ya Simba kutoa msimamo mzito leo Alhamisi.
  • Hali ilivyo kwa sasa imechukua taswira ya msemo wa mwaga mboga nimwage ugali.
  • Mchezo huo namba 184 ambao awali ulipangwa kupigwa Machi 8, 2025 umepangwa kupigwa Juni 15, 2025.

Mambo yanazidi kuharibika kuhusiana na mchezo namba 184 wa dabi ya Kariakoo ambapo jioni ya leo Julai 6, 2025 kauli ya hatuchezi ya Yanga sasa imehamia Simba kuelekea Juni 15, yaani siku ya Jumapili pale kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Hii ni mara baada ya uongozi wa Simba kutoa msimamo mzito zikisalia siku 3 tu, kabla ya mchezo huo.

Hii hapa taarifa rasmi kwa Umma iliyotolewa na Simba jioni hii

Uongozi wa Simba SC jioni hii umetoa taarifa ifuatayo: “Klabu ya Simba inautaarifu Umma, wanachama na wapenzi wake kuwa itaingia uwanjani siku ya Jumapili Juni 15, 2025 kushiriki mchezo namba 184 kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.

“Mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu. Kwa msingi huo, Klabu ya Simba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa siku ya Junapili Juni 15 2025.

“Tunawaomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kuijaza Benjamini Mkapa siku hiyo muhimu, ili kuiunga mkono timu yetu.”

SOMA HII PIA: Yanga SC vs Simba SC iliyopangwa Juni 15 2025: Ngoma imekuwa ngumu, Yanga yatishia maamuzi magumu

Kuhusu sakata la mchezo namba 184 Yanga SC vs Simba SC

Mchezo huu wa Ligi Kuu Bara umekuwa maarufu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania hasa kutokana na siasa za soka zilizoughubika. Kabla ya kupangwa kwa tarehe mpya ya Juni 15, awali mchezo huu ulipangwa kufanyika tarehe 8 Machi 2025.

Licha ya maandalizi yote ya muhimu ya mchezo huu ikiwemo uuzaji wa tiketi na kikao cha timu zote mbili kabla ya mechi ‘pre-match meeting’, lakini mchezo uliahirishwa muda mfupi kabla ya kuanza kutokana na mivutano iliyozuka kabla ya pambano hilo.

Machi 7, mwaka huu kikosi cha Simba SC kilitangaza rasmi kutoshiriki mchezo huo baada ya kudai kilizuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, tofauti na matakwa ya kanuni ya 17(45) ya Ligi inayoiruhusu timu ngeni kufanya mazoezi kabla ya mechi.

Simba ilidai wachezaji wake walizuiwa kuingia uwanjani na walinzi wa Yanga SC, jambo lililozua mgogoro mkubwa. Katika kujibu tuhuma hizo, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), iliamua kuahirisha mchezo huo ili kuchunguza.

SOMA HII PIA: Simba SC yawatoa mashaka mashabiki yabainisha Kariakoo Dabi itachezwa Juni 15 2025

Semaji Ahmed apigilia msumali mechi ipo palepale

Kuhusiana na sakata la mchezo huo Meneja Idara wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema wao wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo hivyo mashabiki wasiwe na mashaka mchezo upo kwa mujibu wa bodi ya ligi.  

“Sisi kama Simba SC tunafanya maandalizi makubwa ni maandalizi kabambe kuelekea mechi yetu ya tarehe 15, kwa sababu ni mechi ambayo lazima sisi viongozi lazima tuichukue kwa ukubwa wake na itatukutanisha na watani zetu wa jadi.

“Ni mechi ambayo lazima tuifanyie maandalizi makubwa kwa kuwa tunakutana na mpinzani wetu mkubwa katika nchi hii ambaye tunawania naye ubingwa wa ligi.

“Lakini wapo Wanasimba wengine ambao wanayumbayumba, lakini ninapenda kuwathibitishia hii kwa Wanasimba kuwa mechi yetu namba 184 ipo palepale siku ya Jumapili. Kwa mujibu wa bodi ya ligi Tanzania imethibisha hivyo kwa maneno na kimaandishi.”

“Wanasimba wasiwe na mashaka wasiwe na wasiwasi wowote mechi ipo palepale, benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Fadlu Davids linaendelea na maandalizi ya mchezo wetu Uwanja wa Mkapa saa 11 Juni 15 2025 Uwanja wa Mkapa.”

Msimamo wa Yanga ni upi

Uongozi wa Yanga kupitia kwa, Ofisa Habari wa Yanga SC Juni 9 2025 alibainisha kuwa wametoa matakwa manne ambayo ni lazima yafanyiwe kazi kabla ya wao kukubali kucheza mchezo huo katika tarehe nyingine na sio Juni 15.

Katika kutoa msimamo huo, Kamwe amesema: “Takwa letu la kwanza na la pili linahusu ukiukwaji wa kanuni uliofanyika Machi 8. Tunataka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi pamoja na CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wawajibike kwa kujiuzulu.

“Klabu ya Yanga SC haitakuwa tayari kushiriki mechi namba 184 kama kamati nzima ya uendeshaji na usimamizi wa bodi haitajiuzulu. Takwa letu la tatu ni kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao na nne tunataka bodi huru.”

SOMA HII PIA: Mechi Yanga SC vs Singida Black Stars Juni 28 2025: Wananchi wasisitiza ‘Dawa ya deni ni kulipa’

Hitimisho

Hatuchezi ya Yanga SC imehamia Simba SC kuelekea Juni 15 na mpaka sasa hatuchezi ya Yanga SC ambayo imehamia Simba SC na kuelekea Juni 15, inabaki kuwa kitendawili kigumu cha kutatua ikiwa mechi hii itachezwa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.