- Simba SC kucheza mechi nne ndani ya siku 10 Mei 2025 msako wa pointi tatu muhimu dakika 360
- Kiporo chao dhidi ya KMC kupigwa Tabora ndani ya dakika 90 sio Dar
- Deni lao kwa Yanga SC linaanza upya kwenye eneo la utupiaji
SIMBA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ratiba yake kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora ni bandika bandua ndani ya dakika 360.

Mechi hizo zote ni viporo ambavyo vimetokana na Simba SC kuwa kwenye majukumu katika mechi za kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikiandika rekodi ya kutinga hatua ya fainali.
HIZI HAPA MECHI ZA SIMBA SC
Simba SC vs Mashujaa
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Mei 2 2025, Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana uwanjani kwenye msako wa pointi tatu muhimu. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba SC ilipata ushindi wa bao 1-0 ugenini mtupiaji akiwa ni Steven Mukwala akitumia pasi ya Awesu Awesu.

JKT Tanzania vs Simba
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Isahmuyo, Mei 5 ikiwa ni mzunguko wa pili. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba 1-0 JKT Tanzania. Bao la ushindi kwenye mchezo lilifungwa na Jean Ahoua kwa pigo la penati iliyosababishwa na Shomari Kapombe dakika ya 90.
Simba SC vs Pamba
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Mei 8 2025, Uwanja wa KMC Complex. Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake kibindoni ni 57 inakutana na Pamba Jiji iliyo nafasi ya 13 pointi zake ni 27.
KMC vs Simba, Mei 11 2025
Mchezo huu KMC wameamua kuupeleka Tabora licha ya kuwa hutumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani. Inaruhusiwa kwa timu kuchagua uwanja mwingine kikanuni hivyo KMC wameamua kuutumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
Simba SC imefunga mabao 48 ndani ya 18
Rekodi zinaonyesha kuwa Simba SC ni wachezaji ni wakali kwenye kucheka na nyavu wakiwa ndani ya 18 wakiwa wamefunga jumla ya mabao 48. Nje ya 18 Simba SC wachezaji wamefunga mabao manne baada ya kucheza mechi 22.
Kinara wa utupiaji mabao ndani ya kikosi cha Simba SC ni kiungo mshambuliaji Jean Ahoua ambaye ametupia mabao 12 na katengeneza pasi 7 za mabao ndani ya msimu wa 2024/25.
Simba SC ina deni na Yanga SC
Simba SC inadaiwa na watani zao wa jadi Yanga SC kwenye idadi ya mabao yakufunga ambao imeachwa kwa tofauti ya mabao 16 mechi hizi nne ambazo inakwenda kucheza ikikamilisha itawafikia Yanga kwenye idadi ya mechi ambazo ni 26.
Nafasi ya Simba SC
Simba SC ni nafasi ya pili kwenye msimamo inaingia kwenye orodha ya timu zenye mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 52 na pointi zake kibindoni ni 57 ambazo wamekusanya ndani ya msimu wa 2024/25.

Katika dakika 1,980 ilizocheza imekuwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38 ndani ya uwanja. Inaingia uwanjani kwenye msako wa pointi 12 katika mechi nne ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa wapinzani wao wanahitaji pointi tatu pia muhimu.
Wametoka anga la kimataifa
Simba SC imetoka kucheza mchezo wa kimataifa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika wakikata tiketi ya kutinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni rekodi iliyoandikwa na timu hiyo inayopeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa jambo lilisababisha iwe nit imu iliyoheza mechi chache ndani ya ligi.
Ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Amaan ulidumu mpaka dakika 90 za kumsaka mshindi wa jumla kwenye nusu fainali ya pili iliyochezwa Aprili 27 hivyo wamerejea Bongo wakiwa na kazi nyingine kusaka ushindi kwenye mechi za anga la kimataifa hatua ya fainali.
Simba SC itacheza fainali dhidi ya RS Berkane ya Morocco itaanzia ugenini Mei 17 na fainali ya pili itakayoamua mshindi wat aji la Kombe la Shirikisho Afrika itapigwa Tanzania itakuwa ni Mei 25.

