Ateba kimataifaAteba kimataifa

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kimetinga hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kufikisha jumla ya pointi 10 katika kundi A ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho kimataifa.

Kwenye mchezo dhidi ya Bravos baada ya dakika 90 ubao umesoma Bravos 1-1 Simba ukiwa ni mchezo wa tano Simba kucheza na kupata bao kwa kuwa kila mchezo walioshuka uwanjani walikuwa na rekodi ya kufunga iwe ni ugenini ama nyumbani.

SHUTI la Ateba
Mpira uliopigwa na Ateba wa Simba ukizama kwenye nyavu za Bravos kimataifa. Source: Simba.

Ni mshambuliaji Leonel Ateba amefunga bao dakika ya 69 akisawazisha bao walilofungwa Simba kipindi cha kwanza na nyota wa Bravos Abdenego dakika ya 13.

NAMNA SIMBA WALIVYORUHUSU KUFUGWA

Kwenye mchezo dhidi ya Bravos, Simba ilifungwa dakika ya 13 kutokana na makosa ya safu ya ulinzi ya Simba hasa kwenye pasi za mwisho ambapo tatizo lilianzia kwa kiungo mkabaji Yusuph Kagoma kutoa pasi mkaa iliyopokelewa  na beki Che Malone naye akatoa pasi mkaa kuelekea kwa Moussa Camara.

Kabla haijafika kwa mlinda mlango Camara, Abdenego alifanya kazi yake ndani ya uwanja kwa kufunga bao la uongozi mapema na kuwafanya Simba kukomba dakika 45 za mwanzo wakiwa nyuma kwa bao hilo ugenini.

Kwenye mchezo wa kimataifa kipindi cha kwanza ziliongezwa dakika tatu na kipindi cha pili ziliongezwa dakika 5 hivyo ni dakika 8 ziliongezwa katika anga la kimataifa.

Kiungo Yusuph Kagoma ambaye alianza kikosi cha kwanza alikwama kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo uliokuwa na ushindani aligotea dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na Mavambo.

Ateba ambaye alifunga bao kwa Simba akitumia pasi ya Shomari Kapombe naye hakusepa na dakika 90 licha ya kufunga bao moja dakika ya 69 likiwa ni bao lake la kwanza hatua ya makundi aligotea dakika ya 88 nafasi yake ikachukuliwa na Mashaka Valentino.

MATOKEO YA LEO KIMATAIFA

Yusuph Kagoma
Yusuph Kagoma kiungo mkabaji wa Simba 2025. Source: Simba.

Kundi A lilikuwa kazini ambapo kila timu ilikuwa inasaka pointi tatu ndani ya uwanja na matokeo yakawa namna hii:-Bravos 1-1 Simba, bao la Bravos ni Abdenego Mosiathlaga alipachika dakika ya 13 na kwa Simba ni Leonel Ateba dakika ya 69, wababe hawa wamegawana pointi mojamoja baada ya dakika 90.

CS Costantine 3-0 CS Sfaxine mabao ya Zakaria Benchaa dakika ya 30, 70 na bao la jioni likifungwa na Mounder Temine dakika ya 90+4 likiwapa pointi tatu wababe hao wakisepa na ushindi mbele ya wapinzani wao kimataifa.

HUU HAPA MSIMAMO

Msimamo wa kundi A kwa sasa upo namna hii:- Costantine vinara wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 5, Simba nafasi ya pili pointi 10, Bravos nafasi ya tatu pointi 7 huku Faxine nafasi ya nne haijakusanya pointi.

Faxine ndani yah atua ya makundi haijakusanya pointi hata moja katika mechi zake zote uwanjani ilipoteza ina kete moja ya mwisho dhidi ya Bravos ambayo imegawana pointi moja dhidi ya Simba.

Simba ni mabao sita safu ya ushambuliaji imefunga na kinara wa utupiaji ni Jean Ahoua mwenye mabao mawili saw ana Kibu Dennis ambaye ametupia mabao mawili pia kwenye anga la kimataifa.

KIKOSI KAZI MBELE YA BRAVOS

Leonel Ateba
Leonel Ateba mshambuliaji wa Simba alianza kikosi cha kwanza kimataifa dhidi ya Bravos. Source: Simba.

Moussa Camara alianza kikosi cha kwanza alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86 ambapo aliokoa hatari dakika ya 34, 45, 46, 66, 83, Fabrince Ngoma, Jean Ahoua hakusepa na dakika 90 kwenye mchezo wa leo nafasi yake ilichukuliwa na Chamou dakika ya 88, Shomari Kapombe alitoa pasi ya bao dakika ya 69.

Leonel Ateba alifunga bao moja na alikomba dakika 88 nafasi yake ilichukuliwa na Valentino Mashaka, Hamza Jr, Zimbwe Jr, Che Malone alitoa pasi mkaa dakika ya 13, Yusuph Kagoma hakukomba dakika 90 kwenye mchezo wa leo nafasi yake ilichukuliwa na Mavambo dakika ya 45.

Elie Mpanzu hakukomba dakika 90 ugenini mwamba huyu wa Simba aligotea dakika ya 52 nafasi yake ilichukuliwa na Ladack Chasambi, Kibu Dennis alifanya kazi kubwa kusaka ushindi na alikuwa na jukumu la kupiga faulo ambazo hazikuzaa matunda ugenini.

Share this: