- Maumivu makali wanayopitia yana mwisho wake wanaamini unyamani
- Dakika 180 mateso matupu mbele ya Yanga ndani ya Kariakoo Dabi
- Mwamba Aziz KI anawapa mateso mwanzo mwisho ndani ya uwanja
MAUMIVU wanayopitia Simba ndani ya msimu wa 2023/24 yamemuibua Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ambaye ameweka wazi kuwa kila kitu kitakuwa sawa kwa kuwa wanaamini maumivu hayo yatagota mwisho.
“Maumivu ambayo tunapitia kwa wakati huu tunaamini kwamba yatafika mwisho na furaha inakuja. Kweli matokeo ambayo tunapata sio mazuri lakini muhimu kuwa na mshikamano katika nyakati hizi zote,”

.
Ipo wazi kuwa mwendo wa timu hiyo haujawa kwenye ubora kutokana na kushindwa kupata matokeo katika mechi za ushindani ambazo walicheza ndani ya uwanja katika msako wa pointi tatu muhimu.
Kwenye Ligi Kuu Bara ilitoka kupoteza kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga uliochezwa Aprili 20 2024 Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 2-1 Simba.
HAWA HAPA WATUPIAJI
Kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Yanga inayodhaminiwa na SportPesa ilianza kupata bao mapema dakika ya 20 kupitia kwa kiungo mshambuliaji Aziz KI ambaye amekuwa akiwafunga Simba mara kwa mara wanapokutana kwenye mechi za ushindani.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 5 2023 aliwafunga bao moja kati ya matano ambayo Yanga ilifunga.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa pili alipachika bao moja kwa mkwaju wa penalti iliyomshinda mlinda mlango Ayoub Lakred ilikuwa dakika ya 20 baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa faulo na beki Hussein Kazi.
Lile bao la pili lilifungwa na Joseph Guede ilikuwa dakika ya 39 akitumia pasi ya mwamba Maxi Nzengeli ambaye alikuwa kwenye ubora wake ndani ya uwanja kutimiza majukumu ya timu hiyo.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Simba lilifungwa na Michael Fred ilikuwa dakika ya 73 akitumia pasi ya Clatous Chama ambaye ni kiungo mwenye mwendo mzuri ndani ya Simba kwa upande wa rekodi za pasi za mabao ya mwisho.
Chama kafikisha jumla ya pasi saba ndani ya ligi kwa msimu wa 2023/24 akiwa ni namba moja kwa nyota wenye pasi nyingi kwenye kikosi cha Simba ambacho kitashiriki mashindano ya Muungano.
MAUMIVU DAKIKA 180
Ndani ya dakika 180 kwenye ligi ilikuwa ni maumivu kwa Simba mbele ya watani zao wa jadi Yanga kwa kuwa kila walipokuwa ndani ya Uwanja wa Mkapa dakika 90 ilikuwa kicheko kwa Yanga na maumivu kwa Simba.
Simba imefungwa jumla ya mabao saba huku wao wakifunga mabao mawili pekee ndani ya uwanja kwenye mechi za ligi ambazo zilikuwa na ushindani mkubwa mwanzo mwisho.
Yanga inayodhaminiwa na SportPesa imekuwa kwenye mwendo mzuri kuanzia safu ya ushambuliaji na ulinzi wa kutosha ndani ya uwanja kutokana na kuruhusu mabao machache.
Yanga imeruhusu mabao mawili pekee huku Simba ikiruhusu kufungwa jumla ya mabao saba ndani ya dakika 180 hivyo maumivu ni kwenye kukosa pointi pamoja na kuambulia mabao mengi kwenye Kariakoo Dabi.
AZIZ KI NENO LAKE

Mwamba Aziz KI ambaye ni kinara wa utupiaji ndani ya ligi akiwa na mabao 15 kibindoni amebainisha kwamba kikubwa ni kuona wanakuwe kwenye mwendo mzuri na kupata matokeo uwanjani kwa kuwa kila mmoja anaonyesha ushirikiano mkubwa.
KI kwenye ligi kafunga jumla ya mabao 15 na mawili kawafunga Simba msimu wa 2023/24 ambao umekuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja wakisepa na pointi sita za Simba mazima.
“Hakuna ambacho tunafurahia kwenye mechi ambazo tunacheza zaidi ya kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu ipo hivyo kwa kuwa kila mchezaji anapenda kuona tunapata matokeo mazuri.
“Ambacho ninafurahia ni kuona kila mmoja anapata matokeo mazuri ipo hivyo na wachezaji tunashirikiana kuona kwamba kila mchezaji anaona tunafikia malengo yetu ambayo tunaamini itakuwa hivyo.
“Bado kazi inaendelea kutokana na mechi ambazo tunacheza ndani ya uwanja na ipo hivyo ni muda wa kuendelea kupambana kupata matokeo mazuri , mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi ambazo tunacheza muda ni sasa katika kupambania malengo yetu,”.
