- Simba SC 1-3 Singida Black Stars Mei 31, ni mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB, ambao umemalizika kwa Simba kukubali kipigo na kufurushwa nje ya mashindano hayo.
- Kufuatia matokeo hayo, Singida Black Stars wamefuzu fainali ambapo watavaana na Yanga SC kwenye fainali ya CRDB msimu huu wa 2024/25.
- Katika michezo 3 ambayo, Ahoua ameichezea Simba dhidi ya Singida amehusika kwenye mabao yote matatu ambayo Simba wamefunga, amefunga bao moja na kuasisti mara 2, Mpaka sasa kwenye Ligi, Ahoua katoa pasi 8 za mabao na kufunga mabao 15.
Simba SC 1-3 Singida Black Stars Mei 31, ni mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB, ambao umemalizika kwa Simba kukubali kipigo na kufurushwa nje ya mashindano hayo, huku Singida Black Stars wakifuzu fainali ambapo watavaana na Yanga SC kwenye fainali.
Simba SC 1-3 Singida Black Stars Mei 31 mchezo ulikuwaje?

Simba walianza mchezo huu wakiwa na mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chao cha kwanza, ambapo baadhi ya mastaa ambao wamekuwa wakianza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza walianzia benchi wakiwemo Ellie Mpanzu, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein.
Kocha wa Singida BS, David Ouma hakubadilika kutoka mchezo uliopita ambao walipoteza bao 1-0, kwani alihakikisha anakuwa na idadi nzuri ya wachezaji wakati unazuia, walipojenga shambulizi na kuhakikisha wanafanya vitu vya kimsingi zaidi.
Singida BS pia walifanikiwa kuwa na ufanisi mkubwa mbele ya goli la Simba, katika wakati ambao wapinzani wao walifanya makosa mengi tena kwenye maeneo hatarishi hili lilithibitika dakika ya 35 ya mchezo na Emmanuel Keyekeh.
Licha ya kutoanza mchezo vizuri Simba kipindi cha pili walibadilisha aina ya uchezaji wao, tofauti na kipindi cha kwanza na kufanikiwa kufunga bao pekee la kufutia machozi la Jean Ahoua, mara baada ya kutanguliwa kwa mabao matatu na mchezo kumalizika kwa 1-3.
SOMA HII PIA: Simba SC vs Singida Black Stars Mei 31 nusu fainali CRDB Cup, Yanga SC yupo pale
Nyota hawa walikuwa na siku bora kazini
Straika, Jonathan Sowah alikuwa na mchezo mzuri sana leo; nguvu, kasi na umaliziaji bora. Keyekeh ambaye alitajwa mchezaji bora wa mechi na Edmund waliocheza winga walifanya vitu vinavyotakiwa kwa nyakati sahihi.
Mlinzi wa Singida, Assinki “KITASA” alizima vizuri sana, Kennedy mipira yote ya juu yake.
Ahoua aendelea kuitesa Singida Black Stars

Katika michezo mitatu ambayo Ahoua ameichezea Simba msimu huu dhidi ya Singida amehusika kwenye mabao yote matatu ambayo Simba wamefunga, ambapo amefunga bao moja na kuasisti mara 2.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza alitoa pasi ya bao kwa Ngoma na kwenye mchezo wa mzunguko wa pili, Simba SC ilivuna pointi tatu kwa bao la Mukwala ambaye ni mshambuliaji. Nyota huyo naye alitumia pasi ya Ahoua kuimaliza Singida Black Stars.
Mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, Ahoua katoa pasi 8 za mabao huku akifanikiwa kufunga jumla ya mabao 15 msimu wa 2024/25.
SOMA HII PIA: Simba SC 1-0 Singida Black Stars 28 Mei 2025: Matokeo, magoli, wafungaji, h2h, Kifuatacho Kariakoo Dabi
Rekodi za H2H, Simba SC vs Singida Black Stars CRDB Federation Cup
Rekodi zinaonyesha kuwa timu hizo zimekutana mara 10 katika michuano yote na ushindi wa Jumamosi ni wa kwanza kwa Singida Black Stars, kwani katika michezo yote iliyosalia ameambulia sare mara moja na kufungwa mechi 9.
Sowah ndiyo habari ya mjini
Straika wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo kasi yake ya kufunga mabao imeendelea kushtua wengi, licha ya kusajiliwa kwenye dirisha dogo la mwezi Desemba hadi Januari namba zake zinatisha.
Mpaka sasa, Sowah amefanikiwa kuifungia Singida Black Stars mabao 11, huku akiwa amefanikiwa kuwatungua makipa wote bora ambao wanaongoza kitakwimu, Djigui Diarra wa Yanga na Pinpin Camara wa Simba.
Sasa ni Yanga SC vs Singida Black Stars Fainali ya Kombe la CRDB

Kufuatia matokeo ya nusu fainali hii ya pili, Simba sasa ni rasmi ametupwa nje ya mashindano hayo na fainali sasa itazikutanisha timu za Yanga SC ya Dar es Salaam na Singida Black Stars.
Ikumbukwe kwamba Yanga SC waliifikia hatua hiyo ya Fainali baada ya kuwafungashia virago JKT Tanzania, katika mchezo wa Nusu Fainali ambao ulipigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Simba imepoteza uwezekano wa kushinda makombe mawili ndani ya kipindi cha wiki moja, ambapo walianza kwa kupoteza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kisha wamepoteza uwezekano wa kushinda ubingwa wa Shirikisho CRDB.

