
JANGWANI kumekucha wanatemwa 2024/25 nyota wa kikosi hicho kwa kuwa hakuna jambo dogo kutokana na mpango mkubwa kusuka kikosi kazi kwa msimu mpya ujao. Mabingwa hao wa ligi msimu wa 2023/24 wakiwa wametwaa taji la ligi baada ya kufikisha pointi 71 na ilikamilisha msimu ikiwa na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa amesema kuwa kikosi kipya kijacho kitakuwa kwenye ubora mkubwa zaidi ya kilichotwaa ubingwa wa ligi na CRDB Federation Cup kwenye fainali dhidi ya Azam FC iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya tatu.
“Kikosi kijacho ndani ya ligi ninaamini kwamba kitakuwa bora zaidi ya kilichopita. Unaona huu ubora wa Yanga ambao ulikuwa bado kutakuwa na maboresho makubwa hivyo ni jambo la kusubiri.”
Tetesi zinaeleza kuwa kuna nyota ambao watatemwa ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi kutokana na sababu mbalimbali. Wapo ambao wataboreshewa mikataba yao ikiwa ni pamoja na kiungo mshambuliaji Aziz KI, Djigui Diarra ambaye ni kipa. Hapa tunakuletea baadhi ambao wapo kwenye hatihati ya kuachwa mazima na timu hiyo yenye maskani yake Jangwani.
JANGWANI METACHA HATAKUWEPO

Metacha Mnata kipa wa Yanga inaelezwa kuwa ni miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye orodha ya kupewa Thank You ndani ya kikosi cha Yanga hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi msimu wa 2024/25.
Yanga inayodhaminiwa na SportPesa imetwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2023/24 na pia ina taji la CRDB Federation Cup ilitwaa tuzo ya timu bora ndani ya msimu uliogota mwisho Mei 28.
Ikumbukwe kwamba mataji hayo Juni 12 2024 yalikuwa ofisi za SportPesa Tanzania Masaki Peninsula house karibu na Coco Beach ambapo mashabiki walipata fursa ya kupiga picha na mataji yote mawili kwa mpango kazi uliokuwa unakwenda kwa hashtag #SportPesaSelfikaKibingwa
Mnata hakuwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu na wakati wakikabidhiwa medali mabingwa hao kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tabora United, Uwanja wa Mkapa hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga.
OKRA MAGIC

Okra Magic kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni raia wa Ghana anatajwa kuwa kwenye orodha ya wale ambao watasepa kwenye kikosi hicho. Okra hajawa kwenye mwendo bora ndani ya Yanga ambapo alitambulishwa kwenye dirisha dogo la usajili.
Anatajwa kwamba hatakuwa katika kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2024/25. Ikumbukwe kwamba Okra aliwahi pia kucheza Simba msimu wa 2023/24 hajawa na nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Yanga.
GIFT FRED
Beki wa kazi Gift Fred anatajwa kwamba anaweza kuondoka Yanga hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu wa 2024/25. Beki huyo awali ilikuwa inaelezwa kwamba kwenye dirisha dogo la usajili alikuwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo mpango huo ukakwama.
DENNIS NKANE
Wonder Kid, Nkane zama za Miguel Gamondi hajawa na nafasi kikosi cha kwanza. Anatajwa kuwa hatakuwa kwenye kikosi cha mabingwa wa ligi msmu wa 2023/24 wakiwa wameliza msimu na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30.
KENNEDY MUSONDA
Musonda ambaye atakubwa kuwa nyota aliyefunga bao la ushindi kwenye fainali ya CRDB Federation 2023 dhidi ya Azam FC anatajwa kuwa atasepa ndani ya kikosi cha Yanga.
Mshambuliaji huyo alifunga bao hilo Uwanja wa Mkwakwani, Tanga dakika ya tatu lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. Ni shuhuda kwa mara nyingine wakitwaa taji hilo mbele ya Azam FC 2024 kwenye funga msimu Zanzibar waliposhinda kwa penalti 6-5.
SAKATA LA KUFUNGIWA NA FIFA

Timu tano zimeingia kwenye orodha ya kufungiwa kufanya usajili kutokana na kushindwa kuwalipa wachezaji ambao wanazidai ndani ya Bongo na wakashinda kesi zao. Dirisha la usajili lilifungiliwa Juni 15 2024 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 kwa timu za Ligi Kuu Bara NBC, Championship, First League na Ligi ya Wanawake Tanzania.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza namna hii: “Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezifungia klabu zifuatazo kusajili mpaka zitakapowalipa wachezaji wanaozidai.
“Yanga, Singida Fountain Gate FC, Tabora United FC, Biashara United FC na FGA Talents FC. Taarifa hiyo imeeleza kuwa klabu ambayo itawalipa wahusika, itaondolewa mara moja adhabu ya kufungiwa kusajili.”
Hivyo ili timu hizo tano ziendelee na mpango kazi wa kufanya usajili ni lazima zikamilishe malipo ya madeni wakati wowote wakikamilisha wataruhusiwa kufanya usajili.
TABORA UNITED BADO WAMO
Tabora United bado ina uhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa play off dhidi ya Biashara United ya Mara iliyokuwa inapambania nafasi ya kupanda ndani ya ligi.
Ipo wazi kwamba Tabora United mchezo wa kwanza wa mtonao ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mchezo wa pili ikiwa nyumbani iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo jumla inakuwa Tabora United 2-1 Biashara United.
Katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania zote zilizokuwa zinashiriki ligi Tabora United ilipoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 4-0 hivyo JKT Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini ilijihakikishia nafasi ya kubaki kwenye ligi kazi ikabaki kwa Tabora United.
Timu mbili pekee zimeshuka hizo zitashiriki Championship ikiwa ni Mtibwa Sugar ya Morogoro na Geita Gold ambayo funga kazi yake ilishuhudia ubao ukisoma Geita Gold 0-2 Azam FC na mwamba Feisal Salum alifunga bao moja akifikisha mabao 19 ndani ya ligi.

